Ni kipi kifanyike ili kuondoa wizi maofisini na katika mashirika ya Kiserikali?

Mtu anapitisha malipo ya mamilioni,mabilioni ama trillions afu uhakika wa pesa yake ni wa kusuasua?.
Kuna kada ziboreshewe maslahi ili kupunguza tamaa na rushwa
 
Kazi ziwe za mikataba ya muda maalum ambayo inaweza kuongezwa kwa awamu kutokana na utendaji wa mtu husika kwa kutimiza malengo na mipango ya ofisi au taasisi. Malipo mazuri ya kutosha huku mtu anapo ajiriwa lazima atangaze mali zake,kabla ya kurefusha mkataba lazima afanyiwe ukaguzi wa mali zake tena.
 
Ndio maana nikasema 'michakato ya wazi'.
Interviews zifanywe hadharani kukiwa na vyombo vya habari live.
Sio wabunge wote ni wala rushwa.
Bahati mbaya kabisa hao wabunge pia ni Wala rushwa
 
Mkuu, asante Kwa maoni yako, tunachotaka ni kutaka kukomesha kabisa uwizi, haijarishi fisadi ama mkwapuaji, ila tunataka tutoke hapa tulipo
Kama rais mwenyewe anaingia madarakani kwa wizi wa kura, na bunge zaidi ya nusu wako bungeni kama zao la wizi wa kura, unategemea huko maofisini wizi uishe?

Cha muhimu kuwa na taasisi imara, sio kuwa na mtu mwenye maamuzi yote ya nchi, lakini anapatikana kwa wizi wa kura na hawezi kushitakiwa. Kila mtu akishitakiwa, ndio tutaanza kuona wizi ukiisha maofisini.
 
Mkuu, ukipunguza jaziba, unaweza kusaidia ktk hili
 
Mshahara hautakaa utoshe. Tuache visingizio vya ajabu ajabu.
Mtu anasimamia projects za billions of money ila mshahara wake haueleweki..tunategemea nini?.

afu kuna watu kupiga meza tu wanaondoka na millions of money..kuna kitu hakipo sawa
 
Mahitajo ya mwanadamu hayajawai kufika ukomo...!! Kama ao mafisadi au wakwapuaji ata uwape mshahara wa milion 3 kwa mwezi na marupurupu kibao kama mwizi ataendelea kuiba tu ila shida ya watanzania hatuwapendi watu wanyoofu sie tunawaita wanoko...!!
 
Sheria ya mwizi akatwe mkono inaweza ikasaidia??

Kumbe China wananyonga kabisa sio??
 
Mzee baba kama mtu alikuwa anawafukuza kazi hadharan akaambiwa hazingatii sheria na haki za binadamu je uko kunyonga...!!!
 
Mkuu, ukipunguza jaziba, unaweza kusaidia ktk hili
Mkuu hayo ni maoni yangu, ama ulitaka nianze na ishara ya msalaba? Isije ikawa umeanzisha uzi lakini tayari una majibu mfukoni.
 
Kuna jamaa mmoja anahoja, Anasema, Ninyi wa sasa haoni Kazi yenu, Kwanza nyinyi ni wachochezi Sana, halafu mnalipwa pesa nyiiingi, miaka mitano bungeni marupurupu ni mara nne ya Mwalimu mstaafu
 
Inatia faraja sana kuona Mataga nao wameacha kuabudu na wanaungana na Wapinzani katika kutafuta solution, Nchi hii itajengwa kwa kuambiana ukweli.

Wapinzani sio maadui, wala sio Vibaraka wa Mabeberu Wapinzani ni watu Wema sana kwa Taifa hili.
Achana na habari za wapinzani banah..!! Mna kashfa ngap huko za ukwapuaji wa fedha hapo Ufipa..? Tunajadiliana kama Watanzania.
 
Mkuu hayo ni maoni yangu, ama ulitaka nianze na ishara ya msalaba? Isije ikawa umeanzisha uzi lakini tayari una majibu mfukoni.
Mkuu naheshimu maoni yako, Ila nilikuomba upunguze tu kidogo jaziba, huwa nakuelewaga Sana mkuu kwenye mijadala kama hii
 
Mzee baba kama mtu alikuwa anawafukuza kazi hadharan akaambiwa hazingatii sheria na haki za binadamu je uko kunyonga...!!!

Unamfukuza mtu kazi hadharani kusaka political millage, wakati huo huo kuna viongozi wako wengine kibao wanafanya kinyume cha sheria, na huwachukulii hatua yoyote. Peleka mtu mahakamani sheria ichukue mkondo wake. Sasa unamfukuza kazi mkurugenzi kwa kushindwa kusimamia fedha za umma, kisha wakati huo huo unatumia wakurugenzi wengine kuiba kura na kunajisi uchaguzi, kama sio utani huo ni nini?
 
Achana na habari za wapinzani banah..!! Mna kashfa ngap huko za ukwapuaji wa fedha hapo Ufipa..? Tunajadiliana kama Watanzania.

Wenye kashfa regardless wako wapi wachukuliwe hatua, sio unamfukuza wenye vyeti fake, kisha unasimama hadharani unasema mwingine aendelee na kazi hata kama ana division 0, kwakuwa unaangalia uchapa kazi. Katika mazingira hayo utaungwa mkono na wajinga. Kwa mtazamo wako wapinzani sio watanzania, au bado uko kwenye hangover ya siasa za kishenzi za jiwe?
 
Hivi mjadala umeulewa kweli? Yani watu wanashauri ikiwezekana atakaeiba akatwe mkono we unazungumzia kumfukuza kazi kwenye umati wa watu? Tuambie tufanye nini kama Taifa? Usilete visingizio vya ajabu hapa...!!

Hapo Ufipa pia kuna wizi na ubadhilifu wa mali za uma..!! Sasa kama Taifa ili tujikwamue hapo tufanye nini?
 
Kuna jamaa mmoja anahoja, Anasema, Ninyi wa sasa haoni Kazi yenu, Kwanza nyinyi ni wachochezi Sana, halafu mnalipwa pesa nyiiingi, miaka mitano bungeni marupurupu ni mara nne ya Mwalimu mstaafu

Sijawahi kuunga mkono wabunge kulipwa mshahara wa zaidi ya 3m, tena kwa kwenda bungeni kuleta mipasho.
 
Pole mkuu, naona uliathirika vibaya Sana aisee
 

Nasema hivi, sheria za wizi ziko wazi, mtu mwizi peleka mahakamani ashitakiwe. Tena mngeanza na hapo Ufipa kisha mmamlizie kwa Wazalendo uchwara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…