Hoho lina tako wewe utakuwa kama ndimu
Mi enzi hizo za kuishi na msichana wa kazi bhana nikapataga mmoja giant linanizidi urefu na mwili kumbe alijua anakuja kufanya job za shamba, sasa kuja anakutana na shughuli za ndani ndogo ndogo nyumba ina tiles za kioo, kumbe nilipokuwa nikitoka ni mwendo wa kuteleza na kula mweleka nikirudi hasemi mopa na mifagio kavunja yote! 😅😅 wakati huo mi mwnyw kidogodogo tu sikuelewa siku nikapeleka samaki dah dada akawapika hivyo hivyo bila kukwangua magamba wala kutoa utumbo nikaanza kulalamika alivyoharibu mboga eeeeh si ndo kuniambia yeye amechoka kwanza nyumba ina majini yanamuangusha kila siku nataka kumtoa kafara, mara nilijua kuna kazi za shamba, nikasema yesheyesheee tunafanyaje sasa akasema nimpe chake aende, sikubishana nae alikuwa na wiki 2 nikamlipa akaondoka ila ndo alijipodoa km anaenda kufunga ndoa😅😅😅 tangu hapo niliacha kuishi na maids mpaka leo ila nitamtafuta tena hivi karibuni