Ni Kisa/ kituko gani uliwahi kufanyiwa na Dada wa kazi?

Nilimkuta kwa ndugu nilifikia, nikaomba mchezo nikapewa, jioni mezani akanipakulia msosi kwenye pot tofauti na alilowekea wengine kwangu kajaza nyama nyingi na viazi, ilikua kapika ndizi, bahati nzuri nilikua wa kwanza kwenda mezani nikatoa nikarudisha jikoni sikuongea nae ila hakurudia tena🀣
 
Aliifinyia kwa ndani Hadi nikajutaa
 
Hoho lina tako wewe utakuwa kama ndimu


Mi enzi hizo za kuishi na msichana wa kazi bhana nikapataga mmoja giant linanizidi urefu na mwili kumbe alijua anakuja kufanya job za shamba, sasa kuja anakutana na shughuli za ndani ndogo ndogo nyumba ina tiles za kioo, kumbe nilipokuwa nikitoka ni mwendo wa kuteleza na kula mweleka nikirudi hasemi mopa na mifagio kavunja yote! πŸ˜…πŸ˜… wakati huo mi mwnyw kidogodogo tu sikuelewa siku nikapeleka samaki dah dada akawapika hivyo hivyo bila kukwangua magamba wala kutoa utumbo nikaanza kulalamika alivyoharibu mboga eeeeh si ndo kuniambia yeye amechoka kwanza nyumba ina majini yanamuangusha kila siku nataka kumtoa kafara, mara nilijua kuna kazi za shamba, nikasema yesheyesheee tunafanyaje sasa akasema nimpe chake aende, sikubishana nae alikuwa na wiki 2 nikamlipa akaondoka ila ndo alijipodoa km anaenda kufunga ndoaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… tangu hapo niliacha kuishi na maids mpaka leo ila nitamtafuta tena hivi karibuni
 
Bora ulivyomuacha aende maana angekupiga makonzi na hivi ni supertall πŸ˜‚πŸ˜‚

Tafuta vijeba vifupi unaviendesha tu unavyotaka jamani...

Kupigwa makonzi na afisa ulezi inahusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…