Ni kitanda gani kizuri; mbao, chuma au sofa?

Ni kitanda gani kizuri; mbao, chuma au sofa?

Kitanda Cha chuma kitafaa hasa ukiwa unacheza mechi za nyumbani dhidi ya mama watoto F.C 😳👀
 
Wenzangu wa kwenda na fashion mpo!! Mi habari ya kudumu miaka mingi wala sielewi. 😂😂😂
Yaani nitengeneze kitanda Cha kudumu miaka 20, wakati fashion zinabadilika kila uchwao
 
Kanunue cha mbao mkuu
Hakiishi fashion na ni imara
Hongera sana
95cce8f71ead9a7810c3a8a3955b8ad0.jpg
418f5a447ea42b77dcda524af978ec7b.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kitanda gani kizuri na sifa zake nikanunue

Hatimaye kama nilivonuia kwamba mwezi wa tisa hautaisha bila kuwa na kitanda ni karibia mwaka Sasa Mm na mama mtoto wangu tunatupa godoro yetu chini asanteni

Wote mlionipa matumaini tokea siku ya kwanza nilipolalia mabox

MUNGU ASIFIWEEEE
Ukipata cha chuma kiwe na sofa n unyama sana hapo zinapigwa ligi zote ndondo hadi premier league kama n mbao chukua mninga level ya epl hio hio m bedi sofa mingi wanachakachua mechi za mtoano tuh kufuzu makundi hakifai kitachakaa hicho n kwa ajil ya mapumziko nje ya msimu
 
Mbao haitokua na mpinzanii,
Chuma kikianza kulika kwenye maungio ni kelele tuu,
Sofa ndio kabisaa, kuchanika, kuchafuka, kufubaa, bado hujataja uimara na mbao za hovyo zilizofunikwa na kitambaa....

Kua makini na mbao za sikuhizi wanazoita mbao ngumu, mbao inapewa jina mfano Mninga, mkongo n.k, akisema mbao ngumu tuu shtuka.
Hayo ni ma play wood, MBF ya kichina likiingia maji unaokota pumba chini.

NOTE : Epuka furniture iliyopigwa Rangi kabla hujaona mbao yenyewe.
Best option ni kwenda kwa wauza mbao nunua Kwa mahitaji ya kitanda chako then muite fundi atengeneze hapo kwako hapo hutaibiwa
 
Cha mbao ni balaa zikiingia kunguni kama vita ya Drc!
Kama joiner hayupo makini kinaingiza kunguni kwenye mazingira machafu lakini mbao ni fashionable haipitwi na wakati kama chuma, nakumbuka zamani vilikuwepo vitanda vinaitwa Banco viliwika sana miaka ya 70s vikafutika sasa vimekuja vya square na round pipes finishing yake siyo nzuri
 
Back
Top Bottom