Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Ila taarifa kutoka Kenya zinasema jamaa yuko Kuwa train askari wa Kenya, ila siku ilipotokea tukio na yeye alikuwepo hapo kama wateja wengine tu sasa magaid walipolianzisha ikabidi aende kwenye gari yake na kuchukua vifaa kwa ajili ya mapambano maana inasemekans popote anapoenda anakuwa full equipped.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuweka point vizuri, kama wengine walivyosema, huyo mwanajeshi anawafanyia mafunzo special unit ya Kenya. Anatokea Uingereza. Uingereza na Kenya wanaushirikiano wa karibu sana kwenye mafunzo ya kijeshi, hata mwaka jana mtoto wa malkia wa Uingereza aliwatembelea wanajeshi wenzake waliokuwa wanafanya mafunzo ya pamoja alipoitembelea Kenya.

Kuwa kwake pale ni kwa sababu walioitwa ni wanafunzi wake na kama ujuavyo wanajeshi marafiki huwa wana umoja Sana. Sio kweli kwamba alikuwa kwenye eneo la tukio kabla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo yupo kwa ajili ya training kwenye Kenya special forces
Nilisoma kwenye gazeti la Mirror UK wanavyo msifia ni balaa
Jamaa lilimkuta tu tukio hilo akiwa na mambo yake ndipo akarudi kwenye gari lake ambapo zana zake zilikuwa humo.
Akavaa na kuchukua silaha na kuanza kutoa maelekezo kwa jeshi la kenya
Yaani jamaa alishika usukani mpaka anamaliza mission


Sent from my SM using Tapatalk
 
Recce ni kikosi ndani ya GSU. Vikosi vya Recce na flying squad vinafahamika kwa raia. Na nilazima watu wafahamu hivi vikosi kwa sababu ya kujenga hofu kwa wabaya wa nchi na majambazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka mbali na watoto.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unavyosema Navy Seals hawako fit kihivyo mimi ndiyo napata ukakasi kabisa. Maana historia inatuambia kwamba Navy Seals walianzishwa baada ya Delta Force kuonakana haifanyi vizuro kwenye baadhi ya maeneo. Mathalani, nadhani katika dunia hii ya leo vifaa mbali na mazoezi ni moja ya sababu ya kikosi kuwa imara. Hivi kuna kikosi cha makomandoo ambacho kina vifaa vya ajabu kama Navy Seals ? Mwanajeshi wa kawaida wa Marekani akiwa amevaa full gear siyo chini ya milioni 40 za kitanzania (Do your research). Hapa ndipo wanapokuwa mbele ya vikosi vingine duniani.

Lakini sasa nakubaliana na wewe kwamba SAS ni hatari kwenye mambo mengi kwasababu tofauti kabisa na kikosi kingine chochote cha makomando hapa duniani SAS ndicho kikosi kilichopigana vita ya pili ya dunia na kufanikiwa kuonyesha umahiri wa hali ya juu sana.

SAS is ana amalgamation of multiple military units that were under the shadow of the British Empire. Wanahistoria wanasema hivi, Uingereza kama lilivyokuwa dola la Mrumi alikuwa akivamia nchi na kikuta kwamba kuna vikosi vyenye ustadi mkubwa wa kupigana. Alikuwa anachukua ujuzi huo na kufundishia jeshi lake. Alifanya hayo mambo Scotland ambako wanajeshi wake walikuwa wanajua sana vita vya msituni, hapa akatengeneza the Levat Scouts. Akafanya hivyo British India ambako wanajeshi wa Nepal na India wale walikuwa na utaalamu wa pekee sana na Uingereza akatengeza The Ghurkas.

Baada ya kuwatwanga makaburu kule Afrika Kusini, Uingereza alishangazwa sana na ujuzi wa makomando wa kikabiru. Akaamua kuuchukua na kujifunza, vita ya kwanza ya dunia inatokea. Makomando wa Kikaburu ndiyo walitumiwa kuja kupigana na Mjerumani hapa Afrika Mashariki, Namibia na sehemu nyingine. Tafuta kitabu kinaitwa The Boer Commando.

Mwaka 1941 Winston Churchill alipowa mapendekezo ya kuanzisha SAS na wataalamu walishauri kwamba, kikosi hiki kiwe kinaunganisha utaalamu wa vikosi vyote ambavyo Uingereza aliwahi kuvianzisha huko nyuma. SAS ni mchanganyiko wa Ghurkas, Levat Scouts, Boer Commandos na vinginevyo.

Wanautaalamu wa hali ya juu sana, lakini hili halifai kusema kwamba Navy Seals hawana uwezo. Laiti kama Osama Bin Laden angekuwa anaongea basi angalisema hili. Japo siku hizi tena Marekani anatumia kikosi kinaitwa JSOC ambacho kinasemekana kuwa ndiyo hatari zaidi katika kushughulikia maadui wa Marekani. Afghanistani wanasema hiki kikosi kimewashughulikia sana Taliban hadi basi. Ni zao la zao la Jasusi+Ukomando...

Wenyewe hawataki kabisa kizungumziwe hata na vyombo vya habari....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kenya walikuwepo SAS, US navy seal na wengine. Tunashukuru tukio limeisha, poleni wafiwa.

Hero SAS soldier and US Navy Seals 'helped battle Islamist terrorists attacking Kenyan hotel' | Daily Mail Online

Hero US Navy SEALs stormed Kenyan hotel and exchanged fire with Islamist terrorists | Daily Mail Online
 


Upo sahihi, ndio best of the best, Crème de la crème,

USA, Israel, wamejifunza hapo.
 
Au za kule Comoros mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwepo au umeadithiwa mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poa mkuu basi kikosi bora Simba Sports Club. Kikosi kipana. Happy?!
 
Nani amekudanganya kwamba hao magaidi waliuwawa ama kuzibitiwa?wakenya wanacheza movie zao kama ule uongo wa jeshi kuwadhiti magaidi kwenye tukio LA westgate
Kwahiyo mkuu tusiwaamini waliokuwa kwenye tukio wanaosema magaidi wameuwawa tukuamini wewe ambae uko Tandale Kwa Mtogole muda huu?!
 
Jamani kabla hamujaleta uzi mfanyege research kujua sababu ya hao watu kuwepo Katika eneo la tukio.

Kenya kuna kikosa kidogo cha hao jamaa kutrain wanajeshi Kenya. Kilichofanyika walienda kuwasaidia wanafunzi wao sababu kuna Waingereza na Wamarekani Wahanga pia.

Al shabab ni tishio kubwa hivyo wanawasaidia wakenya kupambana nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…