Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Kwa kuwa sasa nimekuwa mtu mzima, nimegundua kuwa nimekuwa na bajeti kali, hasa linapokuja suala la vitu vya kupikia. Nakumbuka zamani nilivyokuwa nikigombana na mama kuhusu matumizi ya mafuta ya kupikia; mara nyingi nilikuwa naweka mafuta mengi kwenye chakula, na kama yakizidi, nilikuwa nachuja na kumwaga yaliyosalia. Mama alikuwa akilalamika kwamba mafuta yanaisha haraka. Lakini tangu nilipoanza kujitegemea, imekuwa nadra sana kwa chakula changu kuwa na mafuta ya ziada.
Ni kitu gani ulikuwa unatumia hovyo kipindi bado unaishi Nyumbani ila sasa umekuja kujua ni bei?
Ni kitu gani ulikuwa unatumia hovyo kipindi bado unaishi Nyumbani ila sasa umekuja kujua ni bei?