Mi nadhani waliojibu wako sahihi, Hata wewe pia huenda ukawa sahihi.
Mkuu ameuliza : Ni kitu gani kilichokufanya uwe addicted nacho?
Swali limelenga "Vitu" au "Mambo" sio cause ya hivyo "Vitu" au "Mambo".
Hili swali linaweza kujibiwa katika namna tofauti, mfano;
•Vitu vya kawaida: Chakula, vinywaji, au michezo.
•Tabia: Kuangalia televisheni, mitandao ya kijamii, Video za ngono au kucheza michezo ya video.
•Vitu vya hatari: Dawa za kulevya, pombe, au sigara.
Swali hili siyo tu linataka kujua chanzo cha uraibu, bali pia linataka kuangazia jinsi ulivyojikuta ukihusiana na jambo hilo, ni kwa kiwango gani limeathiri maisha yako, au sababu ya kuendelea kulifanya.