Waamuzi 13:4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
Au unasema hapa Mtume Paulo alipomshauri Timotheo👇
1 Timotheo 5:23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara....
Msipotoshe Wakuu..kama ni Pombe ,kunyweni tu kama ilivyo Uzinzi .
Wakiristo wa zamani walifanya huduma za dhati za kufunga bila kula huku wakisafiri umbali mrefu kupelekaa injili.
Lkni pia DIVAI ,ilitumika kama Dawa kutibu magonjwa .... Kasome Luka 10:33-34 kisa Cha Msamaria, alipomkuta mtu njiani hajiwezi ( anaumwa) mwili una vidonda, aliamua kutumia DIVAI kumpaka kwenye vidonda, yaan DIVAI ni kama ilivyo Hydrogen Peroxide au kama Iodine
Sasa , Timotheo ambaye alikua amefunga akinywa maji tu uku akitembea umbali mrefu kumtangaza injili , mwili wake ulidhoofu na wanatheolojia wanaelezea kua alianza sumbuliwa na tatizo la tumbo kuuma na kudhoofu.
Ndipo Mtume Paulo, anamshauri Timotheo,. Usinuwe maji tu, "Bali na Divai kidogo" ili huo Divai uende kua Dawa Kwa Timotheo na kumponya.
HAKUA NA MAANA YA KUA ,KUNYWA MVINYOOO KWA STAREHE AU KAMA SEHEM YA MAISHA YA KILA SIKU .
Kunyweni tu ila msitafute sababu za kuhalalisha, Ulevi, Biblia inamtaja mlevi kama mtu ambaye hupatwa na Kila jambo .
Ni kama ilivyo Uzinzi tu!!.
Tusihalalishe kitu, Mungu ni Mungu, hajipingi !!.