Busu la Kenge
JF-Expert Member
- Jun 13, 2025
- 2,583
- 4,776
Uliwahi kuamini ujinga gani ulipokuwa mtoto?
Tukiwa watoto, tunakuwa tunajaribu kuelewa dunia hii kubwa na yenye mambo mengi lakini tukiwa na taarifa chache sana. Hapo ndipo tunaanza kuamini vitu vya ajabu ambavyo ukivikumbuka saivi vinachekesha, lakini vina maana pia.
Labda uliwahi kufikiri mwezi unafuata gari lenu, au radi ni anga likipasuka.
Lakini haya mambo ya ajabu tuliyoamini hayakuwa tu hadithi za kuchekesha; yalikuwa njia ya sisi watoto kujenga picha ya ulimwengu kujifunza kuhusu hisia, mahusiano, na sisi ni nani.
Utafiti unaonyesha watoto hawakariri tuu uhalisia unaoonekana bali pia wanautengenezea maana zinazowasaidia kuelewa maisha.
Je wewe, ulikuwa na imani gani ya ajabu ukiwa mdogo?
Watoto wawili wa kipenzi chetu cha dhati Imam Hussain ibn Ali AS Ali Al-Sajjad ibn Hussain na Ali Al-Akbar ibn Husssain wakikimbia huku wakilia baada ya kupata habari baba yao kauliwa kikatili 😭😭😭😭😭😭Ilitakiwa wakueleweshe tu, sisi tuliamini mtoto anaokotwa chini ya jiwe kubwa ambalo liko mtoni.
Mpaka leo napendaga sana kusikiliza story za watoto wanadanganyana hadi sio poa 😂😂
adriz Mufti kuku The Infinity