Ni kitu gani kinafanya makabila mengi Tanzania kutokuwa na utamaduni wa kurudi kwao?

Kiuchumi haijakaa poa. Hata kujenga nyumba mbili mbili, mjini na kijijini haijakaa poa kiuchumi.
Kuna watu mijini wana majumba mpaka matano, wengine Magorofa, ni ajabu kushindwa kujenga a simple nice house kijijini kwenu ambako hata ukiwa haupo wazazi wako waishi conformable... Wengine huko town wamewajengea mpaka mchepuko na kununulia gari [emoji12][emoji12] ni suala la kipaumbele tuu.
 
Kwani wewe kwenu wapi jombaa mbona umepaniki sana? Take it easy, kwenu ni kwenu tuu na mkataa kwao mtumwaaa tuuu hata ubishe vipi. Muasisi wa taifa hili Nyerere, ambaye ndiye wa kwanza kuhimiza umoja kwa watanzania bado, pamoja na yoooteee aliyokuwa anafanya na kuyahimiza, alikuwa anaenda kwao Butiama mara kwa mara, na alizikwa huko. Pia JPM kila mara alikuwa anaenda kwao na amepaendeleza sana nyumbani kwake, na si yeye tuu hata Mzee wetu wa Msoga...
 
Mkataa kwao ni mtumwa,

Hii ndio sababu hilo kabila limepiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo, kurudi kwenu ni jambo zuri linalohamasisha umoja, upendo na mshikamano.

Kuna watu humu hawajui kabisa hata mila zao wala kujua asili zao
 
Huyo keisongora kinachomsumbua ni wivu tu,huyu probably kijijin kwao kenyamanyori tarime atakuwa hajajenga so he feels jelous to us leave him.
 
Tanzania mkuu
 
Kisa ukenya ama Nini,najua mkalenjini haendi kufundisha kwa wajaluo lakini.anafundisha kwao.
 
Nyerere kukataza lugha za makabila
 
We Rwanda ushafika au unaandika tu
 
Ni kweli, nyinyi wachaga ndiyo mnajitangaza kuwa mnarudi kwenu hadi kwenye magazeti,makabila kibao yanafanya hivyo hila hawana hizo mbwembwe,wewe unataka kila Kabila lijitangaze kuwa linarudi kwao kama nyinyi ambavyo mnavyofanya?
Hawana hiyo popularity ya kujitangaza,watajitangaza watu watano? Sisi ni dhahiri shairi,dar décembre foleni inapunguaga kabisa ndo uje effect yetu
 
Mkataa kwao ni mtumwa

Hii ndio sababu hilo kabila limepiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo, kurudi kwenu ni jambo zuri linalohamasisha umoja, upendo na mshikamano.

Kuna watu humu hawajui kabisa hata mila zao wala kujua asili zao
Duniani wazungu wamefanikwa sana kwa sababu ya uthubutu wa kuiacha kabisa Ulaya na kwenda kuishi kwingine duniani kwenye fursa kubwa, wameishia kuichukua Marekani Kusini na Kaskazini pamoja na sehemu kubwa ya Africa na rasilimali zake. Wewe endelea kupuyunga na kwenu tu.
 
Kurudi wanarudi lakn, huwezi waona kwasababu hawarudi kwa makundi Wala mwezi Fulani kila mwaka Kama nyumbu wanahama la hasha!
 
Watumwa waliopelekwa Jamaica warudi kwao!? Huwezi kuwa seriuos. Wanafahamu walikotoka vizazi vyao vilivyotekwa mamia ya miaka nyuma!? Au unadhani waliondoka kwa hiari yao kama unavyoamua wewe kwenda kokote utakako!?
 
Aisee, watu kwenda kwao ni ukabila!? Hii ni mpya. Porojo nyingi tu hapa ambazo zipo nje ya mada.
 
Hata huko umakondeni kuna mambo hayo. Nina machinga wenzangu huwa wananipa stori za huko. Sio poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…