Hapa kwetu Njombe
Mwez wa kumi na mbil mwaka 2021 nlikutana na binti flani
ambaye kwa macho yangu namuona mzuri Sana, nlimuelewa sana yule dada.
alikuwa anapita sana kwenye kachochoro ambako ndipo ofisi yangu ilipo.
Basi ikawa kila akipita namuangalia sana naishia kusema kesho ntamsimamisha ila akipita tena napata uoga,
Sasa wiki iliyopita nikawa nimejipanga kabisa kwamba leo lazima nimsimamishe hata niongee nae kidogo,
Ile nimekaa sina hili wala lile mtoto huyo namuona anakuja, basi mwanaume nikajitosa nkamuita.
Dada wa watu akasimama nikasogea taratibu,,
sasa hapa ndo tatizo lilipoanzia,
Nilipokuwa namkaribia nilishtuka sana, alikuwa ameshika cm mkono mmoja af mwingn kashika pochi, sasa nilipokuwa nampa mkono tusalimiane.. alinipa ule mkono wenye cm kumbe kwenye kidole kimoja alikuwa kaingiza ile ring ya funguo ambazo zilikuwa zimekaa kwa nyuma ya kiganja, mm nikawa naona cm tuu kumbe mtoto mkono huohuo kaning'iniza funguo za ndinga na remote ya BMW.
Kiukwel nlipoziona nilishtuka sana, mistari yote niloipanga kichwani ikayeyuka. Mwanaume nikakosa point kwa sababu nlianza kupata hofu kwamba mtu huyu sikumdhania kama anaweza kuwa na pesa ivoo.
Nliona nimeparamia sehem sio level yangu
Nliishia kumwambia samahan sister nmekufananisha na dada mmoja huwa anapita sana hapa.
Saivi huwa anapita ananipa hai mana nipo kwenye kabanda flan kana geti tuu so kila anapopita lazma tuonane.
Zile hisia za kumpenda zilishakata asee