Ni kitu gani ulitamani kukijaribu lakini ulipojaribu ukaapa hutakuja kurudia tena

Ni kitu gani ulitamani kukijaribu lakini ulipojaribu ukaapa hutakuja kurudia tena

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
WEKA EXPERIENCE YAKO YA JINSI KITU ULICHOTAMANI KUKIFANYA KILIVYOKUTIBUA SIKU ULIPOKIJARIBU, HUJI KURUDIA

Kuna vitu unaweza kutamani kuvijaribu lakini vinakukataa kabisa. Mfano ni vilevi, baadhi vinakubali lakini vingine vinakataa kabisa, huna budi kuviacha.

Experience yangu hii hapa

Kwa muda mrefu sana nilikuwa natamani nije kuvuta bangi, nilikuwa natamani sana kujua feeling na stimu zake, yani mtu anajisikiaje akivuta.

Msukumo huo niliupata nilivyokuwa nikiona watu hasa wasanii kwenye TV wanavyoisifia, mtaani niliona ikivutwa na hata ile harufu yake nilikuwa naipenda so nikasema "WHY NOT, LAZIMA NIJARIBU".

Siku ikafika uvumilivu ukanishinda, sikutaka kujifunza kwa mtu yeyote nikihofia wengine wanachanganya na mambo mengine, nikamfata mtu mzima kidogo wa mtaani tumezoeana, huwa anavuta lakini yupo smart, anavaa fresh, ana biashara na familia yake.

Basi nikampanga anifanyie mpango, msokoto ukawashwa, nikapiga pafu kama tano hivi )sikupata shida nimeshazoea kuvuta sigara), sikuona chochote pale nikarudi nyumbani, nilipofika nyumbani nimejilaza kwenye kitanda, moyo ukaanza kudunda kwa speed kali sana, nikapata shambulizi ya hofu (panic attack) na shinikizo la damu kupanda sana. kwenda kujiangalia kwenye kioo jicho limeiva kama nyanya, nilipaniki, nikajaribu kulala lakini wapi, ile hofu ikafanya hali iwe mbaya zaidi siwezi hata kuelezea.

Nikagundua kwamba naipenda bangi lakini bangi imenikataa, Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza na ya mwisho nikaona heri nibaki kwenye sigara na vibia
 
Back
Top Bottom