EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 10,576
- 16,644
Kuna vitu tumekua tunaogopa au kuhofia visije kutupata katika maisha yetu. Tukianza na mimi hivi ni miongoni mwa vitu ambavyo vinanisababishia hofu:
- Kupata ajali ya aina yoyote pikipiki au gari
- Kung'atwa na viumbe vyenye sumu kama nyoka, n'ge, tandu au buibui
- Kuuawa
- Kupata ulemavu wa viungo kama mikono, macho, au miguu
- Kupata maradhi kama TB, ukimwi, kisukari au magonjwa ya moyo au magonjwa ya hatari
- Kuumizwa na vitu kama visu, panga risasi au vyenye ncha kali
- Kufungwa jela
- Kupigwa na watu wanaoweza kunizidi nguvu kama askari
- Kunyang'anywa kitu changu chochote au kuvamiwa na majambazi
- Na mwisho kupoteza marinda