Ni kitu gani unahofia/unaogopa kisikupate mpaka unaimaliza safari duniani?

SULEIMAN kwenye kitabu cha MITHALI anatuambia

MITHALI 1:7
"Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."
Kabisa kwa wenye ufahamu wa kweli ukishakosa imani kwa muumba wako unakosa kimbilio na matumaini. Na Mwisho wake always ni mbaya sana Mama, Tuendelee kumuomba mungu asitufanye tumsahau yeye[emoji120][emoji120]
 
Kuna vitu tumekua tunaogopa au kuhofia visije kutupata katika maisha yetu. Tukianza na mimi hivi ni miongoni mwa vitu ambavyo vinanisababishia hofu:
  • Kupata ajali ya aina yoyote pikipiki au gari
  • Kung'atwa na viumbe vyenye sumu kama nyoka,n'ge ,tandu au buibui
  • Kuuawa
  • Kupata ulemavu wa viungo kama mikono, macho, au miguu
  • Kupata maradhi kama TB, ukimwi, kisukari au magonjwa ya moyo au magonjwa ya hatari
  • Kuumizwa na vitu kama visu, panga risasi au vyenye ncha kali
  • Kufungwa jela
  • Kupigwa na watu wanaoweza kunizidi nguvu kama askari
  • Kunyang'anywa kitu changu chochote au kuvamiwa na majambazi
  • Na mwisho kupoteza marinda
Unataka kusema nini mkuu?
 
Kupatikana na hatia na mwishowe kufungwa jela ,hili jambo naliogopa sana ukiachilia mbali kukaa lockup.

Kuugua malazi ya kukuweka kitandani kwa mda mrefu,hatari sana hii pia

Kumuasi mola wako,ni jambo baya sana ingawa watu wengi huchukulia poa,

Mwisho umasikini ,ni hatari mno ,ogopa sana kuwa masikini ,inatesa sana na kufedheesha utu wako,
 
Kabisa kwa wenye ufahamu wa kweli ukishakosa imani kwa muumba wako unakosa kimbilio na matumaini. Na Mwisho wake always ni mbaya sana Mama, Tuendelee kumuomba mungu asitufanye tumsahau yeye[emoji120][emoji120]
Amina
 
Ulemavu wa akili na viungo
Kufungwa jela
Dah naomba sana kwa Muumba wangu hayo Mambo aniepushe nayo hadi nadanchi
 
Kuna vitu tumekua tunaogopa au kuhofia visije kutupata katika maisha yetu. Tukianza na mimi hivi ni miongoni mwa vitu ambavyo vinanisababishia hofu:
  • Kupata ajali ya aina yoyote pikipiki au gari
  • Kung'atwa na viumbe vyenye sumu kama nyoka, n'ge, tandu au buibui
  • Kuuawa
  • Kupata ulemavu wa viungo kama mikono, macho, au miguu
  • Kupata maradhi kama TB, ukimwi, kisukari au magonjwa ya moyo au magonjwa ya hatari
  • Kuumizwa na vitu kama visu, panga risasi au vyenye ncha kali
  • Kufungwa jela
  • Kupigwa na watu wanaoweza kunizidi nguvu kama askari
  • Kunyang'anywa kitu changu chochote au kuvamiwa na majambazi
  • Na mwisho kupoteza marinda
Mambo yote uliyoyataja, mengine kama ajali za vyombo vya moto, kuumwa na wadudu wenye sumu, kuvamiwa na wakulungwa( majambazi)tayari vishanitokea na sivihofii.

Hofu yangu kuu ni kufungwa jela kwa hukumu.

Hiyo ndiyo hofu yangu kubwa, ni heri ya kifo kuliko kufungwa jela let say kuanzia miaka mutatu na kuendelea.

Hiyo kwangu naiona ni adha kubwa sana kuliko jambo jingine lolote katika maisha yangu.
 
Nipe kidogo mkanda uliumwana na nini na ulivamiwaje n majambazi
 
Naogopa Umasikini. Lakini nnaogopa zaidi akili zangu kupoteza uwezo wa kufanya kazi ipasavyo.
 
Binafsi vyote navihofia MWENYEZI MUNGU atunusuru navyo🙏🙏🙏
True mkuu kitu anachokisense mtu ni kibaya mtu mwingine yeyote timamu atakisense ni kibaya otherwise asiye sense lazima nati zitakuwa loose kichwani
 
Nipe kidogo mkanda uliumwana na nini na ulivamiwaje n majambazi
Ni mkanda mrefu kidogo kutokana na matukio hayo kuwa yamenitokea katika maisha lakini kwa nyakati tofauti.

Nianze na majambazi:
Matukio hayo yamenitokea mara mbili, la kwanza nilivamiwa nyumbani kwangu, siku hiyo niliingia na gari la kukodi lililonibebea vifaa vya ujenzi.

Walipoviteremsha nahisi wale ma day worker mmoja alikuwa ni jambazi akakagua namna ya kuingia na usiku wakatinga.

Walikuwa wamejipanga haswa, kilichonisaidia huwa sihofii kifo linapokuja jambo la hatari mbele yangu.

Maisha nimekwisha yaishi hivyo kufa sihofii hata kidogo, kwa sababu sina cha kupoteza.

Nikivamiwa sibabaiki, bali hutuliza akili kuona njia bora ya kufanya kujihami, hasa kutumia silaha zilizopo.

Ndani kukiwa na panga ama chochote chenye ncha kali, jambazi ajipange vinginevyo namuua kirahisi sana.

Mara nyingi majambazi hutumia vitisho vya maneno kukudhoofisha ili usiwadhuru na wakupore kirahisi.

Kifupi nilipambana wakagwaya wakaondoka kwa matusi na kuahidi kurudi na kweli walirudi siku nyingine ambapo ndipo nilipoua mmoja.

Walipovamia walifanza zoezi la kubomoa dirisha baada ya mlango kuwashinda kuuvunja.

Dirisha lilipodondokea ndani, kwanza wakaanza kubishana nani aanze kuingia.

Yule wa kwanza kuingia, aliingia kwa kurukia ndani akanikuta nimejibaza katika angle sahihi na kulikuwa na giza, yeye kashika tochi.

Bila kuchelewa, kabla tochi yake haijanielekea nikampiga shoka la shingo, kishindo kikubwa kikasikika hadi nje pamoja na kelele yake dhaifu ya 'eee yaalah', wenzake wakatimua mbio.

Kifupi shoka lile lilimchinja kwa nyuma na kubakiza kipande kidogo sana cha koromeo.

Nilichogundua kuwa majambazi ni waoga, hawataki kujulikana ama kujeruhiwa kwa vyovyote ili wasije kujulikana, ndiyo ababu ya vitisho vyao hivyo.

Suala la kuumwa na nyoka ama mdudu:
Niliwahi kuumwa na nyoka nikiwa kijana mdogo darasa la pili.

Ni kwamba nilikuwa napenda sana kupanda miti (clever climber), hasa miembe na mipera.

Siku moja nikiwa nimepanda mwembeni, kumbe tawi la mwembe lililonitamanisha kulikuwa na nyoka wa kijani sikumuona!

Niliponyoosha mkono kuchuma hilo embe, yule nyoka nadhani alihisi nataka kumkamata, maana alikuwa pembeni mwa lile tunda!

Nilihisi kama nimechanjwa na kiwembe mkononi, kumbe ndiyo kuumwa kwenyewe huko!

Nilipochunguza nikamuona nyoka pembeni kakasirika anataka kurudia kuniuma.

Nikapaniki na kupoteza fahamu.

Nilijikuta nipo chini na maumivu makali na uvimbe, nikakurupuka kukimbia nyumbani.

Nikapewa huduma ya kwanza kwa kubandikwa "jiwe" (aina fulani ya mifupa ya wanyama iliyochomwa) hutumika kuzuia na kunyonya sumu za nyoka ama nge.

Baadaye nikakimbizwa hosipitali nilikoenda kutibiwa na kupona.

Mwisho kuhusu ajali:
Ajali za vyombo vya moto nimezipata mara tatu kwa muda tofauti.

Nasimulia hii ya mwisho ya mwaka jana mwezi October.

Nilimchukua kijana wangu twende kijijini kufuatilia miradi tuliyowekeza huko.

Nikamwambia aendeshe yeye, tukaondoka na kufika salama.

Baada ya shughuli za huko, wakati wa kurudi ndiyo kimbembe kilipotokea.

Barabara ya kijijini, ilikuwa imechongwa na kuwekwa changarawe, kati kati ikawa imenyenyuka kama tuta.

Kijana wangu hajazoea kupita akiendesha bara bara za aina hiyo.

Wakati wa kurudi kabla ya ajali, nilimsikia akiniuliza "baba, hivi leo vipi hii gari, naona inavutia pembeni".

Kabla sijamjibu lolote, gari ipo kwenye mwendo akafosi usukani kuirejesha katikati mwa barabara!

Wee!

Gari ikayumba, akaifosi tena kuirudisha huku mguu kausahau kwenye moto.

Gari ikaongeza mwendo na kupaa nje ya barabara kuparamia tuta la pembeni.
Tuta halikuzuia kutokana na kasi ya mwendo ilivyoongezeka ghafla.

Tukawa tumeacha njia tukaenda kuuparamia mti mkubwa pembeni mwa barabara.

Matendo yote hayo yalifanyika mimi nikiona ajali namna inavyoenda kutokea, kwa hiyo sikupaniki na nilikuwa nimefunga mkanda!

Sisi hao tukaenda kuuvaa mti katikati, si kishindo hicho, bhuuu!
Gari ikaanza kupiga honi za ajali, raia tele washafika!

Kutaka kufungua mlango, nikakuta umejilock.

Kijana wangu, yeye akafungua na kutoka nami nikatumia mlango wa dereva kutoka huku kelele za honi zikiendelea kulia huku oil na coolant vikimwagika ovyo, maana rejeta lilipasuka.

Nikafungua bonet haraka na kudisconnect bateri kunyamazisha mlio.

Kuja kujikagua, sote hatujaumia!

Hata mikwaruzo, hata maumivu ya ndani kwa ndani kutokana na kishindo hicho hakuna hatukupata, Mungu alitulinda ingawa gari iliumia pakubwa!

Mpaka leo, hii ajali ya mwisho huniijia kichwani, namna ilivyokuwa kubwa lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu tukatoka salama bila hata mikwaruzo!

Kwa hiyo niseme tu kuwa hofu yangu kubwa katika maisha ni kifungo pekee.

Yaani kusoteshwa jela ndiyo jambo ninalolihofia katika maisha yangu, lakini mambo mengine, nimeyapitia na kuyavuka salama kwa ulinzi wa Mungu na hayanitii mashaka pindi yanapokuwa mbele yangu.
 
Hayo yote uliyoyapitia ni life threatening moja kati hayo lingeweza kutwaa uhai wako hasa la nyoka na ajali.
 
Umasikini wa kitupwa, Mke wa hovyo. Addiction ya vitu.
 
Upo kwenye hatari sana, Shetani atatumia baadhi hivyo kukunyoosha. Unaogopa mambo mengi mno.
 
MTAKAVYOTAJA NYIE MJUE NDO KILA MWANADAMU HAPENDI VIMKUTE.
 
Back
Top Bottom