Ni Kitu ghani ulishawahi kuona kwenye nyumba/chumba cha mtu ukashindwa kabisa kuelewa kilifikaje fikaje pale?

Ni Kitu ghani ulishawahi kuona kwenye nyumba/chumba cha mtu ukashindwa kabisa kuelewa kilifikaje fikaje pale?

Kipindi nipo chuo 2nd year nilikua na jamaa yangu alikua anapenda sana kuja kwangu lakin sikuwahi kwenda kwake alikua anakaa mbali na huwa sina tabia ya kwenda kwa watu hovyo. Kuna siku akachukua adopter ya pc akawa mgumu kurudisha zikapita wiki mbili kila nikimwambia anasema ataleta lakini haleti. Siku moja tumetoka kipind jioni nikaunga nae hadi kwake tumefika akanikarobisha ndani kwakuwa ni mshkaji nikazama ndichi. Kuingia tu naona wale jamaa ukutani wapo wengi mno mwamba ananiambia karibu ukae, ebhana ee niliogopa kukaa nikasimama katikati ya chumba nisijekaa nikawabeba. Nilibaki najiuliza hivi huyu mwamba anaishije na kunguni kiasi kile na alikuwa very smart.
Kunguni ni either uchafu au kuna mtu ni kikojozi au damu ushasikia mtu anakwambia una dam ya kunguni?? unaweza ukawa huna hivp vitu ukaenda sehem wapo ukahisi utawabeba lakini ikawa hola??
 
Kunguni ni either uchafu au kuna mtu ni kikojozi au damu ushasikia mtu anakwambia una dam ya kunguni?? unaweza ukawa huna hivp vitu ukaenda sehem wapo ukahisi utawabeba lakini ikawa hola??
Uchafu pia huchangia sana kunguni kuweka kambi.
kunguni m1 tu ukimbeba anatosha sana kukuletea janga la kunguni
 
Uchafu pia huchangia sana kunguni kuweka kambi.
kunguni m1 tu ukimbeba anatosha sana kukuletea janga la kunguni
mkuu kuna hilo balaa la kuishi na vikojozi usiombe, kuna mama mtu nilimwazima mtandio bas kabla hajaurudisha napita kwake nakuta anatoa magodoro nje na vitanda namuuliza kulikoni leo ananambia kunguni nilifadhaika na nguo yangu siku anaurudisha nilikua nauanika nje jua kali nikitoka hapo naufua nauanika tena kama mara tatu hivi nikauacha nje usiku upigwe nanbaridi ndipo nilipouweka kabatini
 
Kwanini usingemuachia au ungeutupa kabisa. Hiyo mifugo ni tishio ni vidudu vidogo lakini korofi sana.
 
Katika harakat za maisha nilipga kambi kw mwnangu, nilikaa kwake km mwezi hiv cku nimechlewa kuamka naweka mazngra sawa ya ktnd upande anaopenda kulala nikahisi kitu km kijiwe hv c nipekue nitoe nakuta ni hirizi
 
Kwenye harakati za maisha unaweza kwenda kwa mtu,mshikaji au ndugu yako ukakutana na vitu ukajiuliza vimefikaje pale ukakosa majibu.

Mimi nna visa kadhaa ambavyo nilivikuta kwa washikaji zangu kwenye magheto yao huwa najiuliza sana nakosa majibu hadi leo..nabaki kucheka tu kila nikikumbuka.

1: Kitanda cha kujenga Na tofali alafu nyumba ni yakupanga nilipo uliza umekikuta akajibu hapana nili jenga nikauliza ulijenga vp akajibu nilikua nakuja Na tofali moja moja kwenye begi ili mwenye nyumba asijue ujenzi unao endelea nikauliza kwahio hapa akitaka uhame? Akajibu ndio hio siku atashangaa nikisha hama

2: Mimi nilienda ghetho kwa mshikaji wangu nikamkuta jamaa analalia kitanda cha hospital sijui kilifikaje pale ghetho.

3: Nilienda kwa MWALIMU wangu wa primary, nikakuta MILANGO imeandikwa STD 1,STD 2 mpka la SABA 😁😁 nkajisemea tuu kimoyo kimoyo HUU NDO WIZI sasa.

4: Nilienda kwa jamaa angu ukonga nikakuta kitandani ametandika shuka za MSD.
Kila nikijaribu kumuuliza anaishia kucheka tu😆😆😆😆.

Je, wewe mkuu ushawahi kukutana na nini huko maghetho au nyumbani
C.H.A.I
 
Katika harakat za maisha nilipga kambi kw mwnangu, nilikaa kwake km mwezi hiv cku nimechlewa kuamka naweka mazngra sawa ya ktnd upande anaopenda kulala nikahisi kitu km kijiwe hv c nipekue nitoe nakuta ni hirizi

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ukaondoka siku hiyo hiyo
 
Hiyo ni kweli.Nimewahi kulala nyumba moja ya wageni kitanda kikiwa modeli hiyo.Nililala kama nipo kibarazani huku nacheka usiku karibia wote.Hapo kwenye nyumba ya kupanga kunahitaji maombi zaidi.[emoji23][emoji23]
Kuna gesti moja RUANGWA mkoani Lindi kuna vitanda vya Tofali za kuchoma.. wamepiga marumaru. Safi kabisa
 
Hiyo ni kweli.Nimewahi kulala nyumba moja ya wageni kitanda kikiwa modeli hiyo.Nililala kama nipo kibarazani huku nacheka usiku karibia wote.Hapo kwenye nyumba ya kupanga kunahitaji maombi zaidi.😂😂
Zanzibar wanajenga haya mavitanda kwakweli mara ya kwanza sikuweza kulala mana niliona kama tayari nshajiingiza mwenyewe kaburini bila kukata roho....Alafu wapemba sio wa mambo ya kunyanduana kwa nguvu iweje wajenge matofari?
 
Ghetto kijijini nilipoenda kusalimia nikapewa nilale na huyo bro anayelala hapo anaingia kama sasa sita usiku .Bhana nimeenda kulala kama saa nne kasoro aisee nashangaa panaletwa Mbuzi mule ndani tulale nao wapo kama watano hivi na nilikuwa nipo alone jamaa bado hajaja mpaka saa sita.

Hao mbuzi hawalali wanatafuna usiku mzima na unasikia kabisa "kwachu kwachu kwachu " na mule ndani hamna majani sijui wanayatoa wapi?
 
Back
Top Bottom