Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Kuna jambo kubwa sana la kujifunza hata ambao hawajakutana na visa au hata kue desha kabsa.
Ili siku ukiwa na ndiga lako usiendeshe kwa mazoea ujue kabsa kwamba nikiendesha ivi au vile naweza kutana na hatari.
Visa ni vingi watu wamevielezea zaidi vinahusiana na hatari ya
1.ku overtake bila kuchukua tahadhari zaidi.
2.matumizi ya cm wakati wa kuendesha.
3. Kukatisha sehemu zenye mikondo ya maji chukua tahadhari kubwa.
Hii nakazia iko ivi kitaalamu tairi zimejazwa kwa upepo hivyo zinatabia ya kuelea zinapopita kwenye sehemu yenye kina hata kidog cha maji...inakuwa kama yale maboya yanayoelea kwenye maji.
3. Overspeed ni hatari kwasababu hata likitokea la kutokea inakuwa risk kubwa hata kujiokoa unabaki kusubir huruma za allah.

NB: Najifunza kwamba hata nikiwa barabaran nisijisahau kwa kuwafikiria wale madereva ambao wanaweza kukusababishia hatarii
Speed speed speed ni majan[emoji879][emoji879].
Tuendelee kutoa uzoefu kuna kundi kubwa linajifunza.
 
Daaaah acha kabisa kuna siku nimetoka dar saa 12 jion kuja mwanza niko peke yangu kwenye gari, basi nikafika moro nikaona isiwe shida acha nitafte abiria, bahati nzuri nikapata wa mwanza na shy gari ikakaa level seat.

Mida ya saa tisa usiku nlikuwa singida sehem reli inapishana na barabara, and kabla ya hapo huwa kuna kona ya mushoto sasa nlikuwa nimetanguliza semi nikaona inanichelewesha, usiku nikitaka kuovertake kwenye zero visibility huwa naangalia taa za gari inayokuja mbele yangu nikiona kimya huwa nachomoa tu.

Bwana eeeeh ila nimetokeza tu hivi nipo ubavuni mwa semi katikati gjafla naona semitrail ingine inapandisha ipo speed, jamaa ilibidi tu awe mstaarabu akaitoa nje ila nlikuwa nishakubali yaishe.

Abiria wangu hakuna alojua kitu walikuwa wamelala wote
Duh pole sana. Uwe makini sana safari za mkoa zinataka utulivu sana na umakini wa mwili na akili especially kwa mtu ambaye hausafiri mara kwa mara kwenda mikoani ruti ndefu.
 
Mimi nafikiria kuchomekea kipisicha nondo chini ya gas pedal ili nisivuke 80, au kuna njia nyingine? au nibandike karatasi "speed kills" kwenye usukani.
Maana unajisahau unakuwa rough mpaka unajishangaaa.
Weka picha aina ya passport size ya mtoto wako,mkeo, bi mkubwa au ya dingi kwenye dashboard eneo la spidi kuanzia 90km/h ili ikifika ukiona picha imeziba utakumbuka kuwa wanaokupenda bado wanakuhitaji.
 
Hizi sehemu zimetuama maji barabarani huwa naziheshimu sana.
kabisa... huwa zina matatizo yake..tena sehemu nyingine unaweza kuta kuna lami vizuri kabisa kumbe sehemu ambayo maji yametuama kuna shimo yale mashimo ya kwenye lami yanakuwa na ncha kali sana. kuna gari moja nilikuta imekaa ilikuwa canter tairi za nyuma zimeachana na body kumbe ile sehemu ina shimo kali sana nadhani jamaa akalivamia akijua ni maji tu yametuama kizembe
 
1. 2020 nikiwa naelekea moro kutoka dom saa 9 alfajiri, niko na run x, nyuma ya landcruiser kwa mbele kuna taa moja imefifia nikajua ni boda boda , nikatoka kuovertake jamaa wa lori kawasha full hadi zile taa za juu kumbe ni semi bana. Nikashika brake nikarudi nyuma ya cruiser. Nikasema Mungu mwema.
 
Back
Top Bottom