Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Haah! Umefanya nirealize kitu; ivi kumbe neno santa kalawe litakuwa limetokana na santa claus ndo maana la ajabuajabu hata sio kibantu. Sandakalawe wich!??Unazigawa bure kama santa Claus nije nizifungashe fasta πππ
Nilitaka kushauri the same. Kwa nini asiue chumba kimoja akatoa vyoo viwili tena unaua chumba jirani na master unapata master toilet na common toilet.Vyumba vitano vyote vya nini, aue chumba kimoja afanye kutengeneza vyoo vya ndani. Tena achague chumba kilichopo karibu na chumba chake ili atengeneze choo cha master na choo cha public.
Serikali sijui huwa inakwama wapi kupima maeneo ya viwanja vya makazi. Ujenzii holela ni janga nchi nzimaNilikuwa wa kwanza kujenga nyumba sehemu ambayo ilikuwa imepanuliwa kuwa sehemu ya jiji la Mwanza sehemu za Mkolani. Nikajenga nyumba yangu kubwa ya kisasa kwa gharama kubwa sana hasa kwa vile ilinilazimu kujivutia maji na umeme mwenyewe. Baada ya miaka 15 eneo likavamaiwa na ujenzi holela wao wakiuita upimaji shirikishi na hivyo jumba langu kuzungukwa na vijumba visivyo na mpangilio kiasi kuwa hata njia ya kwenda nyumbani kwangu haipo tena inabidi nizunguke zunguke kwa kubahatisha hadi kufika nyumbani.
Ushauri wangu ni kwamba epuka kujenga eneo ambalo halijajengwa kwani hujui litakuja kujengwa vipi.
Mbona rahisi tu kudrill. Mie nyumba yangu ya ghorofa moja na nimedrill na kuweka pangaboi za Panasonic safi nakula upepo tuNimejenga underground iliyofanywa na fundi wa mtaani (local fundi), wakati wa kumwaga slab, kwenye wiring map ya umeme hawakuweka zile hook za feni (pangaboi), sasa baada ya kumiminwa slab juu hakuna mahali pa kufunga feni au la niweke mbao za dari ili nipate mbao ya kufungia hook, kitu ambacho ni hasara, maana nitakuwa na slab na bado nimeweka dari.
Ninalazimia kutumia feni za kusimama ambazo sizipendi na zinaleta ghasia tu, sijui kama inawezekana kudrill ili tuweke hook ya feni ili nifunge pangaboi.
Tatizo ni siasa.Serikali sijui huwa inakwama wapi kupima maeneo ya viwanja vya makazi. Ujenzii holela ni janga nchi nzima
Aisee kumbe inawezekana!! Nimewahi kufikiri kufanya hivyo sema nikatishwa kuwa inaweza kusababisha kama crack joints kwa ile concrete (slab), sasa sijui kama ni kweli. Hongera sana kusolve tatizo. Na baada ya kudrill ulifunga hook kwa nati na fisha au ulisiliba na simenti kali?Mbona rahisi tu kudrill. Mie nyumba yangu ya ghorofa moja na nimedrill na kuweka pangaboi za Panasonic safi nakula upepo tu
Daah m nilitaka kuua mtu huu ujinga, tena mtu namuamin sana akafanya ujinga mkubwa siku naenda site nataman kuzimia Hali iliyokuwepo na pesa iliyotumikaHii kitu najuta sana yani sana hapa nimebidi nifukuze fundi nimeleta mwingine arekebishe makosa
hapa ndipo kwenye changamoto hasa hivi viwanja visivyozidi 20mx20m ( vya bei ya kati )barabara ya kueleweka kwanza.
Bro angu mmoja kaamua harakaharaka kununua kiwanja cha mbele yake maana kahofia akili ya ambaye angepachukua ingekuwaje?hapa ndipo kwenye changamoto hasa hivi viwanja visivyozidi 20mx20m ( vya bei ya kati )
kujua barabara ipo ni mpaka ukute pamejengwa hapo la sivyo utakua unapiga ramli, unaona bikon imeishia pale,
anakuja wa kuitwa jirani anan'goa, anajenga anazidi, au anajenga ukuta na unazidi, gari haiwezipiga kona tena
au anaweka tofali kwa mbele kidogo au , njia inazidi kua m'banano, nimeona sehemu kadhaa hii
jamaa ana bonge wa mjengo na mgeti wa ku-slide ila kwa mbele kapigwa pini kimtindo, matokeo yake gari haipiti/haiwezi piga kona, analaza CCM
Kwa mfano ukijenga vyumba vitatu kimojaa master hiyo nayo ni kubwa??Mjumba mkubwa hakikisha unaumalizia vizuri upendeze, la sivyo utauchukia. Kingine si tulikubaliana utazaa watoto wawili tu, sasa mjumba mkubwa wa nini[emoji1787]
Mambo Sumbai?Blaza blaza vyumba vingine vya ndugu kutoka kishimundu na ugweno. Au tukija utatulaza guest ??
Vyumba vitatu ni standard kwa maisha ya mtanzania wa kawaida mkuu.Kwa mfano ukijenga vyumba vitatu kimojaa master hiyo nayo ni kubwa??
Hapo nimeangalia jinsia za watoto kama wakiume na wakike.
Halafu hela ya kuunga unga ushauri tafadhali kabla sijalikoroga
Sio tu uzungu tunakwepa pia gharama plus hela yenyewe tunaunga unga.Ni kweli, wakati ninajenga nilimpeleka rafiki yangu mmoja site kumuonesha (na yeye alikuwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake wakati huo) kuna sehemu akaniuliza, " hapa ni kwa ajili ya nini mbona umeacha hivi" ilikuwa ni jikoni, nikamjibu " hapa nina plan ya kuweka dish washer" baadae akauliza na hapa " nikamwambia hii ni laundry room, plan yangu ni kuweka washing mashine, drying mashine na meza ya kupigia pasi. Alichoniambia baada ya hapo kilinishangaza kidogo, alisema " ACHA MAMBO YA UZUNGU MZEE, JENGA SIMPLE TU". So hii ndio mentality ya wabongo wengi..tunaogopa "uzungu"
Hata sikuwepo siku walipokuwa wanafunga feni, nilikuta fundi kazifunga na zinachapa kazi. Sidhani kama ilikuwa issue kubwa kwa mafundiAisee kumbe inawezekana!! Nimewahi kufikiri kufanya hivyo sema nikatishwa kuwa inaweza kusababisha kama crack joints kwa ile concrete (slab), sasa sijui kama ni kweli. Hongera sana kusolve tatizo. Na baada ya kudrill ulifunga hook kwa nati na fisha au ulisiliba na simenti kali?
Yes lakini pia licha ya uwezo tuweke pia provision ya kuweka hivyo vifaa hata kama kwa sasa hela huna. Mfano unajenga bafu basi weka provision ya heater au vyumbani weka provision ya AC, sio siku unapata hela ndio unaanza kuvunja tiles na kuta ili upitishe nyaya.Sio tu uzungu tunakwepa pia gharama plus hela yenyewe tunaunga unga.
Kwa wale wenye uwezo huo wafanye tu mana hakuna asiyependa vitu vizuri basi tu tunatofautiana uwezo.
Mbaya zaidi hatutaki kukubali hatuna uwezo bali tunaleta maneno ya kujifariji kuwa huo ni uzungu
Ni kweliYes lakini pia licha ya uwezo tuweke pia provision ya kuweka hivyo vifaa hata kama kwa sasa hela huna. Mfano unajenga bafu basi weka provision ya heater au vyumbani weka provision ya AC, sio siku unapata hela ndio unaanza kuvunja tiles na kuta ili upitishe nyaya.
Mie nimeweka mpk pipes za internet ndani maana huwezijua kuna siku unaweza kuta zitahitajika halafu kwako kukaonekana kituko.
Utamalizia ukistaafuKwa kweli sio jambo la kitoto. Ni kwamba unajenga nyumba mbili kwa wakati mmoja, na kipato chenyewe cha kuunga unga. Mpaka sasa sijapaua, ila nimeshahamia nakaa kwenye andagraundi, japo jasho linanitoka sana kumaliza jengo.
Kujenga bila kupumzka.. nyumba inakua na mapungufu mengi sanaHabari wana JF
Ni kosa gani ulilifanya kipindi unajenga na ungependa wengine wajifunze ili lisitokee kwao?
Inaitwa "Kuotesha Uyoga"Kujenga bila kupumzka.. nyumba inakua na mapungufu mengi sana