Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Sijajenga lakini jana nimetembelea eneo moja la squaters Kalobe huko na pikipipiki, ile ziara imenifundisha kitu kikubwa.

Makazi holela sio ya kukimbilia maana kuna maeneo nikajisemea hivi hata kama serikali ikaamua kuwasaidia kukarabati barabara itaanzaje? Itapitisha wapi hilo greda hadi lije lifike hapo ndichi? Chobingo kona kalikali ambazo hadi kwa pikipiki tu zinazingua🤔

Kuna maeneo ukichagua kujenga unakuwa tayari umejifungamanisha na roho ya kukwama njiani, kuvamiwa na maji na kukosa njia ya kutokea. Kataa kabisa. Au jiridhishe kuna barabara ya kueleweka kwanza.
 
Vyumba vitano vyote vya nini, aue chumba kimoja afanye kutengeneza vyoo vya ndani. Tena achague chumba kilichopo karibu na chumba chake ili atengeneze choo cha master na choo cha public.
Nilitaka kushauri the same. Kwa nini asiue chumba kimoja akatoa vyoo viwili tena unaua chumba jirani na master unapata master toilet na common toilet.
 
Nilikuwa wa kwanza kujenga nyumba sehemu ambayo ilikuwa imepanuliwa kuwa sehemu ya jiji la Mwanza sehemu za Mkolani. Nikajenga nyumba yangu kubwa ya kisasa kwa gharama kubwa sana hasa kwa vile ilinilazimu kujivutia maji na umeme mwenyewe. Baada ya miaka 15 eneo likavamaiwa na ujenzi holela wao wakiuita upimaji shirikishi na hivyo jumba langu kuzungukwa na vijumba visivyo na mpangilio kiasi kuwa hata njia ya kwenda nyumbani kwangu haipo tena inabidi nizunguke zunguke kwa kubahatisha hadi kufika nyumbani.

Ushauri wangu ni kwamba epuka kujenga eneo ambalo halijajengwa kwani hujui litakuja kujengwa vipi.
Serikali sijui huwa inakwama wapi kupima maeneo ya viwanja vya makazi. Ujenzii holela ni janga nchi nzima
 
Nimejenga underground iliyofanywa na fundi wa mtaani (local fundi), wakati wa kumwaga slab, kwenye wiring map ya umeme hawakuweka zile hook za feni (pangaboi), sasa baada ya kumiminwa slab juu hakuna mahali pa kufunga feni au la niweke mbao za dari ili nipate mbao ya kufungia hook, kitu ambacho ni hasara, maana nitakuwa na slab na bado nimeweka dari.

Ninalazimia kutumia feni za kusimama ambazo sizipendi na zinaleta ghasia tu, sijui kama inawezekana kudrill ili tuweke hook ya feni ili nifunge pangaboi.
Mbona rahisi tu kudrill. Mie nyumba yangu ya ghorofa moja na nimedrill na kuweka pangaboi za Panasonic safi nakula upepo tu
 
Serikali sijui huwa inakwama wapi kupima maeneo ya viwanja vya makazi. Ujenzii holela ni janga nchi nzima
Tatizo ni siasa.
Serikali ilitakiwa iwe na msimamo, isiwe na huruma, isipitishe ramani kama haiendani na mipango miji
 
Mbona rahisi tu kudrill. Mie nyumba yangu ya ghorofa moja na nimedrill na kuweka pangaboi za Panasonic safi nakula upepo tu
Aisee kumbe inawezekana!! Nimewahi kufikiri kufanya hivyo sema nikatishwa kuwa inaweza kusababisha kama crack joints kwa ile concrete (slab), sasa sijui kama ni kweli. Hongera sana kusolve tatizo. Na baada ya kudrill ulifunga hook kwa nati na fisha au ulisiliba na simenti kali?
 
Hii kitu najuta sana yani sana hapa nimebidi nifukuze fundi nimeleta mwingine arekebishe makosa
Daah m nilitaka kuua mtu huu ujinga, tena mtu namuamin sana akafanya ujinga mkubwa siku naenda site nataman kuzimia Hali iliyokuwepo na pesa iliyotumika
 
barabara ya kueleweka kwanza.
hapa ndipo kwenye changamoto hasa hivi viwanja visivyozidi 20mx20m ( vya bei ya kati )

kujua barabara ipo ni mpaka ukute pamejengwa hapo la sivyo utakua unapiga ramli, unaona bikon imeishia pale,
anakuja wa kuitwa jirani anan'goa, anajenga anazidi, au anajenga ukuta na unazidi, gari haiwezipiga kona tena

au anaweka tofali kwa mbele kidogo au , njia inazidi kua m'banano, nimeona sehemu kadhaa hii
jamaa ana bonge wa mjengo na mgeti wa ku-slide ila kwa mbele kapigwa pini kimtindo, matokeo yake gari haipiti/haiwezi piga kona, analaza CCM
 
Bro angu mmoja kaamua harakaharaka kununua kiwanja cha mbele yake maana kahofia akili ya ambaye angepachukua ingekuwaje?

Na hata sio lazima akose ustaarabu, ni kwamba asipokubali kukuhurumia tu umekwisha. Ukienda kihaki humshindi.
 
Mjumba mkubwa hakikisha unaumalizia vizuri upendeze, la sivyo utauchukia. Kingine si tulikubaliana utazaa watoto wawili tu, sasa mjumba mkubwa wa nini[emoji1787]
Kwa mfano ukijenga vyumba vitatu kimojaa master hiyo nayo ni kubwa??
Hapo nimeangalia jinsia za watoto kama wakiume na wakike.
Halafu hela ya kuunga unga ushauri tafadhali kabla sijalikoroga
 
Ni kweli, wakati ninajenga nilimpeleka rafiki yangu mmoja site kumuonesha (na yeye alikuwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake wakati huo) kuna sehemu akaniuliza, " hapa ni kwa ajili ya nini mbona umeacha hivi" ilikuwa ni jikoni, nikamjibu " hapa nina plan ya kuweka dish washer" baadae akauliza na hapa " nikamwambia hii ni laundry room, plan yangu ni kuweka washing mashine, drying mashine na meza ya kupigia pasi. Alichoniambia baada ya hapo kilinishangaza kidogo, alisema " ACHA MAMBO YA UZUNGU MZEE, JENGA SIMPLE TU". So hii ndio mentality ya wabongo wengi..tunaogopa "uzungu"
Sio tu uzungu tunakwepa pia gharama plus hela yenyewe tunaunga unga.
Kwa wale wenye uwezo huo wafanye tu mana hakuna asiyependa vitu vizuri basi tu tunatofautiana uwezo.
Mbaya zaidi hatutaki kukubali hatuna uwezo bali tunaleta maneno ya kujifariji kuwa huo ni uzungu
 
Aisee kumbe inawezekana!! Nimewahi kufikiri kufanya hivyo sema nikatishwa kuwa inaweza kusababisha kama crack joints kwa ile concrete (slab), sasa sijui kama ni kweli. Hongera sana kusolve tatizo. Na baada ya kudrill ulifunga hook kwa nati na fisha au ulisiliba na simenti kali?
Hata sikuwepo siku walipokuwa wanafunga feni, nilikuta fundi kazifunga na zinachapa kazi. Sidhani kama ilikuwa issue kubwa kwa mafundi
 
Sio tu uzungu tunakwepa pia gharama plus hela yenyewe tunaunga unga.
Kwa wale wenye uwezo huo wafanye tu mana hakuna asiyependa vitu vizuri basi tu tunatofautiana uwezo.
Mbaya zaidi hatutaki kukubali hatuna uwezo bali tunaleta maneno ya kujifariji kuwa huo ni uzungu
Yes lakini pia licha ya uwezo tuweke pia provision ya kuweka hivyo vifaa hata kama kwa sasa hela huna. Mfano unajenga bafu basi weka provision ya heater au vyumbani weka provision ya AC, sio siku unapata hela ndio unaanza kuvunja tiles na kuta ili upitishe nyaya.

Mie nimeweka mpk pipes za internet ndani maana huwezijua kuna siku unaweza kuta zitahitajika halafu kwako kukaonekana kituko.
 
Ni kweli
 
Kwa kweli sio jambo la kitoto. Ni kwamba unajenga nyumba mbili kwa wakati mmoja, na kipato chenyewe cha kuunga unga. Mpaka sasa sijapaua, ila nimeshahamia nakaa kwenye andagraundi, japo jasho linanitoka sana kumaliza jengo.
Utamalizia ukistaafu
 
Back
Top Bottom