Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Mkuu hakijaribika kitu watoto wakihama napangisha mabinti wazuri wapate kunifanyia masaji
 
Nimekuelewa sana hapa mkuu
 
Hongera sana mkuu, ni nyumba very spacious with all important modern ammenities. Pambana iishe. Kiukweli napenda nyumba sampuli yako in size.
Karibu na asante kunitia moyo... nawe nakuombea kwa Mungu akupe kwa kadri ya matamanio yako.
 
Wewe ndo mshamba kwa kuona uchaguzi wa wenzako wa kishamba wako ndo bora zaidi.

Wewe kama unapenda ndogo ni wewe. Waache wanaopenda kubwa wafanye wakipendacho.
 
Though sijawahi kuwa na nyumba wala kujenga ila kosa ambalo siwezi kufanya ni kuachia upenyo wowote, nitajipanga vizuri na hela yao yote cash na nitakuwa nao site kufuatilia kila hatua huku nikiwa na nguo za kazi ikibidi kusaidiana nao kabisa.
Usipate homa kuna kipindi utapigwa tu, kijanja janja.

Utapunguza tu machungu utakapokuwepo site.
 
Kila mtu amalize haja zake chumbani kwake,
Kuna ubaya
Na wageni wapitanjia watakwenda wapi ikitokea dharura?

Ningekushauri (na ndivyo nilivyofanya mimi) choo kimoja cha master br, choo cha pili kwa kushare vyumba viwili na choo cha tatu kwa ajili ya wageni tu (kisitumike sana na familia labda kwa dharura). Hichi cha wageni wa kupita kiwe na toilet na basin ya kunawia mikono tu (hamna shower na mazagazaga mengine)
 
Uzuri wa umasikini ni mnyororo mgumu sana kuukata.
 
Halafu mchwa walivyo na tabia mbaya wanatafuna ndani kwa ndani siku ya siku unashtukia unagusa ubao unabonyea
 
Wewe mangi uandishi wako raha sana...sio kufunja ni KUVUNJA[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
KOSA KUBWA AMBALO WAJENZI NA WAJENGEWA HUKIFANYA SIKU ZOTE;.
Ni kuharibu nyumba kuanzia kwenye msingi.
Nyumba sio chini ya 96% Tanzania, ujenzi wake umekosewa kuanzia msingi.

Msingi unatakiwa usiwe chini ya 60cm kutoka usawa wa Ardhi.
60cm ni sawa na laini 4 za tofali za nchi 6 au ngazi nne.

Kwani ni makosa kukosea msingi?
Unakosea msingi kwa mfano nyumba ikawa na laini 2 kutoka usawa wa ardhi;
1. Nyumba itapoteza uwiano kati ya msingi, boma na paa

2. Nyumba hukosa mvuto.
3. Mvua inaoonyesha matone yanayodondoka chini hurukia barazani au ukutani na kuharibu rangi.

4. Mara nyingi husababisha nyumba inakuwa fupi hivyo kuwa na joti kalu ndani.

...USHAURI;.Kabla hujaanza ujenzi pata ushauri wa kitalaam
 
Mkuu kuna baadhi ya sehemu lazima ununue bidhaa bora ili kuepuka asala kubwa, frem ungejitaidi ungeweka za mbao ngumu ya mbuga na paa ungeweka mbao zenye dawa, kuna sehemu ukifika kwenye kujenga husimskmilize fundi na kufata ushauri wake ata kama hauna pesa bora utulie ujipange, kuna sehemu kwenye ujenzi ukinunu vitu vya bei chee tu lazima itakugharimu kama hapo kwenye frem na vitenda inaonekana umetumia mbao za viwango vya chini sana mpaka mchwa wanakula mbao, hiyo frem ingekuwa mninga mchwa wasinge jaribu kuusogelea wangepita mbali na kwenye fenicha pia.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Halafu mchwa walivyo na tabia mbaya wanatafuna ndani kwa ndani siku ya siku unashtukia unagusa ubao unabonyea
Tatizo la vijana wasikuizi hawajui kutofautisha ya aina ya mbao wenyewe wananunua tu bila kufahamu hii frem ninaweka kwenye nyumba yangu je ni imara wadudu wanaiogopa, kuna aina ya mbao mdudu haisogelei miaka na miaka.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Wakati wa kuset na kuchora ramani kwenye kiwanja jitahidi sana uwepo site
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…