Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Aisee kumbe inawezekana!! Nimewahi kufikiri kufanya hivyo sema nikatishwa kuwa inaweza kusababisha kama crack joints kwa ile concrete (slab), sasa sijui kama ni kweli. Hongera sana kusolve tatizo. Na baada ya kudrill ulifunga hook kwa nati na fisha au ulisiliba na simenti kali?
Mpate funfi mzuri. Kuna special nati baada ya ku dril unafunga zinabana bila hata kuweka plasta.
 
Nilimpa Fundi ramani akaanza (akaseti) msingi nikiwa sipo.

Kurudi nakuta nyumba ameisogeza sana nyuma. Means makaro ya choo na sehemu ya kuanikia vitabanana upenuni (pembeni). Wakati kama msingi angesogeza mbele hayo makaro (sewage) yangekaa nyuma.

Madai yake anaacha parking kwa mbele.
Hiyo sio mbaya, utakuja mshukuru baadae.
 
Nilimpa Fundi ramani akaanza (akaseti) msingi nikiwa sipo.

Kurudi nakuta nyumba ameisogeza sana nyuma. Means makaro ya choo na sehemu ya kuanikia vitabanana upenuni (pembeni). Wakati kama msingi angesogeza mbele hayo makaro (sewage) yangekaa nyuma.

Madai yake anaacha parking kwa mbele.
Hilo sio la kujutia sana mkuu.
Kuacha parking kubwa ni muhimu hujui kesho mkuu
 
Ramani za wenzetu mbele huko store kwao sio muhimu kama laundry room ona hapo chumba cha katikati ya jiko na public toilet ni laundry room, mbongo angefanya hiyo iwe ni store

Halafu jiko ni open kitchen saafi kabisa.

Ramani simple na imejitosheleza kwa wale wa kipato cha kawaida inawafaa
Open kitchen kwa wabongo haifai, uchafu mwingi sana. Unaweza jaza moshi na harufu za samaki nyumba nzima
 
Open kitchen kwa wabongo haifai, uchafu mwingi sana. Unaweza jaza moshi na harufu za samaki nyumba nzima
Open kitchen inataka usafi sana. Na finishing kwenye jiko iwe ya maana hata mtu akikaa dining room avutiwe na mwonekano wa jiko

Screenshot_20220502-001231_Pinterest.jpg


Screenshot_20220510-065448_Pinterest.jpg
 
Hivi hapa bongo Kuna watu wanaweza kufanya finishing kama hizi?
Wachache sana na mara nyingi ni kampuni kubwa za ujenzi

Mafundi wa kibongo wa tiles na plumbing bado wengi kazi zao chafu, pia kwa upande wa materials wenye nyumba wengi wananunua za low quality

Kwa upande wa gypsum sasa hivi mafundi wa kibongo wanajitahidi naona improvement
 
Siriazi vyumba vitatu sqm 76!! Hapo sasa utakua umejenga nini!!,Hio nyumba itakua haina hewa kabisa na imebanana kila kona.standard vyumba vitatu ni sqm 150 ikiwa spacious inafika 200sqm,hii inaitwa medium size house.

Lakini kila mtu ana mapenzi yake ,kiukweli sipend nyumba yenye vyumba vidogo sana hii ni kutokana na nyumba niliyokulia kwa wazee,kipind hicho nipo form 6 naona kabisa chumba ni kidogo hakina hewa vitu vimebanana nikawa najisemea ikitokea nimefanikiwa kujenga yangu huko badae ntaongeza kidogo ukubwa.ila sio mita 5 hizo ni nyingi labda kwa masta.

Asikuambie mtu kuna raha ya kulala kwenye chumba kikubwa chenye hewa .
Vyumba vya watoto vinakuwa 3.5 m × 3.5m hiyo ni nje ya nafasi ya kabati ya ukutani ambayo unaiweka au nafasi ya choo. Ndio maana pakaitwa Bedroom sababu mule kinakaa kitanda basi na vitu vichache sasa kibongo bongo tunataka nafasi kubwa sababu tunapenda kujaza makorokoro chumba cha kulala.

Mimi makorokoro huwa sipendi ndani.
 
Tatizo kubwa tunalofeli watanzania ni upangiliaji wa vitu,sasa mtu unakuta kijiko chumbani ama jembe sebuleni linafanya nini!,jenga nyumba ndogo pangilia vitu vizuri utaondoa fikra za kujenga magodauni kwa kudhani ni nyumba
Toa basi mapendekezo /ushauri/utaalamu wako binafsi ili tujifunze kupitia wewe at least hata kwa mifano miwili mitatu.
 
Mojawapo ya makosa niliofanya
1. Vyumba vya kulala vidogo (3*3.5m)
2. Fundi wa kupaua kaharibu paaa
Vyumba ni vikubwa hivyo. Ila utakuwa unahifadhi makorokoro mengi ndani ndio yanakuletea shida.
 
Serikali sijui huwa inakwama wapi kupima maeneo ya viwanja vya makazi. Ujenzii holela ni janga nchi nzima
Hapa wa kulaumiwa ni raia kwanza then viongozi.

Raia anawajibu wa kutoa taarifa ya ujenzi kwa halimashauri na wilaya husika ili ujenzi ufanyike kwa kuzingatia standards za mipango miji.

Kuna mzee pale kigamboni kipindi ana hamia eneo lake hakukua na ujenzi na viwanja vilikuwa bado kabisa kuuzwa. So alichofanya akawapanga waliokuwa wanamiliki maeneo yale na kuomba wakubali kupangika kwa mpangilio wa mtaa na michoro yao ije fanyiwa survey na kuwa registered huko mamlaka husika kwaajiri ya kutunza rekodi.

Ule mtaa leo ukienda kule kigamboni ni miongoni mwa mitaa iliyopangika vizuri sana na hauna shida kabisa kuingia na kutoka nyumba zimekaa very Smart.

Viongozi na watendaji wa serikali kwa upande wao wanawajibu wa kutoka maofisini na kufuatilia maeneo mapya na kutoa maelekezo ya upimaji ili watu wasiuziane na kufanya ujenzi holela kwenye maeneo yao. Kila mtu ana akili yake wapo wenye busara atafikiria kuachia njia ila wapo vichaa wao kazi yao ni kuziba kila uwazi. Ukija kustuka eneo halina sehemu za wazi za watoto kuchezea, mitaa haitoki inaishia kwenye geti la mtu. Kuna nyumba hauwezi fika hata kwa bajaji maana kona ni nyingi na vichochoro na kumebanwa hata hewa tu hakuna.

Kimsingi inabidi sisi raia na hawa viongozi na watendaji wao wawe very serious na ufuatiliaji wa ujenzi ili usiwe wa kiholela.
 
Yes lakini pia licha ya uwezo tuweke pia provision ya kuweka hivyo vifaa hata kama kwa sasa hela huna. Mfano unajenga bafu basi weka provision ya heater au vyumbani weka provision ya AC, sio siku unapata hela ndio unaanza kuvunja tiles na kuta ili upitishe nyaya.

Mie nimeweka mpk pipes za internet ndani maana huwezijua kuna siku unaweza kuta zitahitajika halafu kwako kukaonekana kituko.
Ujenzi hautakiwi kukurupuka. Na usisubiri upate pesa ndipo uplan ujenzi wako utaanzaje. Muda mzuri wa kuplan nyumba ni pale ukiwa hauna hata mia mfukoni. Akili huwa inafanya kazi vizuri sana.

Haya ni mambo ya msingi ya kuyatafakari na haitakugharimu kuyafanya:

1. Kadiria mahitaji ya makazi yako je ni ya kudumu au unajenga makazi ya mpito huku ukiwa na plan ya kujenga makazi mengine ya retirement.

Mfano, unaweza kwa sasa kulingana na mazingira yako na hali ya uchumi ukawa unaona inakugharimu sana kupanga nyumba au kuishi kwa ndugu au nyumba ya familia so unahitaji kupata sehemu yako ya kuwa huru kwa muda ili uweze hata kupanga maisha yako vizuri. Hii itakusaidia ni ujenzi gani utafanya.


2. Ukishajua ni aina gani ya ujenzi unataka kufanya itakusaidia kujua ni ukubwa gani wa eneo utaanza nalo. Mfano unaweza kuwa unataka makazi ya mpito so hata eneo la Meter 15 kwa 30 likawa ni sawa tu maana unajenga makazi ya kukuficha kwa muda wakati ukikusanya nguvu za kuanzisha sasa makazi ya kudumu au retirement home.

Au unaweza ukawa unataka kuanza straight ujenzi wa makazi ya kudumu so hata eneo utakalohitaji litatakiwa kuwa kubwa kwa size mfano meter 80 kwa 80 au hata ekari moja kulingana na mipangilio yako.

3. Ukishafahamu aina ya ujenzi unataka kufanya na eneo linalohitajika utakuwa sasa na nafasi ya kupangilia mkao wa makazi yako kwa mazingira ya nje na ndani. Nyumba itakaa kona gani au eneo gani. Makaro ya maji yatakaa wapi, tenki la maji utaweka wapi, parking ya gari ni wapi, na landscaping itakaa mkao gani geti litakaa upande gani na kadharika.

4. Jambo lingine muhimu la kutazama wakati utakuwa umeshajua makazi unajenga na mpangilio ni mahitaji yako. Kosa ambalo huwa linafanyika ni kuwahi kumaliza nyumba ili kuhamia ila tunasahau features za hiyo nyumba. Matokeo yake ndio unaingia katika nyumba inakosa sifa za kuwa nyumbani (home [emoji537] [emoji536]) inabakia kuwa jengo yaani building. Hii ndio inakufanya hata ukianza kuishi hapo mahala ukose amani na utulivu matokeo yake unaanza kupata msongo wa mawazo ukiwa kwako na hata furaha ya kuishi hauoni ila unashangaa ukienda kwa rafiki yako ambaye alituliza kichwa wakati wa ujenzi unapata amani sana katika makazi yake hadi unatamani mbadilishane makazi akupe kwake ubakie.


5. Vema sana kuchagua location nzuri ya makazi kulingana na mahitaji yako ya makazi. Mfano unanunua kiwanja uswahilini au high density area ila wewe si mtu wa kujichanganya na haupendi makelele, mazoea ya hovyo, kelele za muziki sijui Bar kelele za hovyo. Kuna maeneo ambapo ukienda kujenga na kuishi utasema upo ikulu. Kupo kimya hautasikia sauti ya msikiti, wala walokole wakiimba mapambio wala kelele za wala bata.

6. Ni vema kujua nyumba utaidesign vipi na hii ni rahisi na unaweza ifanya wewe mwenyewe hapo ulipo muda huu ukiwa hauna hata mia. Yaani ni simple, kwa kuchukua penseli na karatasi kisha jaribu kuingia mtandaoni na kutazama 3d plans za mijengo kulingana na idadi ya vyumba. Kisha kaa chini fanya rough sketch ya aina ya mpangilio wa nyumba utakuwa kisha chukua huo mchoro au michoro kaa na watu wenye akili timamu wanaoweza kutoa dosari na kukwambia hapa futa weka hivi kwa sababu moja mbili tatu ili kupata matokeo mazuri. Usiogope ni mara ngapi itakulazimu kufuta na kuchora tena sababu haikuhitaji kuwa mtaalamu wa uchoraji kufanya ni kazi ya kitoto sana hata darasa la pili wanaweza kuifanya.

7. Ukishachora na kufuta mara nyingi uwezavyo ma kujua michoro yako itakaaje na umejiridhisha kuwa hapa sasa huu mpangilio ni zero errors katika ujenzi then chukua huo mchoro tafuta hawa madogo wasanifu majengo wa mtandaoni ambao mnaweza kuonana na kuketi chini mkazungumza juu ya kuchora sasa ramani yenye mchoro wa 3d, Cost estimations (BOQ),na vipimo kabisa. Then mzungumze bei ya kukufanyia design ya aina ya mjengo unataka. Huo mjengo utamwambia sifa zake kama unataka zile za hidden roof au za mgongo wa tembo, unataka ghorofa au nyumba ya chini. Then muachie yeye sasa utundu wa kudesign muonekano mzuri kulingana na original idea ya mpango makazi wako.

Kuhusu swala la gharama tazama namna utazungumza nae na kama utaona ni kazi tafuta mtu unayemuamini akusaidie kunegotiate nae bei ya gharama ya usanifu. Wapo wanaoweza kufanya kwa 50,000,100,000,200,000,300,000 hadi laki 500,000. Jitahidi muongee na kuelewana kulingana na uwezekano wa kuifanya kazi yenyewe maana unaweza kuwa na maelekezo mengi sana kiasi kwamba akataka pesa ya juu ili akufanyie kazi nzuri,au ukawa very simple na direct hadi akawa hana kazi kubwa sana.

[emoji779]Angalizo fanya kazi na wasanifu majengo wasio kuwa na makampuni ya ujenzi ambayo yapo busy na ujenzi maana hawa wanakuwaga wajuaji sana na unaweza shangaa anakupangia nyumba kwa matakwa yake badala yako sababu ya Ego. Mimi nimepishana na kuwakataa wengi kwa tabia za ujuaji na kulazimisha ufuate anachotaka yeye kwa design zake na ukimuelekeza unachotaka anakuwa anafanya kazi kama analazimishwa na anataka bei iwe juu. Hawasikilizi mteja then wacustomize michoro kwa kuproject matakwa ya mteja.

8. Utakafanikiwa kumalizana na msanifu majengo then utakuwa umeshapata picha ya ujenzi wako utakwendaje kuanzia gharama zake na namna utafanyika. Huyu anayekuchorea atakuelekeza na kukupa plan ya phases au hatua za ujenzi ambazo hizi zitakusaidia kama utaamua kusimamia ujenzi wewe mwenyewe though ni vema kuwa na mkeo, mumeo wakati wa kupanga haya ili msaidiane kwenye ujenzi eneo la usimamizi au engineering incase hauwezi kumudu kuajiri mtu kusimamia ujenzi wako ila kama unae then mtaketi na kupanga nae namna kazi itaenda.

9. Ukishajua kuwa umetimizia haya itakuwa rahisi sasa kusema upo tayari kuanza ujenzi maana unampango mkakati wa kueleweka sasa kila utakachofanya hapa kitareflect au akisi Plan yako ya ujenzi makazi na sio kukurupuka kurupu kwa kushauriwa na kila mtu au kufuata mkumbo. Unasikia watu wananunua viwanja unakurupuka kuwahi chako kisha baadae unajiuliza why ulikurupuka kununua. Au unaanza ujenzi halafu umefika kwenye rinta unaanza jilaumu kuwa ungefanya hiki ama kile baada ya kutembelea site na washkaji na kuona dosari au kuona designs za wenzako.

Ujenzi hautaki pupa though unaweza kwenda haraka kama umejiandaa vema na kwa akili wasababu ukikosea kubomoa ni gharama na itakuuma na kuendelea ni maumivu maana unaona kabisa namna umevagaa majanga. So be very careful katika mipango yako ikiwa kwa wakati huu hauna hata kiwanja unaweza anza kupanga sasa na ukafanya kitu kizuri sana baadae.

Oh halafu nilisahau, pia zingatia sana gharama za ujenzi ili usiumie kama wengine waliokurupuka kwa kutafiti kwanza bei za manunuzi. Unaweza pata deal nzuri ya cement,tofali,nondo mbao na kadhalika kama utapeleleza vizuri na kukutana na wadau sahihi na ukakata bajeti yake chini kwa hata 60% ya cost ya original plan. Hii itategemea na wewe sasa na utafiti wako unafanyaje na unafanyia wapi. Ila kuwa makini tu usijeuziwa mali za wizi au utapeli. So kuwa makini.
 
Nilimpa Fundi ramani akaanza (akaseti) msingi nikiwa sipo.

Kurudi nakuta nyumba ameisogeza sana nyuma. Means makaro ya choo na sehemu ya kuanikia vitabanana upenuni (pembeni). Wakati kama msingi angesogeza mbele hayo makaro (sewage) yangekaa nyuma.

Madai yake anaacha parking kwa mbele.
Ungemwambia parking ya baba yako au?
 
  • Thanks
Reactions: Gru
Mi ilinitia wazimu nilinyanyua cha kishikaji... cement ikala mifuko 1160 nondo mchanganyiko tani 7 unusu tofali 11,700 nilijuta bado kifusi na mawe, marine board 78, kokoto 80qm, mchanga 100qm mbao , mirunda uwii... bado mzigo wa fundi ilikuwa shida...finishing ndio nilikaa na bank ili niwe na nyumba
Ulikuwa unajenga ghorofa la floor 30 au ghorofa ya aina gani hiyo hadi ikugharimu kiasi hicho?
 
Tofauti Elfu 11700 ni uwanja wa mpira wa miguu ulikuwa unajenga?
Hapa tumepigwa na kitu kizito. Naomba kutoa taarifa kwa mleta hoja aliyetangulia kuwa hizo tofali ni nyingi sana na hivyo vifaa alivyolist ni vingi sana ukilinganisha na uhalisia wa ujenzi unavyokwenda kikawaida.
 
Back
Top Bottom