Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Hujui ujenzi ukiingia utaelewa...

Ngoja nikusaidie msingi tu wenye mzunguko wa tofali 400 mara kozi 7 ni tofali 2800 za kulaza. Boma ni idadi hiyo hiyo ya mzunguko wa msingi yaani 400× kozi 17 = 6800 mpaka kufikia slab/ renta ukumbuke zote zimelazwa then juu mzunguko ni huohuo tena ila hapa ni za kusimama nchi 5 kama ni ghorofa moja ila kozi zinakuwa 10 piga hesabu na huku nilipunguza idadi ya kuta kupata nachotaka zilitumika 2100+ bado kuna vitu vingi sana sijagusia... ukiona mtu kaweka floor kadhaa mpe heshima yake.
Uliweka floor ngapi wewe kama wewe tuache za wengine. Maana tukijadili za wengine watu wapo na mijengo tofauti.
 
Kuwa na slab haina maana hutafunga ceiling, washua wanafunga ceiling vizuri sanaView attachment 2500021
View attachment 2500024
Grill za ukweli balaa nimezipenda kiukweli. Ila chini ya slub hapo sijaona ulazima wa kuweka hizo boards maana ni extra but unnecessary cost. Maana kuna finishing ingepigwa hapo kwa kutumia ile material ya white cement ya kisasa plus wangetia na mauwa ya gypsum plus taa hapo katikati na kwenye kuta aaaaah ingekuwa si mchezo.
 
KOSA KUBWA AMBALO WAJENZI NA WAJENGEWA HUKIFANYA SIKU ZOTE;.
Ni kuharibu nyumba kuanzia kwenye msingi.
Nyumba sio chini ya 96% Tanzania, ujenzi wake umekosewa kuanzia msingi.

Msingi unatakiwa usiwe chini ya 60cm kutoka usawa wa Ardhi.
60cm ni sawa na laini 4 za tofali za nchi 6 au ngazi nne.

Kwani ni makosa kukosea msingi?
Unakosea msingi kwa mfano nyumba ikawa na laini 2 kutoka usawa wa ardhi;
1. Nyumba itapoteza uwiano kati ya msingi, boma na paa

2. Nyumba hukosa mvuto.
3. Mvua inaoonyesha matone yanayodondoka chini hurukia barazani au ukutani na kuharibu rangi.

4. Mara nyingi husababisha nyumba inakuwa fupi hivyo kuwa na joti kalu ndani.

...USHAURI;.Kabla hujaanza ujenzi pata ushauri wa kitalaam
Wait, yaani unaweka mawe kwanza, then unalaza zege halafu kuanzia hapo ndio hizo 60cm au iweje maana sijakupata vema kuwa msingi unaanzia juu ya usawa wa ardhi au kutoka chini ya ardhi hadi kufikia usawa wa surface ya ardhi?!

Hebu fafanua vema hapa.
 
Kosa ni lako, kabla ya kuanza ujenzi ilipaswa uangalie mrejesho wa ramani. Hii ni lazima, hata huyo uliemkabidhi ilipaswa akuhoji vitu flan ili ajue ukubwa wa chumba. Mfano chumba cha watoto unataka vikae vitanda vingapi vya ukubwa gani? Hivyo
Hawa wachora ramani hawana hata passion na kazi yao. Mtu anakuwa na pupa ya kukuonyesha uwezo wake hata kabla hajakusikiliza unataka nini.
 
Open kitchen kwa wabongo haifai, uchafu mwingi sana. Unaweza jaza moshi na harufu za samaki nyumba nzima

Yale majiko hayataki uchafu. Yanataka mtu msafi ambaye usafi kwake ni hobby sio kazi ya lazima. Utapenda jiko hilo ila hawa wanawake tunaokutana nao miaka hii akishashiba anapiga teke sahani na bakuli anajilaza kwenye sakafu anaperuzi Instagram hapo mtoto hajamkagua kama amejisaidia unatoka zako huko na wageni unafika ndio anajikurupusha jiko chafu machakula chakula kila kona, mtoto amevunda harufu ya maziwa, jasho na mikojo ya kwenye nepi zao hizi za kisasa zinazokusanya mikojo hata masaa...

Daaaaah basi tafrani. Tunajenga hizi nyumba ila mtu unatamani ubakie pekee yako saa zingine ili ufurahie uzuri wa nyumba yako.
 
Wachache sana na mara nyingi ni kampuni kubwa za ujenzi

Mafundi wa kibongo wa tiles na plumbing bado wengi kazi zao chafu, pia kwa upande wa materials wenye nyumba wengi wananunua za low quality

Kwa upande wa gypsum sasa hivi mafundi wa kibongo wanajitahidi naona improvement
Wachache sana wanaofanya kazi za plumbing na tiles kwa ubunifu, wengi wanafanya kama kazi ya kujikimu badala ya kazi ya ubora kwa wateja wao.
 
Wachache sana na mara nyingi ni kampuni kubwa za ujenzi

Mafundi wa kibongo wa tiles na plumbing bado wengi kazi zao chafu, pia kwa upande wa materials wenye nyumba wengi wananunua za low quality

Kwa upande wa gypsum sasa hivi mafundi wa kibongo wanajitahidi naona improvement
Yale mataa taa ndo wanajitahidi?
 
Vyumba vya watoto vinakuwa 3.5 m × 3.5m hiyo ni nje ya nafasi ya kabati ya ukutani ambayo unaiweka au nafasi ya choo. Ndio maana pakaitwa Bedroom sababu mule kinakaa kitanda basi na vitu vichache sasa kibongo bongo tunataka nafasi kubwa sababu tunapenda kujaza makorokoro chumba cha kulala.

Mimi makorokoro huwa sipendi ndani.
Chumba cha choo chatakiwa kiwe masters pekee ili kuangalia usafi wa watoto
 
Wachache sana wanaofanya kazi za plumbing na tiles kwa ubunifu, wengi wanafanya kama kazi ya kujikimu badala ya kazi ya ubora kwa wateja wao.
Halafu bado wengi wana mifumo ya kizamani kwenye kudesign mpangilio wa bafu, vyoo na kitchen
 
Niljenga nyumba kubwa kuzidi mahitaji wa familia yangu na uwezo wangu. Sebule kukwaa, jiko kubwaaa, dinning kubwaaa, stoo kubwaa na coridor kubwa mbele na na jikoni. mwaka wa 10 sasa nyumba haina finishing ya maana.

Mbaya zaidi nikaweka chumba kimoja tu kuwa self wakati vingine vyote vinne vya kulala vikitegemea bafu moja na choo kimoja. Ni makosa ambayo sitakaa niyafanye tena nikifanikiwa kukamata fyedhaa.
 
kibanda changu kina msingi ule wa chini na nilitaka iwe hivyo na sijutii

1. boma limezidi paa kiurefu, paa halijaenda juu sana
2. hmm, kimvuto, labda
3. nimeweka gutter, ni kweli matone yalikua yanadondokea kwa kibaraza
4. joto kali hapa ni uwongo, labda uweke madirisha ya vioo

baadhi ya jirani wamejenga nyumba za msingi wa juu, kwenye kuweka madirisha nyufa kila dirisha, ufa toka pembe ya dirisha mpaka chini

nilikagua kibanda changu kila sehemu ya dirisha kabla pasta na sikuona ufa wowote, nimepiga plasta sikuona ufa wowote ule
Una maanisha nini kusema msingi wa chini au wa juu, Ninachoelewa mimi msingi wa nyumba upo chini na ndio unabeba nyumba. Au msingi hasa ulimaanisha nn?
 
Yale mataa taa ndo wanajitahidi?
Bora umenisaidia kusema. Yaani watanzania wananishangaza sana when it comes to Interior design.

Ni mwendo wa kujaza Ma-gypsum yenye konakona na Mataa taa ya rangi rangi. And they do the same thing kwenye panel ya tv (showcase)... Na wao ndio wanaona wamepatia yani!!!

Sebule/nyumba inakuwa "very busy" unnecessarily....
 
Bora umenisaidia kusema. Yaani watanzania wananishangaza sana when it comes to Interior design.

Ni mwendo wa kujaza Ma-gypsum yenye konakona na Mataa taa ya rangi rangi. And they do the same thing kwenye panel ya tv (showcase)... Na wao ndio wanaona wamepatia yani!!!

Sebule/nyumba inakuwa "very busy" unnecessarily....
Inatakiwa iweje mkuu...tupe mfano
 
Back
Top Bottom