Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Mkuu hakijaribika kitu watoto wakihama napangisha mabinti wazuri wapate kunifanyia masaji
 
Yes lakini pia licha ya uwezo tuweke pia provision ya kuweka hivyo vifaa hata kama kwa sasa hela huna. Mfano unajenga bafu basi weka provision ya heater au vyumbani weka provision ya AC, sio siku unapata hela ndio unaanza kuvunja tiles na kuta ili upitishe nyaya.

Mie nimeweka mpk pipes za internet ndani maana huwezijua kuna siku unaweza kuta zitahitajika halafu kwako kukaonekana kituko.
Nimekuelewa sana hapa mkuu
 
Hongera sana mkuu, ni nyumba very spacious with all important modern ammenities. Pambana iishe. Kiukweli napenda nyumba sampuli yako in size.
Karibu na asante kunitia moyo... nawe nakuombea kwa Mungu akupe kwa kadri ya matamanio yako.
 
Nimegundua watu wengi wanajenga ili wasifiwe na walala hoi bila kujali hasa mtu anahitaji nini hasa!,nasema ni ushamba na ulimbukeni ndio unasumbua raia wengi!
Jenga nyumba ndogo nzuri mambo ya kujenga sqm 200 tuwaachie serikali wajenge shule sio nyumba za kuishi
Wewe ndo mshamba kwa kuona uchaguzi wa wenzako wa kishamba wako ndo bora zaidi.

Wewe kama unapenda ndogo ni wewe. Waache wanaopenda kubwa wafanye wakipendacho.
 
Though sijawahi kuwa na nyumba wala kujenga ila kosa ambalo siwezi kufanya ni kuachia upenyo wowote, nitajipanga vizuri na hela yao yote cash na nitakuwa nao site kufuatilia kila hatua huku nikiwa na nguo za kazi ikibidi kusaidiana nao kabisa.
Usipate homa kuna kipindi utapigwa tu, kijanja janja.

Utapunguza tu machungu utakapokuwepo site.
 
Kila mtu amalize haja zake chumbani kwake,
Kuna ubaya
Na wageni wapitanjia watakwenda wapi ikitokea dharura?

Ningekushauri (na ndivyo nilivyofanya mimi) choo kimoja cha master br, choo cha pili kwa kushare vyumba viwili na choo cha tatu kwa ajili ya wageni tu (kisitumike sana na familia labda kwa dharura). Hichi cha wageni wa kupita kiwe na toilet na basin ya kunawia mikono tu (hamna shower na mazagazaga mengine)
 
Nimegundua watu wengi wanajenga ili wasifiwe na walala hoi bila kujali hasa mtu anahitaji nini hasa!,nasema ni ushamba na ulimbukeni ndio unasumbua raia wengi!
Jenga nyumba ndogo nzuri mambo ya kujenga sqm 200 tuwaachie serikali wajenge shule sio nyumba za kuishi
Uzuri wa umasikini ni mnyororo mgumu sana kuukata.
 
Kujenga nyumba kwenye ardhi yenye kichunguu bila kutreat udongo au msingi wake na madawa ya kuua na kutokomeza kabisa mchwa, matokeo yake pamoja na kuweka tiles full lakini mchwa wanapenya kwenye vishimo na wanajenga ndani mixer kula mpaka vitanda na masofa ukishtuka na kuziba unakuta sehemu nyingine wanaibuka, na kwenye milango ndio kabisa frame ya mlango zinatafunwa ndani kwa ndani kama mikate,

sipati picha wakipenya ndani kwa ndani kwenye kuta na wafike juu darini, naogopa ipo siku gypusm board litanishukia maana wana njaa hao, kuna siku nilichelewa kusogeza kochi nikakuta wamelitafuna mpaka basi[emoji26]
Halafu mchwa walivyo na tabia mbaya wanatafuna ndani kwa ndani siku ya siku unashtukia unagusa ubao unabonyea
 
Hapa jirani yangu Dodoma Kuna jmaa anafunja nyumba yake kwani alimpa fundi kila kitu ili yeye aje achukue funguo tu nyumba ikisha jamaaa kufika kuchukua fungu akakuta sebule Ni ndogo kuliko choo na jiko Ni kubwa kuliko master

Na nyumba ikisha pauliwa kila kitu na kupigwa plaster
Hasra aliyopata hatokah hasau jamaa amemua kufunja baadh ya kuta na room ili kubalance ukubwa wa sebule iliyo ndogo Kama choo na choo kiko kikbwa kuliko sebule

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wewe mangi uandishi wako raha sana...sio kufunja ni KUVUNJA[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
KOSA KUBWA AMBALO WAJENZI NA WAJENGEWA HUKIFANYA SIKU ZOTE;.
Ni kuharibu nyumba kuanzia kwenye msingi.
Nyumba sio chini ya 96% Tanzania, ujenzi wake umekosewa kuanzia msingi.

Msingi unatakiwa usiwe chini ya 60cm kutoka usawa wa Ardhi.
60cm ni sawa na laini 4 za tofali za nchi 6 au ngazi nne.

Kwani ni makosa kukosea msingi?
Unakosea msingi kwa mfano nyumba ikawa na laini 2 kutoka usawa wa ardhi;
1. Nyumba itapoteza uwiano kati ya msingi, boma na paa

2. Nyumba hukosa mvuto.
3. Mvua inaoonyesha matone yanayodondoka chini hurukia barazani au ukutani na kuharibu rangi.

4. Mara nyingi husababisha nyumba inakuwa fupi hivyo kuwa na joti kalu ndani.

...USHAURI;.Kabla hujaanza ujenzi pata ushauri wa kitalaam
 
Kujenga nyumba kwenye ardhi yenye kichunguu bila kutreat udongo au msingi wake na madawa ya kuua na kutokomeza kabisa mchwa, matokeo yake pamoja na kuweka tiles full lakini mchwa wanapenya kwenye vishimo na wanajenga ndani mixer kula mpaka vitanda na masofa ukishtuka na kuziba unakuta sehemu nyingine wanaibuka, na kwenye milango ndio kabisa frame ya mlango zinatafunwa ndani kwa ndani kama mikate,

sipati picha wakipenya ndani kwa ndani kwenye kuta na wafike juu darini, naogopa ipo siku gypusm board litanishukia maana wana njaa hao, kuna siku nilichelewa kusogeza kochi nikakuta wamelitafuna mpaka basi[emoji26]
Mkuu kuna baadhi ya sehemu lazima ununue bidhaa bora ili kuepuka asala kubwa, frem ungejitaidi ungeweka za mbao ngumu ya mbuga na paa ungeweka mbao zenye dawa, kuna sehemu ukifika kwenye kujenga husimskmilize fundi na kufata ushauri wake ata kama hauna pesa bora utulie ujipange, kuna sehemu kwenye ujenzi ukinunu vitu vya bei chee tu lazima itakugharimu kama hapo kwenye frem na vitenda inaonekana umetumia mbao za viwango vya chini sana mpaka mchwa wanakula mbao, hiyo frem ingekuwa mninga mchwa wasinge jaribu kuusogelea wangepita mbali na kwenye fenicha pia.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Halafu mchwa walivyo na tabia mbaya wanatafuna ndani kwa ndani siku ya siku unashtukia unagusa ubao unabonyea
Tatizo la vijana wasikuizi hawajui kutofautisha ya aina ya mbao wenyewe wananunua tu bila kufahamu hii frem ninaweka kwenye nyumba yangu je ni imara wadudu wanaiogopa, kuna aina ya mbao mdudu haisogelei miaka na miaka.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Nilimpa Fundi ramani akaanza (akaseti) msingi nikiwa sipo.

Kurudi nakuta nyumba ameisogeza sana nyuma. Means makaro ya choo na sehemu ya kuanikia vitabanana upenuni (pembeni). Wakati kama msingi angesogeza mbele hayo makaro (sewage) yangekaa nyuma.

Madai yake anaacha parking kwa mbele.
Wakati wa kuset na kuchora ramani kwenye kiwanja jitahidi sana uwepo site
 
Back
Top Bottom