Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

mkuu Mimi ninahasira zakaribu namtu mwenyewe nimwana mke.bora kushindana namwanaume mwenzako kuliko mwana mke.unaweza kupiga mtu kofi ukaumiza ukajikuta uko kituoni..
Hata mimi anaenifanyia ujinga huo ni mwanamke akishirikiana na kaka zake wanaoishi mbali kidogo na site kwangu. Ila huyo mama ndo anaishi jirani na waliponiizia. Alafu ujue hawa akina mama baadhi yao hujiona sana na wanadharau sana kulingana na haki zao wanazolilia. Mimi ndugu yangu hunishindi kwa ghadhabu na maamuzi magumu, na hapo tu site kuna jiran alijenga fensi akaingilia na kuminya njia, nilipopata nafasi ya kwenda nikamuueleza akaleta nyodo, nilimuakia na kidogo nimuwashe vibao na tangia hapo heshima 100%. Hadi aliwaeleza na ndugu zangu walipoenda kutembelea site, muda huo mi nilishasepa huko na bahati nzuri hatufahamiani nao vizuri, wananijua kijuu juu tu. Ukiishi na majirani wasio na uelewa ni kero kubwa, ila mimi hizo kero ndo huwa nataka ili niwafundishe jinsi ya kuishi na watu.

Hasa ukijenga nyumba bora kidogo kuliko wao, hapo lazima chokochoko haziishi, na dawa Yao ni ku-deal nao tu perpendicularly.
 
1. Kumtafuta fundi ambaye ni ndugu yangu kwa lengo la kuokoa gharama. Aliharibu Foundation ya nyumba, alimanusura nibomoe jengo lote. Niliokoa baada ya kutafuta fundi mwingine.

2. Kujenga nyumba kubwa kinyume na uwezo.
 
Wakati najenga sikuwa na gari Ila njia ilikuwepo ya kufika na gari . Matokeo yake Kabla ya kuhamia Ile njia ikapotea hata pa kupita na pikipiki ilikuwa shida.

Sikuuza niliacha iwe sehemu ya kuniingizia kipato pia. Wapangaji wapo wenye mahitaji ya eneo kama lile.
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Ndio maana mimi nyumba yangu ina rooms 2 tu. Na appartments zingine 2. Hata plan yangu ya kudumu itakuwa hivyo. Watoto wakihama nimezeeka napangisha vijana wastaraabu kunitia joto
 
Kuanza kujenga kwa pesa za pension baada ya kustaafu.
Mzee wangu baada ya kustaafu alifanya hicho kitu. Ni hatari kupita maelezo. Kwanini?

1. Mhusika hashauriki, anataka tu kujenga kwa sababu ana pesa mfukoni.

2. Anachokijenga huwa hakieleweki au hakikamiliki. Anaamini pesa yake ya pension inatosha kufanya chochote au kila kitu kitawezekana. Anaokota ramani popote anataka kujenga.
 
Back
Top Bottom