Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kuna fundi kanijenge nyumba nikiiangalia siiamini, kuna ukuta mmoja mrefu balaa, Tumeforce kujenge nyumba ya kawaida kwenye slope tukikwepa kuweka basement.
Siiamini sana, ila nimechukulia kama pilot stage ya kujifunzia, Ikizingua naiedit kivingine
Sloped land changamoto saana hususan Kwa ujenzi wa kuunga unga
 
Kuamini mafundi nikiambiwa cement imeisha napiga simu tu inapelekwa bila kufatilia. Kuna siku fundi anapiga simu kuwa wamesimama kazi kwa kuwa cement imeisha inabidi ipelekwe haraka.

Ikabidi niende mwenyewe kuangalia kazi imefikiaje hadi cement kuisha hivo, nilivyofika mafundi wakastuka sana maana hawakutarajia kuniona kwa wakati huo. Ikawa kila ninapoingia kukagua jamaa kama ananizuga ili niache nimsikilize yeye. Nikahisi kitu nikaongeza umakini kuangalia chumba hadi chumba.

Bwana weee! Si nikakuta kuna mifuko 9 ya cement haijatumika wameificha kwenye chumba chooni. Asee jamaa alibabaika sana akakosa la kusema.
 
Aisee mimi sijui, ila fundi aliniambia tulisahau wiring ya solar, sasa alichomaanisha ni nini hapo?
hakuna mantiki ya kuweka wiring mbili zaidi ya kuongeza gharama

kinachofanyika ni kuweka 'change over switch' ya kubadili tanesco-solar mle kwenye DB (lile box lenye mifyuzi) na kama solar yako ni Inverterless, hapo utakua unabadili taa, unatoa za AC unaweka za DC ,

kama ni solar ya Inverter hapo hutabadili taa, zaidi fundi ataunga njia zinakazolishwa na solar mle mle kwenye DB kulingana na pendekezo la mteja pindi anapohamisha tanesco to solar
 
Kujenga wenye slope chini kabisa mita kama 75 kutoka kwenye bonde lenye kupitisha maji kipindi cha mvua kubwa , ila nashkuru kuna mtu alinibadilisha akili kunifanya kuona kama niko kwenye fursa,
Nikachimba bwawa la samaki, bustani za mbogamboga na mifugo kuku na nna mpango wa mbuzi….
 
Back
Top Bottom