Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Fundi wa Wiring alitokota. Heater za Maji moto zote zimeungua, AC imeungua, circuit breaker inasumbua na kujiswitch off kila mara kwenye kipindi hiki cha mvua. Radi ikipiga au kumulika Mbeya Mjini mimi huku Rungwe kanajiswitch off. Very interesting.
 
Pole sana
 

Naomba niulize hizi paa ambazo zimechongoka namna hii yaani ni karibia vertical zinatokana na nini? Ni fashion ya sasa hivi au kuna jingine? Hizi roof zingefaa sehemu zenye snow ili snow itereze isigandamize nyumba!
Pia bati hazivuji au kuoza
 
Kwa tunaoanza kujenga kwa mara ya kwanza...anza kwa kujenga kakibanda chako ishi humo then unaanza kujenga kile unachotaka (nyumba ya ndoto yako) polepole unakuwa umetuliza akili.
Ndicho nilichokifanya ,, i wish watu wangesoma hii comment kisha wakaifanyia kazi ,sina stress ya uhifadhi wa vifaa wala kuibiwa hovyo wala uharibifu mwingi ,, nyongeza nimezungusha fensi
 
Pia vyumba nilivyojenga vya uani baadae kimoja ni stoo, kingine ni jiko la nje (familia zetu jiko la ndani pekee ujiandae kwa uchafu mwingi na kuziba makaro na wadudu kama mende) na laundry room (hii room itakuwa na sehemu ya mashine ya kufulia , kupasi ,kuweka nguo chafu , kuweka nguzo zisizovaliwa tena (give away) nk

Epuka kujenga karo la kuoshea vyombo nje refu nimeona wengi sana wamekosea hili
 
Urefu kiasi gani usiohitajika
 
Naweza kukubaliana na wewe. TZ tuna changamoto ya mafundi. Yes wanajua kujenga. Lakini exposure ni tatizo. wazuri wapo Lakini ni wa kutafuta kwa tochi.

kuna mmoja nilikuta kafanya kazi kwa jamaa yangu nikampa kazi. Lakini Huwezi amini tulipelekana mpaka Polisi. Ukimpa pesa humuoni for the next five days.

kiukweli bongo ujanja ujanja siyo kwenye siasa tuu. Ni kila fani. Ingawa ujenzi ni zaidi.

quality bado sana. Ndo maana ukiangalia kwa umakini, finishing za maana ni kule kule wanakokaa wadosi…..
 
Mkuu hakuna anayemdharau fundi hapa. Huhitaji kuongea mengi. Wacha kazi ya mikono yako iongee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…