Nilitoka Ulaya nakiwa nime-save bilioni moja nikitaka nijengewe nyumba yenye ubora sawa na Ulaya. Mafundi wa Dar es Salaam ambar walikuwa wanafisiwa na watu wengi walinifanyia kazi ya hovyo kiasi kwamba maji ya moto yalikuwa hayatoki, nyumba inavuja, rangi haijapakwa vizuri. Tulikaa mwaka mmoja, tukaamua kuhama. Kwa kuwa kiwanja kilikuwa ni prime plot na ilinichukua miaka mingi kukusanya pesa za kukinunua. Sikutaka kuishi kwenye nyumba ambayo sikuwa na furaha. Nikaamua kuibomoa nyumba yote, nikakopa benki halafu nimkatafuta architect kutoka Afrika ya Kusini, nikachora ramani mpya. Nikatafuta kampuni ya ujenzi kutoka Cape Town (Wana uzoefu wa kujenga nyumba za kwenye fukwe au mija yenye joto). Nyumba mpya imenipa furaha kubwa. Somo: Mafundi na wachoraji wa ramani wetu (with all due respect) wanakosa exposure lakini wanaamini wanajua kila kitu. Tanzania tumejifungia Saną; tunahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine. Tunahitaji kuwatia moyo watt wasafiri kwenda Afrika ya Kusini, Kenya na kwingine kote tukiwa tumefungua moyo na akili wa kutaka kujifunza. Kama unataka prime property/high end house, nakushauri uangalie njee ya mipaka ya Tanzania.