Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Mzee hapa mbona ulilikoroga mwenyewe mapema tu...yani Ghorofa la vyumba 6 na watoto ni wakubwa uko serious au umeandika tu kuchangia mada?..

Alafu unamwambia kijana wa miaka 25 - 30 ambaye hana hata mtoto ajenge vyumba viwili?
 
😂😂😂😂😂

Polen saaana
 
Mzee hapa mbona ulilikoroga mwenyewe mapema tu...yani Ghorofa la vyumba 6 na watoto ni wakubwa uko serious au umeandika tu kuchangia mada?..

Alafu unamwambia kijana wa miaka 25 - 30 ambaye hana hata mtoto ajenge vyumba viwili?
ndio jambo ninalojutia, badala unipe moyo unazidi kushambulia.
 
fremu ya mlango inatakiwa kuwa size mmoja kuanzia juu, sehemu ya katikati hadi chini yani ile diameter. mfano upana wa katikati wa fremu ni 90cm, basi sehemu ya chini inabidi isome hiyo 90, juu nako ivoivo isome 90.

urefu wa kutoka juu hadi chini ya fremu inatakiwa na wenyewe ufanane. bahati mbaya sana mambo haya hayazingatiwi sana na mafundi na mabosi wengi hawayajui. matokeo ni milango kuwa na vipimo tofauti unaweza kupima katikati ya fremu ukakuta ni 90, ila ukipima upande wa juu ukakuta ni zaidi au chini ya hiyo 90, vivyoivyo kwa upande wa chini.

makosa haya yanatokana na fundi mjenzi kutozingatia vipimo wakati wa ujenzi. akija fundi selemala akakutana na haya mapungufu lazma atakulalamikia maana yanampa wkt mgumu kufanya kazi yake na kwa bahati mbaya hata yeye hawezi kurekebisha mapungufu haya atajitahidi tu kujazia au kupunguza mbao hapa na pale almradi tu mlango wako uweze kufunga.

milango km hii inaharibu shoo na balansi ya mlango na mara nyingi sio ajabu kukuta mianya mikubwa inayowezesha hata kumuona aliye ndani hata km mlango huo umefungwa.
 
Hadi sasa KUMUAMINI FUNDI 4 SABABU ZINGINE 0 mtanange bado unaendelea
 
Karibuni Nile house designs 🏠 🏠 🏠 🏠!!

kwa sasa tumeboresha huduma zetu Ili kukufikia mteja zaidi, tunatengeneza michoro na muonekano (3d) wa nyumba, majiko, sebule, bars, mandhari( landscape ) na huduma yoyote unayotaka kuanzisha,
Wasiliana nasi Leo tukupe huduma unayohitaji,

Call/Whatsapp 0715477041
 
Usije ukatumia pesa yooote kwenye ujenzi ukakaa usubiri muijiza.

Kwa mfano una 2mil unataka uingiize kwenye ujenzi. Tumia 1.5 tu 500k iweke pembeni.

Au una 20 Mil. Weka 15mil kwenye jengo 5mil iweke pembeni. Utanielewa baadae
Shukurani
 
Baada ya miaka kadhaa lazima waondoe huo ushamba. Huwa napenda sana design ya majengo ya waroma sijui wamishenari, majengo yao huwa na simple design ya nje na ndani ila hata ipite miaka 100, jengo bado linabaki likivutia na paa zao hata si za mikunjo na miinuko mikali.
 
Hicho ndo nilikuwa naongelea.
Kuna nyumba ukiziona ni kubwa ila amejaza mavumba tu ndani ceiling fupi, master haina closet, vyoo vidogo.

Mtu ana ghorofa ila hakuna AC hata 1
Hana Laundry room na Washer n Dryer, Steamer
Hana water treatment tank
Hilo tank la kutibu maji linakuwaje?.
 
Mkuu ingetotea saiv ndio unajenga ni nn kingine ungeonzea au kuounguza maana unamawazi kama yangu wiring ya data kwa Sasa Bora fibers au utp
 
Mkuu ingetotea saiv ndio unajenga ni nn kingine ungeonzea au kuounguza maana unamawazi kama yangu wiring ya data kwa Sasa Bora fibers au utp
Mambo yote ambayo unafanya mara moja tu kama wiring na plumbing ni muhimu kutumia muda sana.

Ningekuwa najenga sasa, ngepiga fiber ku future proof network. In fact nime augment network yangu na fiber kwa sababu natumia 10Gbps routers/switches/ NASes.

Nikifikiria sana, kwa matumizi ya kawaida, ukiwa na powerful wireless router utaweza kufanya mambo mengi kwa wireless. Devices zenyewe siku hizi zinakuwa wireless. Wiki iliyopita nimepewa Thinkpad X1 mpya kazini, haina hata network slot for RJ45, ni wireless tu, na inafanya kazi vizuri tu.

Tatizo linaweza kuja kama unatumia NAS na file transfer processes zinazohitaji speed kubwa utahitaji fiber.
 
Shukurani sana mkuu najiandaa mwezi ujao na ujenzi wa kuunga unga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…