Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kuna fundi kanijenge nyumba nikiiangalia siiamini, kuna ukuta mmoja mrefu balaa, Tumeforce kujenge nyumba ya kawaida kwenye slope tukikwepa kuweka basement.
Siiamini sana, ila nimechukulia kama pilot stage ya kujifunzia, Ikizingua naiedit kivingine
Huo ukuta aweke beams otherwise utakuja wadondokea sababu ya uzito wa paa
 
Kwa monitoring nzuri ya umeme wako wa solar....tumia wiring tofauti.
Labda kama utaamua kuunda backups ya umeme
 
Mwenzako anajuta kujenga basement wewe unaongelea basement haps
Mkuu ukijenga kwenye sloped land ni vizuri ukakadesign kajumba kako vizuri, underground inafanya usijenge limsingi likubwa kupitiliza, lakini unaweza kufanya design nzuri tu, chini sitting, dining, jiko, public toilet, store...then juu ukaweka bedrooms zako za kutosha. Sio lazima kujenga basement ya kufugia mbwa au kuku.
 
Basement na underground ni kitu like kile..ni maeneo yanayotumika Interchangably..issue ni gharama za kujenga hiyo basement..coz itahitaji msingi mkubwa pia na beams za kutosha..gharama ya kujenga vyumba viwili vya basement ni Sawa na gharama ya kujenga nyumba ya vyumba vinne hadi vitano kwa juu..Cha msingi epuka viwanja vya slope kama huna ela
 
Hiyo line ya mwisho ina mantiki saana.
 
Mjumba mkubwa hakikisha unaumalizia vizuri upendeze, la sivyo utauchukia. Kingine si tulikubaliana utazaa watoto wawili tu, sasa mjumba mkubwa wa nini[emoji1787]
Ni fantasy yangu asee...nyumba ndogo sipendi abadan

Hii haiusiani na mambo ya watoto, wabaki au wasepe hiyo ni shauri yao, mi napenda mavyumba makubwaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…