Zamani nilikua naona wanaoacha viwanja muda mrefu hawajengi kama wajinga flani hivi.
ila nimekuja gundua kuna maana kubwa sana ya kuacha kiherehere cha kuanza ujenzi kisa una pesa na unaweza.
Kile kiwanja nilinunua enzi ni pori la maana tu,haraka haraka kimbilia jenga..
Tangu zamani nilishasema sitowahi jenga uswahilini, ila sikua najua wanaojenga uswahili hawakuwahi waza kama patakuja kuwa uswahilini.
Baada ya ujenzi miaka kadhaa mbele ule mtaa haukua na tofauti na tandale, ule uswahili,vile vijumba vilivyokua vikichipuka kama uyoga nikajikuta nimewekwa mtu kati, nmezungukwa na vijumba vingiiiiiii...
Nikaona hapa Usintanie,Madalali kazi yao nini? Nikapauza kama palivyo.
Hela yote nimenunulia kiwanja sehemu nyingine, Sijengi ng'o mpaka nihakikishe ule mtaa ni wanaojielewa.
Ntapanga hivi hivi ila siwezi jenga mtaa ambao sina uhakika nawataokuja.
Hii mambo ya kuharakisha kujenga sehemu nyumba ya maana ndio unaweza jikuta unajenga mtaa kama kwa mtogole...
Baadae watoto wanakuuliza baba ilikuaje ukaja kujenga huu mtaa... Unakosa majibu.