Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Pia njia sio lazima ufungunge mfumo mzima wa solar, unaweza kufunga back za battery na inverter pekee zinajichaji wakati wa unaumeme wa January, ukikatika ngoma unawashwa
Kuna sehemu nilienda yule jamaa ana battery 50 za backup zinatoa 10KV
 
Likijaa hadi juu tegemea bomu .. presha ya maji na ukubwa wa mzingo 10,000 litres lazima liitike kama sio leo siku za mbeleni..

Ushauri wangu....
Usinunue tank...kubwaaa au usilijaze sana, Bora hata ununue mawili ya 5000litres each
Mbona letu mwaka wa 13 halijawahi tokea chochote na linajaa hadi maji yanamwahika?
 
Hii kuna rafiki yangu amejenga nyumba ya kisasa ila imekosa choo ndani..inamuuma saana...kwasababu alikua amejenga kidogo kidogo yani kwa kudunduliza...sasa kama unavyojua maisha yanabadilika...anajilaumu vibaya. Vyumba 5 ndani ila choo cha nje.
Hiyo ni guest house
 
Niliweka Master bedroon karibu sana na kitchen store na jiko, tatizo kubwa ninalopata ni ma house girl ninaopata wanaongea sana na simu hivyo room inakosa kabisa utulivu
Hukuona?
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka dah, mume wangu nae hapendi nyumba kubwa, wakat tunajenga tulibishana sana akajenga two bedrooms tu, saizi familia imeongezeka kichwa kinamuwaka moto [emoji119]
 
Watu wa namna hiyo huwa wachawi. Na mimi Kuna mmoja nakabiliana nae site moja hivi ila nilishamuueleza na ndugu zake kuwa Mimi ni kiboko ya wajinga km wao. Haiwezekani umuuzie mtu kiwanja na kumuonesha njia atakayokuwa anapita, then ghafla kwa sababu ya wivu na ushirikina wako baadae unaziba njia.

Kuuza site/nyumba kwa sababu za wajinga km hao ni uzembe. Mimi Sina mpango wa kuishi hapo leo wala kesho ila muda ukifika watanielewa tu. Mwakani tu nitaenda kuwaonesha show ya kiutu uzima.

Huwezi kuishi kwa kumuogopa mwanadamu mwenzio, na bahati mbaya tu nipo mbali ningewanyoosha.
Kuna ndugu alinunua eneo la familia aliuziwa na mama mwenye eneo ... mama hakushirikisha binti zake... Kitendo cha kuanza kujenga tu ndugu hao,mara kwa mtendaji mara kwa wazee wa eneo husika.....kijana akaenda kwao akawaleta wazee wa kwao yani wazee hata kutembea hawawezi.... Mama akaulizwa eneo la nani...akajibu lake mwenyewe na kaliuza kwa ridhaa yake...wazee wa hapo na mabinti wakaulizwa nyie kipingamizi chenu ni nini? Mabinti wakadai eti ni urithi wao...wale wazee wakawambia hayo malizaneni wenyewe.....Wazee wakaacha onyo....wao wanaondoka na kijana wao anaendelea kujenga, mkimsumbua mtakuwa mnafanya Kazi ya kuuguza na kuzika mpaka muishe wote.....kwanzia hapo kijana alipata ushirikiano mpaka kwa mtendaji...kila hatua walikuwa wanakuja kuangalia anaendeleaje.
 
Back
Top Bottom