Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Wakuu natamani kujenga nyumba simple ya kuanzia maisha nijenge vyumba vingapi niliwaza nijenge vyumba viwili na self container na kajiko vipi hapo?

IMG_8479.jpg

Angalia hii
 
Vyumba viwili..cha master na Cha wa watoto..Bila jiko wala stoo..yaani najuta japo nilikuwa nilikuwa nabana matumizi kipindi najenga..
Nimeamua kujenga kajumba kengine kadogo nje kawe ka wageni au watoto wa kiume
Kwa malengo ya upangishaji baadae,hii ni nzuri,km utaamua kujenga tena nyumba ya ndoto yako hyo ya two rooms utaitumia kibiashara
 
Nilichofanya sasa hivi nimenunua kiwanja hadi na njia ya kunipeleka main road...

haikua njia nimenunua in terms ya viwanja vya 5 kwa 10, nikaenda mbele tena nkakuta 5 kwa 15 nikaenda hvyo hvyo hadi cha kule mbele kilikua na 10 kwa 12 ... vyote hvyo si vya kujenga kitu ila n njia yangu ya kupita na kutoka na gari, Hajengi KIMA yoyote wala otesha mti nyau yoyote yule.

na hamna anaejua nmevnunua viwe njia wote wanajua n viwanja ntakuja jenga mabanda ya kuku.
kuepukana na complications zote hizi nunua plots ambazo ZIMEPIMWA, plot ambazo zimepimwa hakuna hizi habari za kujikuta umezungukwa na waswahili, sijui barabara hakuna

ni gharama ila it is worth it
 
Kama una shimo lubwa kwenye msingi, unaweza kulitumia kama septic tank au kiaima cha maji, lakini hii lazima plan ianze wakati unaaanza kujenga.

Unaweza kuweka shimo la choo kwenye msingi na bado ukawa na hivi vyoo vya kawaida vya kuflash.

Watu qenye viwanja vidogo pia huwa wanaweka mashimo yao kwenye msingi wa nyumba

Kuna nyumba zingine huwa wanaweza visima
Yani unakaa juu ya maji?
 
Kuajiri plumber uchwara. Kuta maji yanavuja rangi imebanduka sana
Kitu kama hii ilinikuta, fundi anafix toilet sink kwa kusakafia na cement! sink la kunawia mikono anafi kwa vipande vya bomba la maji! Daah! ilibidi niite plumber mwingine akarekebisha kwa gharama mara mbili ya ile iliyotumia mwanzo! Nimekoma mie!
 
Hili nalo, watu tunajenga tukiangalia leo badala ya miaka 20 ijayo, laundry room ni muhimu hata kama huna washing machine leo, miaka ijayo utainunua!!

Washing mashine unaweza weka hata jikoni ukai fix vizuri tu ikakaa. Cha msingi kama chumba cha dada au kaka wa kazi kikubwa weka meza ya kunyooshea nguo
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako
Baya zaidi watoto wanafikia kuhamia makwao kabla hata nyumba hujaimaliza finishing!
 
Upo sahihi mkuu mazoezi ni muhimu

Sema wazee wameamua kuhamia chini sio kama hawawezi kabisa kupanda hapana ila wameamua hivyo kwakua wanaona usumbufu wa kupanda na kushuka ngazi kila siku plus risk za kudondoka na kuanguka

si unajua tena uzee injury ndogo tu inaweza ikakuletea madhara makubwa tofauti na atakayopata kijana ambaye bado ana nguvu
Kama unauwezo wa kujenga nyumba ya ghorofa 1 mfano, uwe na master bedrooms mbili. Moja juu na moja chini.
Ukizeeka au kupata changamoto ya kiafya una hamia master bedroom ya chini.
 
Mnaejenga mijumba mikubwa mjitafakari mambo yamebadilika siku hizi hakuna kutembeleana ovyo wala kuishi kwa ndugu kama zamani na watoto wakikua wanakimbilia sehemu nyingine kutafuta maisha ,kwahiyo utabaki na jumba kubwa kama msikiti peke yako

Ingekua vizuri ungetuambia nyumba kubwa inaanzia ukubwa wa sqm ngapi ili tuelewe zaidi? au ina vyumba vingapi?
 
Ingekua vizuri ungetuambia nyumba kubwa inaanzia ukubwa wa sqm ngapi ili tuelewe zaidi? au ina vyumba vingapi?

Unapojenga zingatia vipimo SQM ni lazima upange ziwe ngapi kwenye nyumba nzima!,sasa mtu anaweza akajenga nyumba ya vyumba vitatu tu lakini ina SQM 150 sasa unajiuliza huyu mtu ametoka kwenye hospital ya vichaa ama vipi![emoji276]wakati unaweza ukajenga nyumba ya vyumba vitatu kwa Sqm zisizozidi 76,hivi unapojenga chumba kimoja mita 5 unataka tuzo ama vipi?
Kila siku nasema nyumba kubwa ina faida sana kuwatajirisha wauza vifaa vya ujenzi kuliko mwenye nyumba
 
Back
Top Bottom