Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Niljenga nyumba kubwa kuzidi mahitaji wa familia yangu na uwezo wangu. Sebule kukwaa, jiko kubwaaa, dinning kubwaaa, stoo kubwaa na coridor kubwa mbele na na jikoni. mwaka wa 10 sasa nyumba haina finishing ya maana.

Mbaya zaidi nikaweka chumba kimoja tu kuwa self wakati vingine vyote vinne vya kulala vikitegemea bafu moja na choo kimoja. Ni makosa ambayo sitakaa niyafanye tena nikifanikiwa kukamata fyedhaa.

Linyumba likubwa hivi unapeleka wap boss!! Jenga nyumba y kawaida lakini iwe na vitu vya msingi na yenye muonekano mzuri bila kuacha nafasi ya garden na kufanya shughuli nyingine ndog ndog
 
Mume wangu kuweka siling board ina angusha chokaa, wakati wa ku-duu nikiangalia juu yaani kifo cha mende viuchafu vinaangukia machoni
Hapa Naona Tatizo ni Staili, Jaribu Kubadilisheni Staili na Uikatae Death of Cockroach [emoji3][emoji3]
 
Ulitumia mashine ya umeme yenye mixer na vibrator au ile shindilia ya mkono (bambam)? Ulinunua au ulikodi?

Kuna gharama ya kununua mchanga, cement, vibao, maji ya kumwagilia, gharama ya kuwalipa wafyatua tofali, vibao vya tofali na gharama ya umeme kama utatumia vibrator na mixer


Ili utoe tofali 3000 kwa ratio ya 40 utahitaji cement mifuko 75 (cement 1@16,500)
●Mifuko 75@16,500= 1,237,500

Mchanga wa tofali 3000
●Mchanga mnene trip 2@400,000= 800,000 (FAW ton 20)
●Mchanga mlaini; Bagamoyo/Kibaha trip 1@350,000 (SCANIA mende)

Gharama za wapiga tofali (Mfuko 1@4000)
●Mifuko 75@4000=300,000

Kibao 1@1700
●Vibao 1000@1700=1,700,000


HADI HAPO TAYARI 4,387,500
SIJAHESABIA GHARAMA ZA KUKODI/KUNUNUA MASHINE, MAJI NA UMEME

UKINUNUA TOFALI 3000@1100 NI 3,300,000

NB: GHARAMA INATEGEMEA NA ENEO HUSIKA HIYO HESABU NI KWA MKOA WA DAR

Sasa apa uyo anae kuuzia ina Mana kazalisha kwa 4m plus Kwann aje akuuzie kwa 3m plus mkuu [emoji28]
 
fixed ukutani, imejengewa.
Inawezekana kutolewa sasa mpk saa za kutundika ukutani tutasema kosa la kiujenzi. Hapa tunaongelea vitu kama ukubwa wa chumba, kosa la kuweka madirisha madogo, kusahau kuweka stoo ya chakula n.k ila sasa Tv si unaondoa tu swahiba zile ni fittings tu
 
Back
Top Bottom