Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Nyumba msingi... mfano nyumba ya 104.5 sqm (9.5mx11m) inaweza kutumia tofali 3500 za 6" kwa maana ya kozi 7 za kulaza mzunguko wa nje na kuta za ndani. Kokoto 25qbm hii ni kuanzia kizege cha chini na kumwaga jamvi mchanga 20qbm bado simenti ya kujengea si chini ya mifuko 35 bado jamvi kama mifuko 220 uweke marine bodi ni kama 15 zitazo chanywa, misumari, nondo, mbao za setting na mirunda ya kushikia marine. Hela ya mafundi, maji nk ....ukiviweka vyote 7m ni kawaida sana.
Msingi wangu nakumbuka ulikula 10M hadi boma linasimama ilikula 18M+ gharama zote za ufundi na material
 
Niliunganisha waya za speakers nyumba nzima niweke mtandao wa speakers ukutani, halafu nikaghairi.

Nilifanya second living room (morning room) isiwe na TV/ internet ports kwa kutaka iwe quiet room, halafu baadaye nikaghairi.

Somo.Fanya maamuzi ya wiring kwa uangalifu sana, mara nyingi ukiwa unajenga ndiyo wakati mzuri kabisa wa kufanya maamuzi ya wiring zote, ukishajenga unakuwa uashapoteza nafasi ya kufanya wiring vizuri.
 
Ni njia nzuri sana nimeitumia kwenye material ya dukani kwa hapa Moro kuna duka la Kilosa hardware jamaa yuko poa alikaa na pesa yangu almost mwaka mzima nikijipanga muda ulipofika yaani hata hakuwa na shida kabisa kikubwa uwe na vikaratasi vyake alivyokuandikia kama lisiti kipindi unalipia na upande wa matofali nilifanya hivyo hivyo kule Pangawe jeshini. Utaratibu huu ulinifanya nijenge nyumba faster sana from september 2022 na mwezi May mwaka huu (2023) nimehamia kwangu japo sijaikamilisha baadhi ya mambo. Kiukweli namshukuru Mungu nainjoi upepo wa milima ya uluguru nikiwa kwangu view nzuri ya mji kasoro naifaidi vilivyo hasa kipindi cha usiku kwani saiti yangu ipo kwenye mwinuko.

Ni nyumba ndogo ya kawaida yenye vyumba viwili kimoja master, choo kikubwa cha public, jiko, sebule na vibalaza viwili.

Imetumia matofali 2840, inchi 6 kwa ajili ya msingi 900 yalibaki kidogo, inchi 5 kwa boma 1940, mabati ya migongo mipana 80 yalibaki 6, mabati ya migongo midogo kwa ajili kofia 11 na mbao 360 nazo zilibaki kidogo nazitumia kwa ajili ya majukwaa kwenye plaster n.k
Hongera sana mkuu,umepiga hatua kubwa mno.
 
Hii misingi yenu mnajengaje?
Mimi pia nimeshindwa kuelewa labda kila kitu wananunua, maji, mchanga, mafuta ya gari ya mchanga etc, ni vema kunimprovise eneo la bajeti na malipo ya vifaa vya ujenzi.
 
Usiwaamini sana mafundi wa kitaa. Kama una hela tumia professional fundi au engineer. Napambana na sisimizi haijawahi tokea. Marumaru hadi natamani nibomoe nianze upya space kati ya tile na tile walibana sana kiasi kwamba grout haikai matokeo yake space ni nyingi na sisimizi wanatokea humu. Fundi rangi pia naye ni shida pia nilimwamini sana fundi wangu lakini nimekuta baadhi ya vitu hajui. Kama issue za Marumaru, rangi, furniture nk.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
Kwamba huyo professional ndo anajenga?

Hujui hao huwa kazi yao kushika makaratasi tu?
 
Ahsante mkuu wangu, niliona kuanza na nyumba ya ndoto itanichukua muda wa kutosha.
Ni kweli mkuu na kama kipato siyo kikubwa unaweza kujikuta unakata tamaa. Uzuri wa nyumba ni kuijenga iishe mapema ili ule uzuri wake usipotee.
 
Ni njia nzuri sana nimeitumia kwenye material ya dukani kwa hapa Moro kuna duka la Kilosa hardware jamaa yuko poa alikaa na pesa yangu almost mwaka mzima nikijipanga muda ulipofika yaani hata hakuwa na shida kabisa kikubwa uwe na vikaratasi vyake alivyokuandikia kama lisiti kipindi unalipia na upande wa matofali nilifanya hivyo hivyo kule Pangawe jeshini. Utaratibu huu ulinifanya nijenge nyumba faster sana from september 2022 na mwezi May mwaka huu (2023) nimehamia kwangu japo sijaikamilisha baadhi ya mambo. Kiukweli namshukuru Mungu nainjoi upepo wa milima ya uluguru nikiwa kwangu view nzuri ya mji kasoro naifaidi vilivyo hasa kipindi cha usiku kwani saiti yangu ipo kwenye mwinuko.

Ni nyumba ndogo ya kawaida yenye vyumba viwili kimoja master, choo kikubwa cha public, jiko, sebule na vibalaza viwili.

Imetumia matofali 2840, inchi 6 kwa ajili ya msingi 900 yalibaki kidogo, inchi 5 kwa boma 1940, mabati ya migongo mipana 80 yalibaki 6, mabati ya migongo midogo kwa ajili kofia 11 na mbao 360 nazo zilibaki kidogo nazitumia kwa ajili ya majukwaa kwenye plaster n.k
Jumla ya tofali umetumia ngap nyumba nzima mim Niko moro huku nanenane natarajia kujenga kama yako two rooms
 
Wakuu naomba msaada hii inshu mashimo sewage system ya vyoo yasiyojaa au wanasema hayana harufu sana. Haya mashimo ynayopigiwa pambio kila sehemu mitandaoni. Naomba experience ya aliyejenga.
 
Back
Top Bottom