Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kipindi nasoma A level kuna Aunty yangu alinikopa hela tena ilikuwa ada ya shule ili afanye kama mtaji wa kuanzisha biashara yake ya kuuza mashuka ya mitumba akasema atairudisha kabla hatujaanza kufanya mitihani ya mwisho wa muhula.

Tukazungushana wee kumbe hakuna cha biashara wala nini. Sijui ile pesa alipeleka wapi hajawahi kunirudishia. Ila alipiga simu nyumbani kuwaambia nimepoteza ada na ninaogopa kusema.

Ikabidi na mimi nikae kimya hadi ili ilipwe kwa sababu it was my word against hers na yeye alikuwa mtu mzima sana.

Hadi leo siwezi kopesha ndugu hela bora nimpe tu nijue nitoa sadaka
 
Kudharau mtu akieleza kuhusu Afya yake, kuna sehem nlikua nafanya kazi jamaa mmoja akawa analalamika anaumwa mara kwa mara watu wakaona ni mvivu anatafuta sababu tu ya kutokufanya kazi.

Mara ya mwisho alisema anajiskia vibaya alivyoondoka huku nyuma watu wakawa wanamtuhumu anajisingizia maradhi jioni yake tukaskia amefariki.
 
Serious hii ipo sana
 
Kipindi nasoma A level kuna Aunty yangu alinikopa hela tena ilikuwa ada ya shule ili afanye kama mtaji wa kuanzisha biashara yake ya kuuza mashuka ya mitumba akasema atairudisha kabla hatujaanza kufanya mitihani ya mwisho wa muhula.

Tukazungushana wee kumbe hakuna cha biashara wala nini. Sijui ile pesa alipeleka wapi hajawahi kunirudishia. Ila alipiga simu nyumbani kuwaambia nimepoteza ada na ninaogopa kusema.

Ikabidi na mimi nikae kimya hadi ili ilipwe kwa sababu it was my word against hers na yeye alikuwa mtu mzima sana.

Hadi leo siwezi kopesha ndugu hela bora nimpe tu nijue nitoa sadaka
Hiki kama kisa changu afadhal wako alpga cm nyumbn
Huyu wangu alikaa kimya na nilipomwambia hayo maneno aliongea nilienda kulilia chooni.....usikopeshe pesa ndugu.

Huyu ndugu yangu alinikopa pesa ambayo ni ya Ada nilipewa na baba
 
Back
Top Bottom