Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Kudharau mtu akieleza kuhusu Afya yake, kuna sehem nlikua nafanya kazi jamaa mmoja akawa analalamika anaumwa mara kwa mara watu wakaona ni mvivu anatafuta sababu tu ya kutokufanya kazi.

Mara ya mwisho alisema anajiskia vibaya alivyoondoka huku nyuma watu wakawa wanamtuhumu anajisingizia maradhi jioni yake tukaskia amefariki.
Ilitokea kazini kwetu mwaka fulani , mpaka leo tunajilaumu sana kumbe alikua anaumwa kweli aisee!
 
Hii nayo inatutesa wengi!
Moja ya udhaifu mkubwa unaotukabili ni kupenda engo ya mapenzi..
Ningekuwa na uwezo ningeacha kupenda.
Ahhahaha kwangu naona imezidi ase kuna kipind inafika unashindwa jizuia kabisa
 
Kipindi nasoma A level kuna Aunty yangu alinikopa hela tena ilikuwa ada ya shule ili afanye kama mtaji wa kuanzisha biashara yake ya kuuza mashuka ya mitumba akasema atairudisha kabla hatujaanza kufanya mitihani ya mwisho wa muhula.

Tukazungushana wee kumbe hakuna cha biashara wala nini. Sijui ile pesa alipeleka wapi hajawahi kunirudishia. Ila alipiga simu nyumbani kuwaambia nimepoteza ada na ninaogopa kusema.

Ikabidi na mimi nikae kimya hadi ili ilipwe kwa sababu it was my word against hers na yeye alikuwa mtu mzima sana.

Hadi leo siwezi kopesha ndugu hela bora nimpe tu nijue nitoa sadaka
Ukiwa nae sehemu moja unamwangaliaje?
 
Back
Top Bottom