Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Kudharau mtu akieleza kuhusu Afya yake, kuna sehem nlikua nafanya kazi jamaa mmoja akawa analalamika anaumwa mara kwa mara watu wakaona ni mvivu anatafuta sababu tu ya kutokufanya kazi.

Mara ya mwisho alisema anajiskia vibaya alivyoondoka huku nyuma watu wakawa wanamtuhumu anajisingizia maradhi jioni yake tukaskia amefariki.
Maskini nimeumia, apumzike kwa amani 🙏
 
Kipindi nasoma A level kuna Aunty yangu alinikopa hela tena ilikuwa ada ya shule ili afanye kama mtaji wa kuanzisha biashara yake ya kuuza mashuka ya mitumba akasema atairudisha kabla hatujaanza kufanya mitihani ya mwisho wa muhula.

Tukazungushana wee kumbe hakuna cha biashara wala nini. Sijui ile pesa alipeleka wapi hajawahi kunirudishia. Ila alipiga simu nyumbani kuwaambia nimepoteza ada na ninaogopa kusema.

Ikabidi na mimi nikae kimya hadi ili ilipwe kwa sababu it was my word against hers na yeye alikuwa mtu mzima sana.

Hadi leo siwezi kopesha ndugu hela bora nimpe tu nijue nitoa sadaka
Huyo Mshangazi alikuwa na roho ngumu sana, hapo huenda kuna kitu kilimsukuma kufanya hivyo, sio bure kufanya hivyo.

Nawaza laabda aliwahi kugombana na Kaka yake(baba yako) na akaamua kulipa kisasi kwa namna hiyo. Kitendo cha yeye kutoa taarifa kuwa umekula Ada kinadhihirisha hii scenario kwa kiasi chake.
 
Kushuka kwenye daladala kabla haijasimama🤣
Iliwahi kunitokea hii huwa nashuka mara nyingi tu ila ni mwendo ukiwa kawaida siku nilipitishwa kituo kdgo nikasema siwezi shuka kituo kinachofuata acha nidrop weeeeeh! Ilikuwa htar kw ule umbali niliokimbia ili kwenda sawa na ile spid ya gari nilijkuta niko kituo kile nilchgoma kwenda kushuka na sikuw nakimbia kawaida yani ni km wale jamaa wa marathon m100 wanapomalizia ule mstari wa mwisho
 
Kudharau mtu akieleza kuhusu Afya yake, kuna sehem nlikua nafanya kazi jamaa mmoja akawa analalamika anaumwa mara kwa mara watu wakaona ni mvivu anatafuta sababu tu ya kutokufanya kazi.

Mara ya mwisho alisema anajiskia vibaya alivyoondoka huku nyuma watu wakawa wanamtuhumu anajisingizia maradhi jioni yake tukaskia amefariki.
Hii imemtokea dgo niko na mtaani akiwambia wenzie mguu unamuuma wanamuita mvivu alianza sister kabisa wa kuzaliwa nae kumuona dgo mvivu alikuwa anaishi nae dgo ikabidi ahamie ofsini raia wakazidi kumuandama kuwa mvivu kuna watu wameumbwa na mioyo yao wanakosa uwezo tu kuna bimkubwa alimpa 50k aende hsptl mpka muda hu tunavyozungumza dgo amekatwa mguu kumbe ilikuwa kansa
 
Back
Top Bottom