Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Ni kosa gani umewahi kufanya na hauwezi kulirudia tena kwenye Maisha yako?

Huyo Mshangazi alikuwa na roho ngumu sana, hapo huenda kuna kitu kilimsukuma kufanya hivyo, sio bure kufanya hivyo.

Nawaza laabda aliwahi kugombana na Kaka yake(baba yako) na akaamua kulipa kisasi kwa namna hiyo. Kitendo cha yeye kutoa taarifa kuwa umekula Ada kinadhihirisha hii scenario kwa kiasi chake.
Mashangazi wengi wanoko na fitina nyingi, hata umtendee jema lipi atakukomoa tu so unaweza kuta ni hila zake
 
Kuacha chuo semester ya mwisho bila sababu ya msingi.
Duh.. Kuna mwanangu alinacha chuo wiki mbili tu kabla ya UE ya mwisho ya mwaka wa 3.
Nilisikitika sana.

Sijui kama ameshawahi kujutia au la. Hawezi kuniambia maana sikumuunga mkono hata kidogo.
 
Duh.. Kuna mwanangu alinacha chuo wiki mbili tu kabla ya UE ya mwisho ya mwaka wa 3.
Nilisikitika sana.

Sijui kama ameshawahi kujutia au la. Hawezi kuniambia maana sikumuunga mkono hata kidogo.
Mkuu acha kabisa, mwenyewe niliacha week moja kabla ya mtihani wa mwisho, kujuta lazima hasa maisha yakikuchapa.
 
Kosa nililofanya ni kupuuzia red flags mwanzo wa mahusiano.
Nilikuwa nina kiu sana ya kupata mtoto, so nikawa napuuzia mawenge ya huyo manzi.
Lakini leo hii siishi hata na huyo mtoto mwenyewe.
 
Mashangazi wengi wanoko na fitina nyingi, hata umtendee jema lipi atakukomoa tu so unaweza kuta ni hila zake
Hapo ndio tunaona hila zake wazi wazi, iweje mtu mzima ukope hela ya Ada ya Mwanafunzi halafu baadae uanze kusema uongo mbele ya wazazi wa mtoto.

Bora angesema amepata hasara tofauti na alivyotarajia, yeye kauchuna halafu anaenda kusaga kunguni
 
Kudharau mtu akieleza kuhusu Afya yake, kuna sehem nlikua nafanya kazi jamaa mmoja akawa analalamika anaumwa mara kwa mara watu wakaona ni mvivu anatafuta sababu tu ya kutokufanya kazi.

Mara ya mwisho alisema anajiskia vibaya alivyoondoka huku nyuma watu wakawa wanamtuhumu anajisingizia maradhi jioni yake tukaskia amefariki.
Dah
 
Kumkopea mtu pesa maana kwa sasa kama sina ni sina.
 
Hapo ndio tunaona hila zake wazi wazi, iweje mtu mzima ukope hela ya Ada ya Mwanafunzi halafu baadae uanze kusema uongo mbele ya wazazi wa mtoto.

Bora angesema amepata hasara tofauti na alivyotarajia, yeye kauchuna halafu anaenda kusaga kunguni
Shangazi ni muuaji kakosa sumu tu
 
Back
Top Bottom