Tatizo una akili ambazo unafikiri Kwa kutumia masabuli!!
Mm nimezaliwa Familia maskini kabisa!!
Tena Baba allinikataa! na Mama aliolewa na mwanaume mwingine. Hivyo Mimi nilelewa na Bibi Mungu amlaze mahali pema Bibi yangu!!
Niliishia Elimu ya msingi. Lakini nilisoma QT mjini Moro Kwa Rikado maria,( peku peku) niliishi Moro takribani miaka 19
Nikijidhughulisha na shughuli mbali mbali. Ikiwepo kufuga kuku, na nilipata tenda ya kupeleka nyama ya ngo'mbe kwenye chuo kikuu kimoja hapo mjini Moro.
Lakini alikuja COVID-19 ilinirudisha nyuma Kwa kiasi kikubwa!! Sikukata tamaa!! Nikarudisha mpira Kwa kipa. Nikarudi Singida. Singida tuna neema ya mabwawa mengi!! nikajiingiza kwenye shughuli za uvuvi. Kwa kifupi mpaka Sasa namiliki million 50 nipo Tabora Loya..
Acha kukariri dogo! Mungu ni mwema Kwa Kila mtu!!