Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Ajuza asante kwa kunirekebisha,amani haisemi kwa maneno bali kwa vitendo.
Jiwe...
Katika vitu vinavyonisikitisha ni kusoma kejeli na matusi.
Kwani ukiandika kwa adabu utapungukiwa nini ndugu yangu?

Kwa nini unataka kuuvuruga uzi ambao tunaweza tukafundishana mengi?
Faiza wala si mzee mimi hanipati hata kidogo.
 
Nyerere alijenga Taifa moja lisilo na ubaguzi au migawanyiko ya kikabila, kikanda au kidini sasa ni zamu yenu nyie watoto na wajukuu wake kujenga uchumi imara katika Taifa. Badala ya kujikita kufanya hili, huyu mzee wako kucha kutwa analalamika kuhusu wazee wake wa Kariakoo kufunikwa umaarufu na Nyerere na udini.

Sasa tangu lini wauza kahawa wasio enda shule walio kalia kucheza bao wakawa na akili zaidi ya chuki na illusion za dini ya waarabu,
 
Kalamu,
Umerejea tena.


Kalamu,
Umerejea tena.

Vitu ninavyoweka hapa si lazima usome.

Viti ninavyoweka hapa nimewakusudia wale wanaofuatilia mjadala huu wasome na watujue sote wawili kwa uzuri kabisa:

PROF. ALI MAZRUI MWALIMU WANGU WA MASAFA MAREFU
Leo alfajir nimeikuta video ya Mwalimu wangu wa masafa marefu Prof. Ali Mazrui.
Imenikumbusha mbali.

Nina umri wa miaka 15/16 namsoma Ali Mazrui katika Sunday Nation kutoka Kenya.
Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."

Sikusita nikakinunua.
Nikimpenda Mazrui sana.

Katika umri ule nilikuwa namsoma Kwame Nkrumah, "Challenge of the Congo."
Namsoma Nkrumah anavyochambua matatizo na fitna ya kampuni kubwa ya Wabelgiji - Union Miniere kwa Patrice Lumumba.

Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.

Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.

Hela zangu zilikuwa zinakwenda kwanza kwenye comics, ice cream, records na mwisho tiketi za cinema kuangalia movies Jumamosi mchana na Jumapili asubuhi saa nne Empire Cinema.

Mara yangu kumuona Prof. Mazrui ilikuwa miaka ya mwishoni 1960s Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sikumbuki ilikuwa kwenye sherehe gani na Julius Nyerere alikuwapo.
Nilikuwa nimefuatana na kaka yangu na rafiki yangu pia Shaabani Muhunzi maarufu kwa jina la Mkorofi yeye alikuwa mwanafunzi pale chuoni na nikimuusudu sana kwa hilo.

Shaaban alinitia hamu ya mimi kufika alipofika yeye.

Chumbani kwangu nilikuwa na ubao na ubao huu alinipa Abdallah Tambaza.
Hivi sasa Abdallah ni mwandishi nguli wa historia ya Dar es Salaam.

Shaaban akija chumbani kwangu mwisho wa juma akitokea Chuo Kikuu anakuta kwenye ubao juu kabisa nimeandika, "English Literature."

Chini yake patafuatia ''passages'' za William Shakespeare tena nikiziandika kutoka kichwani.

Yeye atafuta ataandika, "Literature in English," kunisahihisha bwana mdogo wake.
Akiondoka nitafuta na nitaandika kama nilivyoandika mwanzo.
Juma linalofuatia itakuwa mchezo ni ule ule.

Atanisahihisha mwanafunzi mkaidi na mwalimu wangu akiondoka nitafuta.

Sasa nimekuwa kijana wa kati Mazrui akatengeneza ile ''documentary'' maarufu sana, "Africans: A Triple Heritage."

Hapa ndiyo alinimaliza kabisa.

Nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Said Baamumin tukikaa jirani yeye akifanyakazi UNDP.

Siku moja akaniambia angependa kunipeleka kwao Mtondia Mombasa nikamuone mama yake.

Said Bamumin akanifahamisha kuwa wao wamejenga na wana mashamba katika ardhi ya ukoo wa Mazrui.

Tulipofika Mtondia akanipeleka Takaungu kuona msikiti wa Mazrui ambao una umri kiasi ya miaka 400 na kisima cha asili kipo hapo na bado kinatoa maji.

Ardhi hii ya ukoo wa Mazrui ina historia ndefu katika historia ya Kenya na Mombasa.
Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilimpelekea nakala mwalimu wangu na niliandika ''Kwa Mwalimu wangu wa Masafa Marefu Prof. Ali Mazrui.''

Hivi ndivyo nilivyofahamiana na Prof. Mazrui na tukawa tunaandikiana.

Nakumbuka baada ya kupata kile kitabu Prof. aliniandikia kunishukuru na akaniambia, ''Nimefurahi jinsi ulivyowaandika Waswahili.''
Miaka ikaenda.

Harith Ghassany ndiye yeye aliyenijulisha tena kwa Prof. Mazrui kwa staili nyingine kabisa.

Nilikuwa nimealikwa mkutano Kampala na Prof. Mazrui alikuwa na yeye amealikwa pia.

Nilipomfahamisha Harith akanipa salamu nimfikishie Prof. Mazrui.
Harith alisomeshwa na Prof. Mazrui University of Michigan.

Sote tulikuwa tunakaa Hilton Hotel.

Nilikuwa nimesimama kwenye ''lobby'' ya hotel kwa mbali nikamuona Prof. Mazrui anakuja upande wangu.

Aliponikaribia nikapiga hatua nikamtolea salamu.

Akaniitikia na alipoona ile tabasamu yangu hakupita akaniuliza, ''Tunafahamiana?''
Nikamwambia pia nina salamu zake kutoka kwa Dr. Ghassany.

Nilikuwa nimemtajia Prof. Mazrui watu wake basi akaniambia tukae kitako tuzungumze.

Nilimstaajabisha sana nilipomwambia kuwa nimefika hadi kwao Takaungu na tulizungumza mengi na haukupita muda jamaa wengi wakaja pale tukakaa na Prof. Mazrui na kuzungumzanae.

Mazrui ni mtu asiye na makuu mwepesi wa kuingilika.
Alizungumza na sisi kama vile ni watu tunajuana miaka.

Siku anaondoka kurudi Marekani kanikuta pale ''reception,'' kaja ku-''check out,'' na mimi nina ''check out,'' tukaagana.

Nakumbuka ''typical Mazrui trend,'' alimwambia Manager on Duty pale Hilton, ''Tengenezeni hizi lift kwani zinagoma sana na ikija Mmarekani kanasa kwenye hizi lift zenu atawapelekeni mahakamani.''

Sijui kama wenzangu waliokuwa pale walielewa lakini kwangu mimi ujumbe ulikuwa umefika sawia.

Nikamkumbuka katika ''The Africans: A Triple Heritage,'' anaonekana anafungua bomba la maji katika hoteli moja ya Nyota Tano katika mji mmoja mkubwa Afrika bomba linakohoa halitoi maji.

Mimi kwa tahadhari ile Prof. akawa kanikumbusha hoteli moja Lagos ndiyo nimefika nataka kukoga, nimefungua bomba la maji kwanza bomba likakohoa kisha maji yakaanza kutoka lakini rangi yake ilikuwa ya udongo rangi ya kahawia.

128947353_851955588885154_8850432947121578944_n.jpg

129218847_851957128885000_2995618980404867812_n.jpg

Na Prof. Ali Mazrui
Nile Hilton Kampala 2003
129253231_851965788884134_828535121649428160_n.jpg

Unapoteza muda na nguvu zako kuandika maandiko marefu yaliyojaa majivuno kujisifu na kujiona wa maana kumbe ni takataka tu,mlengo wako unajulikana.
 
Uko sahihi mkuu! After then wazee wengi waliomsaidia kupigania uhuru hawakuwa wasomi! Lakini hata hivyo alijitahidi sana kumridhisha kila mtu lakini ukizingatia nchi ilikuwa changa na masikini asingeweza kumtosheleza kila mtu!

Sysafiri,
Tatizo hapa si ''kutosholeza'' au kiti kingine katika hayo uliyosema ya elimu nk.
TAA haikuwa inaendeshwa na watu ambao hawakuwa na elimu.

Itapendeza kwanza ukaijua historia ya TAA ndipo uandike.
Tatizo lililopo ni kuwa historia ya TANU iliyoandikwa si sawa ina mkosa mengi.

Hili ndilo lililonifanya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes kusahihisha.
 
Kuna conmen wanatoka hadi vyuo bora kabisa duniani kama Havard, kwa sasa wako hadi katika mabunge yote mawili ya Marekani.
Yoda,
Tupe historia za hawa watu bila shaka zitavutia.
Nimepita huko nimewaona na suti zao.

1679082979653.jpeg

Capitol Hill
Washigton DC​
 
Hivi na jamii nyingine kama Wachaga nao wakianza kudai "wazee wao" kama Thomas Marealle waenziwe sawa na Nyerere kupigania uhuru utakubali?
Yoda,
Mimi sijadai wazalendo waliopigania uhuru waenziwe kama anavyoenziwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hili haliwezekani.

Nilichofanya mimi katika kitabu cha Abdul Sykes nimeandika historia kama inavyotakiwa kuwa.

Ikiwa umesoma kitabu hicho utakuwa umekutana na mengi ambayo hukuwa unayajua.

Msome Chief Thomas Marealle hapo chini:

KUMBUKUMBU KIFO CHA MANGI MKUU THOMAS MAREALLE 14 FEBRUARY 2007: PARAMOUNT CHIEF THOMAS MAREALLE KATIKA NYARAKA ZA RAJABU IBRAHIM KIRAMA WA MACHAME NKUU

Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.

Nimekuja kukutana tena na Mangi Mkuu Thomas Marealle baada ya kiasi cha miaka 30 kupita katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha ya Mzee Rajabu wa Machame Nkuu.

Napenda kama kumbukumbu ya kifo cha Mangi Mkuu nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.

Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga, Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam na mtu aliyeueneza Uislam Uchaggani akianzia harakati zake kijijini kwake Machame Nkuu katika miaka ya 1930.

Harakati hizi zilileta uadui mkubwa kati yake na Chief Shangali.

Mwishoni wa miaka ya 1800 Wajerumani baada ya kuchoshwa na vita visivyokwisha baina ya Wachagga wenyewe kwa wenyewe waliamua kuwakamata takriban mangi wote isipokuwa Shangali na Marealle.

Jumla ya mangi 19 walinyongwa hadharani isipokuwa Chief Marealle na Chief Shangali.

Haya ndiyo madhila yaliyowakumba Wachagga chini ya utawala wa Wajerumani.
Watoto wa machifu hawa wawili hata hivyo walikuja kupata nguvu kubwa sana katika utawala wa Waingereza.

Katika utawala wa Waingereza na katika hali ya amani na utawala Wachagga waliunda chama - Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) (Umoja wa Raia wa Kilimanjaro).

Petro Njau akiwa kiongozi wa chama hiki alipewa jukumu la kusimamia maslahi ya Wachagga kama taifa.

Katika kanuni za KCCU kanuni hizi zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.

Petro Njau alikinadi chama hiki kuwa ni ‘’chama cha siasa cha kikabila.’’

Nilipokuwa nasoma Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama nilishangaa sana kusoma kuwa Wachagga kwa asili waliichukulia Kilimanjaro yote kuwa ni nchi.

Nyaraka za KCCU zimejaa maneno ya itikadi ya: ‘’nchi,’’ ‘’taifa,’’ ‘’raia,’’ ‘’uchaguzi,’’ ‘’kura,’’ na ‘’utawala.’’

Petro Njau Rajabu na Ibrahim Kirama walikuwa wanaunganishwa na kukubaliana katika jambo moja kubwa na muhimu sana katika utawala wa Wachagga nalo ni kuwa Mangi walikuwa na nguvu zilizopea wakati raia wao hawakuwa na sauti yoyote.

Kwa ajili hii basi wanastahili kuondolewa wote na awekwe kiongozi mmoja tu atakaetawala Kilimanjaro yote na Wachagga wote.

Petro Njau alikuwa mwandishi wa Mzee Rajabu na pia mwandishi wa Chief Thomas Marealle pale Kilimanjaro ilipokuwa katika siasa za uchaguzi kutafuta Mangi Mkuu atakaekuwa juu ya Mangi wote, yaani Paramount Chief.

Rajabu Kirama alisimama bega kwa bega na Petro Njau katika fikra hii.

Thomas Marealle na Abdiel Shangali ndiyo walikuwa wanagombea nafasi ya Mangi Mkuu na bahati mbaya sana kwa Abdiel Shangali ni kuwa alikuwa na uadui mkubwa na Rajabu Ibrahim Kirama.

Rajabu Kirama akasimama kumsaidia Chief Marealle awe kiongozi wa Wachagga wote.

Hivi ndivyo Thomas Marealle alivyokuja kuchaguliwa kuwa Paramount Chief, yaani Mangi Mkuu.

Picha: Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, Mangi Mkuu Thomas Marealle wa Marangu na Chief Abdiel Shangali wa Machame.

274069029_1119182355495808_4383308951877542266_n.jpg

273983192_1119182948829082_5959692333401352877_n.jpg

274050755_1119184155495628_7865162672895913103_n.jpg

Chief Abdiel Shangali​
 
Huko Zanzibar Historia ya Mapinduzi imeandikwa kumzunguka Karume ila hukomalii kuonyesha kuna watu wengi walihatarisha maisha yao kumuondoa Sultan ila kwa Nyerere aliyeweza kuzungumza na wazungu wakawahi kuondoka ndio umeng'ang'ana kumuonyesha alikuwa wa kawaida tu!
Yoda,
Nilikuwa Reseach Assistant wa Dr. Gharith Ghassany kwa miaka minane wakati anaandika kitabu cha mapinduzi ya Zanzibar, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Hili nadhani hulijui.
Nimeandika sana kuhusu historia ya Zanzibar na Mapinduzi.

Nimefanya vipindi vingi vya radio na TV.

KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU: KITABU KIONGOZI KATIKA VITABU VYA HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Nakumbuka mara ya kwanza nilipoonana na Dr. Harith Ghassany nyumbani kwake Muscat aliyenipeleka alikuwa Abdullah Amour ambae sasa ni marehemu na alikuja kuwa rafiki ndugu na alikuja hadi Tanga kunitembelea.

Ilikuwa mwaka wa 1999 ndipo nilipokutana na Dr. Harith Ghassany.

Mwezi wa Ramadhani ulinukuta Muscat Harith alinialika futari nyumbani kwake.

Harith alinifahamisha kuwa ana azma ya kuandika kitabu kuhusu Zanzibar na hapo ndipo nilipomfahamisha kisa nilichosikia Tanga kuwa kulikuwa na kambi ya Wamakonde Kipumbwi ambapo ndipo walipokuwa hawa Wamakonde wakipewa mafunzo kisha kuvushwa kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP uchaguzi wa wa 1961 na mwaka wa 1964 kushiriki katika mapinduzi.

Harith alinisikiliza kimya wala hakunisaili na akasema kuwa atakuja Tanga ambako mimi ndiko nilikokuwa naishi.

Alifika Tanga na nikaweka miadi na Mzee Mohamed Mkwawa.
Nilimshusha Harith nyumbani kwa Mzee Mkwawa sehemu za Kisosora kisha mimi nikaendelea na shughuli zangu nyingine.

Niliporudi mchana kumchukua kitu kilichonistaajabisha ni kuwa nilimkuta Harith kakalia mgongo, kachoka na kasawajika.

Sikusema neno.
Tulikuwa tumeandaliwa chakula cha mchana.

Nakumbuka tulipiga kipunga na samaki.
Kumaliza namwambia Harith twende zetu.

Jibu alilonipa lilinishangaza.

''Guy wewe nenda njoo nichukue jioni mimi na Mzee Mkwawa hatujamaliza mazungumzo yetu.''

(Mimi na Harith tunaitana, ''Guy,'' na hiki ni kisa naamini mtapenda kukisikia tulihadithiwa na Mzee Ahmed Rashad mkasa wake na rafiki yake Ahmed Abdullah Alkharui maarufu kwa jina la Bamanga.

''Guy,'' ndilo jina wakiitana.

Marafiki hawa mwaka wa 1952 walishitakiwa mahakamani kwa kosa la uchochezi).

Nikashangaa nikajiambia haya mazungumzo toka asubuhi hadi dhuhri yapata saa nne hayajesha na sasa wanaendele ahadi alasiri...

Nilipokuja kumchukua jioni ile alipoingia kwenye gari kitu cha kwanza nilichomuuliza ilikuwa, ''Guy imekuwaje mbona umechoka hivyo umenitisha sana leo.''

''Sikiliza Guy, ufunguo wa kitabu chetu anao Mzee Mkwawa mimi nimetembea maktaba zote kubwa sijakuta haya aliyonieleza Mzee Mkwawa.''

Kwa mara ya kwanza Harith anaelezwa na Mzee Mkwawa yaliyotokea Pemba ya yeye kushauriwa akimbie Pemba asije kuuliwa na Hizbu.

Mkwawa wakati huo kijana labda wa miaka 25 alikuwa mwanachama wa ASP na mmoja wa vijana wa kazi wa Abeid Amani Karume.

Alipofika Tanga akadakwa na Ali Mwinyi Tambwe na wenzake na kumuomba msaada wa yeye kurejea Zanzibar kwa kazi maalum ya ''kufa na kupona,'' kwa ajili ya uhuru wa Waafrika wa Zanzibar.

Mimi sasa nikawa nayasikia hayo mengine kwa mara ya kwanza kutoka kwa Harith.

Mzee Mkwawa kumbe hakunipa yote.
Nilishusha pumzi.

Sikushangaa kwa nini Harith nilimkuta kakalia mgongo wake na kachoka sana.

Hakika Mzee Mkwawa alikuwa kashika ufunguo wa kitabu chake Dr. Harith Ghassany.

Kilichobaki ilikuwa kumfikisha Dr. Harith Ghassany Kipumbwi kisha amkutanishe na Victor Mkello.

Ali Mwinyi Tambwe ana historia ya pekee katika historia ya Tanganyika na Zanzibar na leo hakuna anaeijua historia yake.

Kuna picha katika kitabu cha Abdul Sykes inamuonyesha Ali Mwinyi Tambwe amekaa pembeni kwa Kleist Sykes na Abdul Sykes yupo katika picha hiyo mtoto mdogo wa shule ya msingi.

Hii ni picha ya mwaka wa wa 1936 ya viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Mwaka 1953 huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwapo nyumbani kwa Hamza Mwapachu katika mazungumzo kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu walipojadili na kukubaliana kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 waunde TANU.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe ndiye aliyemtia Mohamed Mohamed Omar Mkwawa katika vyombo vya usalama na kumpa usimamizi wa kambi ya Kipumbwi.

Inasemekana Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mtu wa Special Branch toka ukoloni.

Hii ndiyo barabara Mzee Mkwawa aliyompitisha Dr. Harith Ghassany hadi kumfikisha Kipumbwi kisha akampeleka Nguvumali Tanga mjini nyumbani kwa Victor Mkello.

Watafiti wote wa historia ya mapinduzi hawakuwajua watu wa mfano wa Mzee Mkwawa kwa hiyo walipitwa na sehemu muhimu sana katika historia ya Zanzibar.

Kichekesho kikubwa ni kuwa na hata wale waliowajua Wapinduzi hawa wanajifanya kama vile watu hawa hawakupata kuwepo.

Wamejifanya pia hawajui kuwa Victor Mkello alikutana na Mzee Karume Zanzibar baada ya mapinduzi na Mzee Karume alimshukuru kwa kazi yake.

Mimi binafsi namshukuru sana Dr. Harith Ghassany kwa kunishirikisha katika utafiti wake na huu utafiti ndiyo ulionifunza hIstoria ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.




 
Wapelekee wanaozitaka, kwa nini uniletee mimi takataka nisizozithamini, huoni kuwa huo wenyewe nii uchizi unaokusumbua wewe?
Kalamu,
Nitakusaidia tena.
Tufunge mjadala.

Kaa kimya.
Hutonisikia.

1679109251001.jpeg

Chuo Kikuu Cha Azhar
Cairo 1991

 
Sasa tangu lini wauza kahawa wasio enda shule walio kalia kucheza bao wakawa na akili zaidi ya chuki na illusion za dini ya waarabu,
Jiwe...
Niruhusu nikueleze historia ya Msham Awadh na wenzake ''wauza kahawa wasioenda shule...'' katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tangnayika.

''Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake.

Msham Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.

Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba.

Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni Tanganyika.

Hawa ndiyo wazalendo ambao historia yao ilifutwa.

Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya kimagharibi.

Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.

Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.

Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda kutoka Mtwara kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.

Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe wananchi kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.

Wakati haya yanafanyika wamishionari wa Peramiho kulikuwa na mipango ya kuizuia TANU isiingie Jimbo la Kusini.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998).

274395611_1121771918570185_8123025436190972313_n.jpg

Nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji Makonde Street Lind aliyoitoa kwa TANU kama ofisi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.​
 
Habari Mh. Mohamed Said ,Tafadhali jibu hoja,Ni Kipi kilichomfanya J.K Nyerere kuwazidi Ujanja wazee wa DONTA?
Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...
 
Mpe...
Umependezewa na historia ya babu yangu?
Mpe,
tuendelee na historia ya babu yangu Salum Abdallah:

''Mwaka uliofuata, African Association Tabora ilikuwa imejiimarisha vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kushiriki katika mgomo wa mwaka 1947 ambao ulianza katika bandari ya Dar es Salaam.

Kuwako kwa Waislam wengi sana katika ajira ya bandarini kwa kiasi kikubwa kulichangia kuwasha moto wa mshikamano uliolipua mgomo.

Wakati wa mgomo Tabora, Mwalimu Pinda, aliyekuwa miongoni mwa walimu wa St. Mary's School na mwanachama wa African Association, alichukua jukumu la kuwa mtu wa kati baina ya wawakilishi wa wafanyakazi waliogoma na African Association.

Siku ya mgomo wafanyakazi wengi wao kutoka Loco Shed (karakana ya magari moshi) wakiongozwa na Salum Abdallalh, walikusanyika katika viwanja vya Tabora Town School chini ya miembe.

Tabora ni maarufu kwa wingi wa miembe.

Kuanzia siku hiyo viwanja hivyo vikawa ndiyo mahali pa mikutano yote ya African Association.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Julius Nyerere alikuwapo Tabora lakini hakujihusisha na hizi harakati za tabaka la wafanyakazi zilizokuwa zikiibuka.''

1679111638969.jpeg

Kulia Christopher Kassanga Tumbo (Secretary) Salum Abdallah (Chairman) wakati huu ni tayari washaunda Tanganyika Railways African Union (TRAU)​
 
Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...
Hei...
Tunaweza tukafanya mjadala wa maana usiokuwa na mihemko.
Litengeneze swali lako liwe linaloweza kueleweka.

In Shaa Allah nitakuja kukupa majibu.

Muhimu ni kuwa kwanza uwe na subira ya kusoma rejea nitazokuwekea hapa
(nyingine ni za Kiingereza).

Hapa nazungumzia kusoma kurasa kama 500 hivi.

Uzoefu umenionyesha kuwa wengi wetu hapa hatuna kwanza elimu ya haya tunayotamani kujadili na pili tunapenda kuja hapa kushambuliana na kumshambulia Mohamed Said.

Napenda kuhitimisha kwa kukueleza kuwa ilibidi ipatikane ridhaa ya Mwalimu Nyerere kuweza kujibu mengi katika uliyochanganya katika swali lako hapo juu.

Mwalimu alitoa ridhaa yake na kimeandikwa kitabu ''Nyerere Biography,'' (2020).
Soma kitabu hiki kitakusaidia kupata majibu.

Lakini kabla ya kusoma kitabu hiki itabidi kwanza usome In Shaa Allah hizo rejea nitakazo kuwekea.
 
Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...
Deliberate.
 
Hei...
Tunaweza tukafanya mjadala wa maana usiokuwa na mihemko.
Litengeneze swali lako liwe linaloweza kueleweka.

In Shaa Allah nitakuja kukupa majibu.

Muhimu ni kuwa kwanza uwe na subira ya kusoma rejea nitazokuwekea hapa
(nyingine ni za Kiingereza).

Hapa nazungumzia kusoma kurasa kama 500 hivi.

Uzoefu umenionyesha kuwa wengi wetu hapa hatuna kwanza elimu ya haya tunayotamani kujadili na pili tunapenda kuja hapa kushambuliana na kumshambulia Mohamed Said.

Napenda kuhitimisha kwa kukueleza kuwa ilibidi ipatikane ridhaa ya Mwalimu Nyerere kuweza kujibu mengi katika uliyochanganya katika swali lako hapo juu.

Mwalimu alitoa ridhaa yake na kimeandikwa kitabu ''Nyerere Biography,'' (2020).
Soma kitabu hiki kitakusaidia kupata majibu.

Lakini kabla ya kusoma kitabu hiki itabidi kwanza usome In Shaa Allah hizo rejea nitakazo kuwekea.
Kwanza naomba msamaha katika nilichoandika sababu nimeandika sikusoma kila kitu lakini nikawa napitia maandiko yako humu na kuelewa unachoaminisha na mimi ni mtu napenda sana kusoma history na umri wangu sio mkubwa kujuwa kila kitu ila ningependa kuongea kidogo katika historia na sio ya Tanzania tu nyingi ziliandikwa kwa malengo fulani ya kisiasa lakini ukweli haukundikwa hata katika suala la kupigania uhuru mimi siamini na sio kwa Tanzania tu ni kwa yaliyokuwa makoloni ya waingereza yote kupewa uhuru ilikuwa arranged sababu England walikuwa hawana uwezo tena ki mali kuendelea kutawala ilikuwa mipango kuziachia nchi hizi zote naamini utatuma darasa kwenye hili uhuru ulipiganiwa au tulipewa? Nyerere alikuwa mwana siasa na siasa ni mchezo na akaucheza ila wazee wengi hawakuwa wanasiasa labda walidhani kama kushabikia Yanga na Simba ndio maana wakaishia njiani. Kitu kimoja na uhakika 100% historia imeandikwa kunufaisha kikundi fulani sio ukweli maana ukweli siku zote unaleta shida ndio maana sijawahi kuamini Iddi Amin alikuwa anakula nyama ya watoto wake lakini wakati ule niliamini sababu tulilishwa propaganda na history yetu kama propaganda. Naomba ushauri ni vitabu gani naweza kusoma haya unayoandika na wapi vinapatika sababu napenda kusoma upande wa pili. sababu sina upande ila nataka kujuwa ukweli kwa faida yangu tu mwenyewe kama hii issue ya Bibi Titi kusimama kupinga ni kitabu gani naweza kusoma hiyo history.
 
Unapoteza muda na nguvu zako kuandika maandiko marefu yaliyojaa majivuno kujisifu na kujiona wa maana kumbe ni takataka tu,mlengo wako unajulikana.
Jiwe...
Hapana sipotezi muda kuandika ndiyo kazi yangu.
Mtu hapotezi mudu katika kufanya kazi.

Nimechukua moda kujibu kuhusu, ''majivuno,'' ''kujisifu,'' na ''kujiona wa maana.''

Nimewapa kazi hii wahariri wanaopitia maandishi yangu niliyoandika zaidi ya miaka 30 hadi leo.

Nimewaomba wanipe tathmini yao kama kuna vitu hivyo katika maandishi yangu.
Nakueleza waliyonieleza huenda yakatusaidia sote kujitathmini.

Hawa wahariri wanasema kuwa hata wao wameshangazwa na mimi.
Wanasema waliona kitu katika maandishi yangu ndiyo sababu wakaomba kazi kwangu.

Lakini wameshangazwa na waliyoyakuta katika kazi hiyo.

Hawakujua ni kwa kiwango gani mimi nimeshuhubiana na duru za kisomi katika vyuo vikuu.

Wanasema hakuna mahali ambapo nimefikia ''peak'' ya kujieleza kama JF.
Wamesoma mijadala mingi (randomly) kwani si rahisi kusoma mmoja baada ya mwingine.

Walichogundua ni kuwa wengi wa wasomaji wanaokuja kutaka kujadili nami hawajui kina cha maji wanachoingia kuogelea.

Kina hiki kinawadhihirikia tayari wameshatumbukia na inakuwa tabu kutoka.

Wanasema wanashindwa kutoka kwa sababu ya ''ego'' hawataki kuonekana kuwa wameshindwa.

Hitimisho lao wanasema katika mijadala hii ndipo inapowadhihirikia kuwa wewe si kiwango chao cha wao kuweza kusimama na wewe na kushinda.

Haya ndiyo waliyoyaona.
Wanasema hakuna ''majivuno,'' ''majisifu'' nk. katika uandishi wangu.

NB:
Hawa wahariri tunao humu ndani wanatusoma kila siku.
 
Wewe mzee story zako zinafurahisa sana wakati mwingine. Hivi unafikiri muuza make-up kwenye kwenye kikapu(yani kama leo hii hawa hawa vijana wetu wanozunguka kupaka wanawake rangi kucha na kuosha miguu yao) angeweza kusimama kupambana na Waingereza awanyang'anye nchi na awe katika uwanja sawa na Nyerere ambaye alikuwa Mwalimu(taaluma iliyokuwa ikiheshimika sana kipindi hicho) msomi wa degree mbili kutoka vyuo vikubwa duniani!
Jiwe...
Niruhusu nikueleze historia ya Msham Awadh na wenzake ''wauza kahawa wasioenda shule...'' katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tangnayika.

''Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake.

Msham Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.

Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba.

Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni Tanganyika.

Hawa ndiyo wazalendo ambao historia yao ilifutwa.

Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya kimagharibi.

Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.

Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.

Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda kutoka Mtwara kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.

Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe wananchi kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.

Wakati haya yanafanyika wamishionari wa Peramiho kulikuwa na mipango ya kuizuia TANU isiingie Jimbo la Kusini.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998).

274395611_1121771918570185_8123025436190972313_n.jpg

Nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji Makonde Street Lind aliyoitoa kwa TANU kama ofisi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.​
 
Back
Top Bottom