Nidhamu? Juu ya kitu gani 'conmanship'?Huna nidhamu
Utakuwa huelewi maana ya hilo neno 'nidhamu'.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nidhamu? Juu ya kitu gani 'conmanship'?Huna nidhamu
Duh!Umeandika uongo umestukiwa na sasa unajishaua.
Mwandiko wako ni ule ule(arrogantly) haufichiki hata ukija na id nyingine, tunaukumbuka miaka ile mkaungana kikundi mkijidai mtakuja na kitabu, mkadondokea pua mpaka leo hii.
Nikujuwe wewe nani zaidi ya kuja hapa na uongo ukastukiwa.Duh!
Na wewe umeibuka toka pango gani linalokuhifadhi kusikofika mwanga!
Humjui 'Kalamu' wewe?
Kalamu,Yatanisaidia kitu gani haya mimi!
Wewe achana na mambo ya TANU. Unachoandika chochote kinaishia kwa Sykes na uislamu. Wewe ni mtu hatari.Mama...
Naamini kabisa unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Soma hapo chini kisha rejea tuendelee na mjadala.
Nimekuta historia hii katika Nyaraka za Sykes:
WANYASA WANAULIZA DENIS PHOMBEAH NI NANI KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA ?
Raia Mwema la 14 - 20 Agosti limechapa makala ambayo kwanza ilikuwapo hapa Majlis, ''Tulikotoka Kufika SADC Kisa Cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda.''
Nia yangu ya kuweka hapa makala ile ilikuwa baada ya kupigiwa simu na kuombwa nishiriki katika kipindi cha Channel Ten Zahir Hotel ambako wajumbe wa SADC wangefika pale na kuniuliza maswali kuhusu historia ya mgahawa huu na wapigania uhuru wa nchi za Kusini.
Kwenye mlango wa kuingia mgahawa huu kuna kibao kinachoeleza kuwa hapo palikuwa sehemu wakikutana wapigania uhuru wa nchi Kusini ya Afrika.
Kipindi hiki nilifahamishwa kitarushwa mubashara.
Ukweli nilimkatalia huyo aliyenipigia simu na sababu kubwa ni kuwa mwaliko wenyewe umenifikia mchana milango ya saa saba hivi na kipindi kinakwenda hewani saa kumi jioni kwa hiyo hapakuwa na muda wa matayarisho.
Mambo kama haya yanahitaji maandalizi hasa ikiwa kipindi ni mubashara kwa kuchukua tahadhari kusema maneno siyo.
Nikamfahamisha hilo ndugu yangu aliyenifikishia mwaliko nikamwambia hawa ni wageni wa serikali wasije wakaniuliza maswali ambayo majibu yake yanapishana na historia rasmi inayofahamika.
Ikawa nimekataa kushiriki katika kipindi kile.
Lakini ikanijia fikra kuwa ninao bado mchango wa kuchangia katika historia ya Tanganyika na SADC.
Ndiyo nikaamua kuweka hapa safari ya mwaka wa 1953 ya Ally Sykes na Denis Phombeah kwenda Lusaka Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa kutoka nchi Kusini ya Sahara ulioitishwa na Kenneth Kaunda akiwa Rais wa ANC ya Northern Rhodesia.
Ndugu zetu Wanyasa baada ya kusoma gazeti la Raia Mwema na kukuta Mnyasa anaiwakilisha Tanganyiaka katika mkutano ule wamepiga simu nyingi Raia Mwema kutaka kujua mchango wao katika uhuru wa Tanganyika.
Kisa hiki hiki kilichosomwa na wengi hapa Majlis kama ningekieleza mbele ya camera za televisheni tena mubashara athari yake kwa watazamaji ingekuwa nyingine kabisa.
Lingeweza kuja swali kwangu, ''Ally Sykes na Denis Phombeah ni nani na iweje hawa wawakilishe Tanganyika kwani Julius Nyerere alikuwa wapi?''
Unajibu vipi mtu maswali kama haya?
Mhariri wa Raia Mwema kakwepa kuliunganisha jina la Ally Sykes, Denis Phombeah na jina la Kenneth Kaunda.
Si bure kwa yeye kuamua kufanya hivi.
Anazo sababu zake.
Picha: Ally Sykes na Denis Phombeah wakiwa Chileka Airport, Blantyre Nyasaland wakiwa njiani kurudi Dar es Salaam.
![]()
![]()
Wazee wa Kariakoo hawakuwa tofauti na wale wazee wa kichaga waliotaka uhuru wa uchagani tu. Hao nia yao ilikuwa sio kuikomboa nchi nzima.. Mwalimu Nyerere alifanya vizuri kuwafutilia mbali kwasababu nia yao ilikuwa ovu ya kujinufaisha na kuueneza uislamu. Wewe mwenyewe ulishawahi sema ulishiriki kwenye kuwavunia wafanyabiashara mabucha yao ya kitimoto. Mngesikilizwa si mngefanya mambo mengi zaidi ya kipuuzi kwenye nchi huru?Mama...
Mimi nitakuwa mjinga sana kama nitapuuza uwezo wa Mwalimu Nyerere.
Kwanza fikiria uwezo watu hawa ambao ndiyo walikuwa ndani ya TAA Political Subcommittee mwaka wa 1950: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Mshauri wa hii kamati akiwa Earle Seaton.
Sijui kama wewe unajua uwezo waliokuwanao watu hawa.
Hawa ndiyo walikuwa wanapanga mipango ya kuikomboa Tanganyika na hawa ndiyo waliomtia Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA.
Kwa kipande hiki cha historia kinaonyesha uwezo mkubwa wa Mwalimu Nyerere.
Swali langu kwako ni hili.
Wewe ulikuwa unawajua hawa niliokutajia kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika?
Mimi nimenyanyua kalamu kusahihisha historia iliyokuwa inamtaja Nyerere peke yake na kueleza historia ya TANU kama ilivyotakiwa kuandikwa.
Kubwa na hili ndilo wengi hapa linawaumiza ni kutaja mchango wa Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika kupigania uhuru.
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi za TANU misikitini na aliwaongoza Waislam kumuunga mkono Julius Nyerere.
Je, wewe hupendi haya yakaelezwa katika historia ya uhuru?
Hakuna mahali unaweza kusema hawa wazalendo waliishia hapa katika kudai uhuru na Nyerere akaanzia hapa.
Hawa na wazalendo wengine walikuwapo na Nyerere toka walipompokea 1952 hadi uhuru unapatikana 1961.
Nyerere angekuwa mbali sana angeunda TANU nje ya watu hawa na labda angeunda chama chake.
Lakini Nyerere kamkuta Abdul na wenzake katika harakati za uhuru katika African Association (1929) na Al Jamiatul Islamiyya (1933) iliyoundwa na baba yake.
Iweje historia hii ifutwe?
Unaweza vipi kuwafuta wazalendo hawa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ukambakisha Nyerere peke yake?
Sikuandika kitabu kumdogosha Nyerere.
Nimeandika kitabu kusahihisha historia iliyojaa makosa mengi sana.
Hii ndiyo sababu Prof. Haroub Othman alimshauri Mwalimu akubali iandikwe historia ya maisha yake ipatikane nafasi ya kufanya marekebisho ya historia iliyokuwapo ambayo kitabu cha Abdul Sykes iliibomoa.
Unasema ningekuwa na uwezo?
Uwezo ninao na umetambulika.
Kleist Sykes ametiwa katika Dictionary of African Biography (DAB) Oxford University Press, New York 2011.
Kitabu nilichoandika "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)," Minerva Press London 1998 kimechapwa matoleo manne tunakwenda la tano na kipo kwa Kiswahili pia Phoenix Publishers, Nairobi 2002.
Niko hapa JF sasa mwaka wa 11 nafundisha historia hii.
Kimeandikwa kitabu cha Nyerere (2020) nimeshirikishwa na nimenukuliwa sana ndani ya kitabu hicho.
View attachment 2554651View attachment 2554657Mahojiano na TBC kuhusu Nyerere Biography
View attachment 2554660
Mama...Wewe achana na mambo ya TANU. Unachoandika chochote kinaishia kwa Sykes na uislamu. Wewe ni mtu hatari.
Mama...Wazee wa Kariakoo hawakuwa tofauti na wale wazee wa kichaga waliotaka uhuru wa uchagani tu. Hao nia yao ilikuwa sio kuikomboa nchi nzima.. Mwalimu Nyerere alifanya vizuri kuwafutilia mbali kwasababu nia yao ilikuwa ovu ya kujinufaisha na kuueneza uislamu. Wewe mwenyewe ulishawahi sema ulishiriki kwenye kuwavunia wafanyabiashara mabucha yao ya kitimoto. Mngesikilizwa si mngefanya mambo mengi zaidi ya kipuuzi kwenye nchi huru?
Kalamu,Mkuu 'Baba-mwajuma', mimi siyo mwanasiasa, na wala sitegemei hata siku moja nitafute sifa maalum za upendeleo toka kwa yeyote. Mimi nawasilisha mawazo yangu, uyapende usiyapende hiyo ni juu yako mwenyewe kufanya uamzi.
Maoni yangu kuhusu haya ya mzee ni hayo hayo hayabadiliki. Huyu ni 'con' mkubwa aliyechota akili za watu kama wewe kwa mtindo wa uwasilishaji wake wa utapeli mkubwa.
Wewe kama Great thinker unayeheshimika humu ulitakiwa uje na Hoja za kuonesha Huyu mzee ni Con, na sio kutoa tuhuma za maneno matupu na kashfaMkuu 'Baba-mwajuma', mimi siyo mwanasiasa, na wala sitegemei hata siku moja nitafute sifa maalum za upendeleo toka kwa yeyote. Mimi nawasilisha mawazo yangu, uyapende usiyapende hiyo ni juu yako mwenyewe kufanya uamzi.
Maoni yangu kuhusu haya ya mzee ni hayo hayo hayabadiliki. Huyu ni 'con' mkubwa aliyechota akili za watu kama wewe kwa mtindo wa uwasilishaji wake wa utapeli mkubwa.
Baba...Wewe kama Great thinker unayeheshimika humu ulitakiwa uje na Hoja za kuonesha Huyu mzee ni Con, na sio kutoa tuhuma za maneno matupu na kashfa
Mambo haya ya kashfa waachie kina Jiwe na kundi Lao.
Samahani mkuu, naomba kujua miongoni mwa wanaharakati wa ukombozi wa Tanzania yupi ni mzazi au una damu nae ya kindugu? Samahani kama mtakuwa nimekukoseaKalamu,
Nakuelewa vizuri.
Hutokea wakati mwingine mtego ukamnasa chui.
Mwindaji mjinga ndiye atausogelea mtego wake.
Ulidhani una uwezo wa kupambana na mimi.
View attachment 2554163
Columbia University, New York.
Ngome,Samahani mkuu, naomba kujua miongoni mwa wanaharakati wa ukombozi wa Tanzania yupi ni mzazi au una damu nae ya kindugu? Samahani kama mtakuwa nimekukosea
Ikawaje sasa baada ya hapo maana umeishia njiani hii simulizi tungeomba uendelee kusimuliaNgome,
Hujanikosea ndugu yangu.
Inapendeza watu tukifahamiana:
BABU YANGU SALUM ABDALLAH POPO
Ikiwa umemsoma babu yangu Salum Abdalah na kigoma chake cha daku utakuwa umeona kuwa alipata kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964.
Hayo hapo chini yatakusaidiwa kumwelewa mtu huyu.
Ilikuwa mwaka wa 1965 babu yangu Salum Abdallah katoka jela ya Uyui Tabora alikowekwa kizuzini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964 hana kazi yuko nyumbani.
Mwaka wa 1953 akiwa na taarifa kutoka Dar es Salaam kuwa kuna harakati za kuunda chama cha siasa yeye na wenzake Tabora wakawa wanafanya mikutano ya siri kila Jumapili Town School ambako Abubakar Mwilima alikuwa mwalimu na yeye Mwalimu Abuu kama walivyopenda kumwita ndiye aliyekuwa akiwafungulia darasa moja kukutana na kupeana habari kutoka New Street Dar es Salaam, Makao Makuu ya TAA.
Hii ailikuwa baada ya kumtuma Katibu wa TAA Western Province, Germano Pacha kwenda Makao Makuu ya TAA kuwapa taarifa kuwa Tabora inataka kuunda chama cha siasa.
Germano Pacha alipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes na akamwambia arudishe salamu Tabora kuwa wafanye subira.
Tufupishe kisa kwani kuna mengi.
TANU ikaundwa mwaka wa 1954 babu yangu akiwa mmoja wa wanachama wa mwanzo.
Mwaka wa 1955 babu na Kassanga tumbo wakaunda Tanganyika Railway African Union (TRAU) babu akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary.
Babu yangu Salum Abdallah ana historia ya uzalendo ya kusisimua ambayo hutochoka kuisikiliza kila inapohadithiwa kwa kuwa mkasa una kuwa ndani ya mkasa mwingine visa vikiunganishwa kama ushanga katika uzi.
Mwaka wa 1965 baba akanifungia safari niende Tabora kumwangalia babu baada ya kutoka kifungoni.
Babu yangu jina lake alililopewa na baba yake Abdallah Mwekapopo (naweza kwenda vizazi saba hadi kwa waliokuwa Belgian Congo) ni Rashid lakini katika ujana wake akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1930 alimpiga Mzungu akafungwa na alipotoka jela akabadili jina lake akawa Salum Abdallah.
Kisa gani akampiga Mzungu?
Huyu Mzungu alikuwa mbaguzi, mnyanyasaji Waafrika kwa hiyo babu siku moja akaamua kumshughulikia.
Hili lilikuwa kosa kubwa sana wakati wa ukoloni.
Hukaa nikafikiri yule Mzungu alikuwa katika hali gani baada ya kuingia katika mikono ya babu kwani alikuwa kapanda juu futi sita ana kifua kipana ile mitambo, yaami maumbo makubwa ya Kimanyema.
Kwa ajili ya umbo hili akiwa kijana Waingereza walimfunza kazi ya kufua chuma, yaani ‘’foundry,’’ kazi ngumu katika moto na joto kali.
Hii ‘’foundry ’’ ilikuwa ndani ya karakana ya Tanganyika Railways.
Humo ndani ya karakana wanaume wako vifua wazi na nyundo nzito ni kelele za chuma kikigonga chuma cheche za moto zikiruka na miaka ile hakuna vifaa mfanyakazi atavaa kuzuia kelele.
Hii karakana ndiyo ilikuwa ikachonga spea za treni.
Wenyewe kwa wenyewe ndani ya karakana wakizungumza kwa sauti za juu.
Labda ndiyo sababu babu hata akizunngumza hata katika mazungumzo ya kawaida sauti yake siku zote ilikuwa juu.
Hii karakana ilikuwa ndani ya eneo la Tanganyika Railway lakini jirani na Arab Street hivi sasa Mtaa wa Nkrumah na ndiko lilipokuwa lango kuu la wafanyazi wa Tanganyika Railways wakiingilia na kutokea katika miaka ile ya 1930.
Babu akiishi Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes).
Nyuma aliyokuwa akiishi ilikuwa inatazamana na nyuma ya Kleist Sykes ambae yeye alikuwa Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu) Tanganyika Railways.
Nafasi kubwa sana wakati ule kwani hio kazi wakifanya Wahindi.
Lakini babu yangu juu ya ubabe wake na haya yote alikuwa mtu karimu sana mimi nimeshuhudia kwa macho yangu na labda huu ukarimu alimrithisha baba yangu kwani mara nyingi nikipisha wageni chumbani kwangu nami kwenda kulala ‘’sitting room,’’hadi waondoke.
Hii Karakana ya Railway ikahamishwa Dar es Salaam mwaka wa 1947 kupelekwa Tabora na babu yangu akahamanayo kwenda huko.
Hakurudi tena Dar es Salaam.
Lakini mwaka huo huo alipofika Tabora akaongoza mgomo wa Railway ulioenea nchi nzima na akafanya hivyo mwaka wa 1947, 1949 na tena mwaka wa 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka.
Huu mgomo wa mwaka wa 1960 ulidumu kwa siku 82 na kuweka rekodi kushida mgomo wa Kenya ulioongozwa na Makhan Singh uliodumu kwa siku 62.
Baada ya mgomo huu wa mwaka wa 1960 Nyerere ilimhidhihirikia kuwa mtu huyu atakuja kumpa shida katika Tanganyika huru akawa sasa anamtazama kwa macho mawili.
View attachment 2555616
Salum Abdallah Popo
Hii nimeipenda sana inafikirisha sana kumbe dunia Ina watu wenye akili nyingi hiviKalamu,
"Con" anahadhiri vyuo vikuu anatiwa kwenye miradi ya Harvard na Oxford University Press ya kuandika vitabu vya historia.
Itabidi nitoe darsa kwa faida ya wasomaji:
COUNT VICTOR LUSTIG JIZI BINGWA
Dunia haijapata kushuhudia mwizi kumshinda Count Victor Lustig.
Nimesoma kitabu chake miaka 50 iliyopita lakini hadi leo jina lake sijalisahau wala kitabu kilichaoandikwa kuhusu yeye, ''The Man Who Sold The Eiffel Tower.''
Hili jizi liliuza Eiffel Tower si mara moja bali mara mbili.
Kila nikifika Paris lazima nikautazame huu mnara marufu duniani ambao ndiyo umekuwa alama ya Paris na kununua kijimnara kidogo kupamba nyumbani kwangu.
Lazima mtu utashangaa vipi jizi hili liliweza kuuza mnara ule si mara moja bali mbili na kuchukua fedha?
Nini ilikuwa siri yake?
Siri yake ilikuwa akili yake.
Hata wizi unahitaji matumizi ya akili na mipango mizuri ya kuiba.
Ukiacha huu wizi wa kuuza huu mnara wa Paris, Count Victor Lustig kawaibia watu wenye akili na nguvu duniani kama Fidel Castro wa Cuba na Papa Doc wa Haiti.
Ingawa Castro hakuwa mtu wa kumfanyia maskhara na ukapona jinsi alivyokuwa na watu ambao kama atamnyooshea mtu kidole watu wake wa usalama wanaweza kukusaka hadi wakakutia mkononi uko hai au maiti lakini hakumpata Count Victor Lustig baada ya kumuingiza mjini.
Count Victor Lustig aliingia Havana Cuba kwa ndege binafsi akitokea Florida na alikuwa na miadi na Castro.
Hakuwa na maneno mengi alimuomba avute pazia za ofisi yake pawe kiza akaweka ''projector'' na ''screen'' akamuonyesha filamu anayotaka kutengeneza ya Castro yuko Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.
Filamu ilikuwa fupi ya kiasi cha dakika kumi hivi.
Akamwambia Castro kuwa yeye ni mtengenezaji filamu na amekusudia kutengeneza filamu ya maisha yake akiwa Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.
Castro alikipenda kile alichokiona na mikataba ikawekwa saini.
Count Victor Lustig akaondoka Havana na mkoba umejaa dola mpya za mia, mia zilizofungwa vyema.
Count Victor Lustig hakuonekana tena Havana.
Castro na wasaidizi wakajua kuwa wameliwa.
Papa Doc wa Haiti aliyekuwa anatawala watu wake kwa uchawi na vitisho vya Ton Ton Macoute.
Papa Doc alimuuzia magari ya kifahari aina ya Cadillac lakini yote yalikuwa yameibiwa Marekani akayavusha kwa njia za panya hadi Haiti.
Papa Doc alipotambua kuwa yale magari yote yalikuwa yameibiwa Count Victor alikuwa kesharejea Marekani siku nyingi.
Mazombie yaani wale Ton Ton Macoute wala uchawi wake uliokuwa unaogopwa na wananchi wake haukuweza kumdhuru Count Victor Lustig.
Maofisa wa serikali yake walishangaa vipi ule uchawi wake na ''vodoo'' na Ton Ton Macoute wake hawakuweza kufua dafu mbele ya akili ya Count Victor Lustig.
Wizi wowote ule ili ufanikiwe unahitaji mipango na matumizi ya akili.
Bila matumizi ya akili na mipango mwizi atakuwa anakamatwa kila siku.
![]()
Eiffel Tower hiyo nyuma yangu
EEeeenHeeee!Nikujywe wewe bani zaidi ya kuja hapa na uongo ukastukiwa.
Ubamtisha Muislam? Umebuugi.
Muislam hamuogopi isipokuwa Allah pekee. Kumbuka hilo.
Kalamu,
Waingereza wanasema, "Seeing is believing."
Hapa unapoweka kitu umekiweka kwa dunia nzima kukiona au kukisoma.
Hii ndiyo faida yake.
Nimemweka Yvonne Chakacha kwa makusudi ili wanaofatilia mjadala huu na kusoma mimi nikibasibishwa na taka wakupime kwa maneno yako.
Hii mosi.
Pili ni kutaka kuhangaisha akili za wasomaji - Mohamed Said na Yvonne Chakacha wapi na wapi?
Wapi wamekutana?
Hapo wanazungumza nini?
Mimi huwa sijibu tusi kwa tusi:
View attachment 2555464
Hizi ni takataka tu kwangu.
Takataka tu hizi.Kalamu,
"Con" anahadhiri vyuo vikuu anatiwa kwenye miradi ya Harvard na Oxford University Press ya kuandika vitabu vya historia.
Itabidi nitoe darsa kwa faida ya wasomaji:
COUNT VICTOR LUSTIG JIZI BINGWA
Dunia haijapata kushuhudia mwizi kumshinda Count Victor Lustig.
Nimesoma kitabu chake miaka 50 iliyopita lakini hadi leo jina lake sijalisahau wala kitabu kilichaoandikwa kuhusu yeye, ''The Man Who Sold The Eiffel Tower.''
Hili jizi liliuza Eiffel Tower si mara moja bali mara mbili.
Kila nikifika Paris lazima nikautazame huu mnara marufu duniani ambao ndiyo umekuwa alama ya Paris na kununua kijimnara kidogo kupamba nyumbani kwangu.
Lazima mtu utashangaa vipi jizi hili liliweza kuuza mnara ule si mara moja bali mbili na kuchukua fedha?
Nini ilikuwa siri yake?
Siri yake ilikuwa akili yake.
Hata wizi unahitaji matumizi ya akili na mipango mizuri ya kuiba.
Ukiacha huu wizi wa kuuza huu mnara wa Paris, Count Victor Lustig kawaibia watu wenye akili na nguvu duniani kama Fidel Castro wa Cuba na Papa Doc wa Haiti.
Ingawa Castro hakuwa mtu wa kumfanyia maskhara na ukapona jinsi alivyokuwa na watu ambao kama atamnyooshea mtu kidole watu wake wa usalama wanaweza kukusaka hadi wakakutia mkononi uko hai au maiti lakini hakumpata Count Victor Lustig baada ya kumuingiza mjini.
Count Victor Lustig aliingia Havana Cuba kwa ndege binafsi akitokea Florida na alikuwa na miadi na Castro.
Hakuwa na maneno mengi alimuomba avute pazia za ofisi yake pawe kiza akaweka ''projector'' na ''screen'' akamuonyesha filamu anayotaka kutengeneza ya Castro yuko Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.
Filamu ilikuwa fupi ya kiasi cha dakika kumi hivi.
Akamwambia Castro kuwa yeye ni mtengenezaji filamu na amekusudia kutengeneza filamu ya maisha yake akiwa Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.
Castro alikipenda kile alichokiona na mikataba ikawekwa saini.
Count Victor Lustig akaondoka Havana na mkoba umejaa dola mpya za mia, mia zilizofungwa vyema.
Count Victor Lustig hakuonekana tena Havana.
Castro na wasaidizi wakajua kuwa wameliwa.
Papa Doc wa Haiti aliyekuwa anatawala watu wake kwa uchawi na vitisho vya Ton Ton Macoute.
Papa Doc alimuuzia magari ya kifahari aina ya Cadillac lakini yote yalikuwa yameibiwa Marekani akayavusha kwa njia za panya hadi Haiti.
Papa Doc alipotambua kuwa yale magari yote yalikuwa yameibiwa Count Victor alikuwa kesharejea Marekani siku nyingi.
Mazombie yaani wale Ton Ton Macoute wala uchawi wake uliokuwa unaogopwa na wananchi wake haukuweza kumdhuru Count Victor Lustig.
Maofisa wa serikali yake walishangaa vipi ule uchawi wake na ''vodoo'' na Ton Ton Macoute wake hawakuweza kufua dafu mbele ya akili ya Count Victor Lustig.
Wizi wowote ule ili ufanikiwe unahitaji mipango na matumizi ya akili.
Bila matumizi ya akili na mipango mwizi atakuwa anakamatwa kila siku.
![]()
Eiffel Tower hiyo nyuma yangu
Mkuu, nilishaeleza msimamo wangu siku nyingi kuhusu haya ya huyu mzee. Hii siyo mara ya kwanza; na hata katika mada hii hii, bandiko langu la kwanza kabisa nimeeleza ninaposimamia.Wewe kama Great thinker unayeheshimika humu ulitakiwa uje na Hoja za kuonesha Huyu mzee ni Con, na sio kutoa tuhuma za maneno matupu na kashfa
Mambo haya ya kashfa waachie kina Jiwe na kundi Lao.
Mpe...Ikawaje sasa baada ya hapo maana umeishia njiani hii simulizi tungeomba uendelee kusimulia