Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Jiwe...Ajuza asante kwa kunirekebisha,amani haisemi kwa maneno bali kwa vitendo.
Nyerere alijenga Taifa moja lisilo na ubaguzi au migawanyiko ya kikabila, kikanda au kidini sasa ni zamu yenu nyie watoto na wajukuu wake kujenga uchumi imara katika Taifa. Badala ya kujikita kufanya hili, huyu mzee wako kucha kutwa analalamika kuhusu wazee wake wa Kariakoo kufunikwa umaarufu na Nyerere na udini.
Kalamu,
Umerejea tena.
Kalamu,
Umerejea tena.
Vitu ninavyoweka hapa si lazima usome.
Viti ninavyoweka hapa nimewakusudia wale wanaofuatilia mjadala huu wasome na watujue sote wawili kwa uzuri kabisa:
PROF. ALI MAZRUI MWALIMU WANGU WA MASAFA MAREFU
Leo alfajir nimeikuta video ya Mwalimu wangu wa masafa marefu Prof. Ali Mazrui.
Imenikumbusha mbali.
Nina umri wa miaka 15/16 namsoma Ali Mazrui katika Sunday Nation kutoka Kenya.
Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."
Sikusita nikakinunua.
Nikimpenda Mazrui sana.
Katika umri ule nilikuwa namsoma Kwame Nkrumah, "Challenge of the Congo."
Namsoma Nkrumah anavyochambua matatizo na fitna ya kampuni kubwa ya Wabelgiji - Union Miniere kwa Patrice Lumumba.
Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.
Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.
Hela zangu zilikuwa zinakwenda kwanza kwenye comics, ice cream, records na mwisho tiketi za cinema kuangalia movies Jumamosi mchana na Jumapili asubuhi saa nne Empire Cinema.
Mara yangu kumuona Prof. Mazrui ilikuwa miaka ya mwishoni 1960s Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sikumbuki ilikuwa kwenye sherehe gani na Julius Nyerere alikuwapo.
Nilikuwa nimefuatana na kaka yangu na rafiki yangu pia Shaabani Muhunzi maarufu kwa jina la Mkorofi yeye alikuwa mwanafunzi pale chuoni na nikimuusudu sana kwa hilo.
Shaaban alinitia hamu ya mimi kufika alipofika yeye.
Chumbani kwangu nilikuwa na ubao na ubao huu alinipa Abdallah Tambaza.
Hivi sasa Abdallah ni mwandishi nguli wa historia ya Dar es Salaam.
Shaaban akija chumbani kwangu mwisho wa juma akitokea Chuo Kikuu anakuta kwenye ubao juu kabisa nimeandika, "English Literature."
Chini yake patafuatia ''passages'' za William Shakespeare tena nikiziandika kutoka kichwani.
Yeye atafuta ataandika, "Literature in English," kunisahihisha bwana mdogo wake.
Akiondoka nitafuta na nitaandika kama nilivyoandika mwanzo.
Juma linalofuatia itakuwa mchezo ni ule ule.
Atanisahihisha mwanafunzi mkaidi na mwalimu wangu akiondoka nitafuta.
Sasa nimekuwa kijana wa kati Mazrui akatengeneza ile ''documentary'' maarufu sana, "Africans: A Triple Heritage."
Hapa ndiyo alinimaliza kabisa.
Nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Said Baamumin tukikaa jirani yeye akifanyakazi UNDP.
Siku moja akaniambia angependa kunipeleka kwao Mtondia Mombasa nikamuone mama yake.
Said Bamumin akanifahamisha kuwa wao wamejenga na wana mashamba katika ardhi ya ukoo wa Mazrui.
Tulipofika Mtondia akanipeleka Takaungu kuona msikiti wa Mazrui ambao una umri kiasi ya miaka 400 na kisima cha asili kipo hapo na bado kinatoa maji.
Ardhi hii ya ukoo wa Mazrui ina historia ndefu katika historia ya Kenya na Mombasa.
Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilimpelekea nakala mwalimu wangu na niliandika ''Kwa Mwalimu wangu wa Masafa Marefu Prof. Ali Mazrui.''
Hivi ndivyo nilivyofahamiana na Prof. Mazrui na tukawa tunaandikiana.
Nakumbuka baada ya kupata kile kitabu Prof. aliniandikia kunishukuru na akaniambia, ''Nimefurahi jinsi ulivyowaandika Waswahili.''
Miaka ikaenda.
Harith Ghassany ndiye yeye aliyenijulisha tena kwa Prof. Mazrui kwa staili nyingine kabisa.
Nilikuwa nimealikwa mkutano Kampala na Prof. Mazrui alikuwa na yeye amealikwa pia.
Nilipomfahamisha Harith akanipa salamu nimfikishie Prof. Mazrui.
Harith alisomeshwa na Prof. Mazrui University of Michigan.
Sote tulikuwa tunakaa Hilton Hotel.
Nilikuwa nimesimama kwenye ''lobby'' ya hotel kwa mbali nikamuona Prof. Mazrui anakuja upande wangu.
Aliponikaribia nikapiga hatua nikamtolea salamu.
Akaniitikia na alipoona ile tabasamu yangu hakupita akaniuliza, ''Tunafahamiana?''
Nikamwambia pia nina salamu zake kutoka kwa Dr. Ghassany.
Nilikuwa nimemtajia Prof. Mazrui watu wake basi akaniambia tukae kitako tuzungumze.
Nilimstaajabisha sana nilipomwambia kuwa nimefika hadi kwao Takaungu na tulizungumza mengi na haukupita muda jamaa wengi wakaja pale tukakaa na Prof. Mazrui na kuzungumzanae.
Mazrui ni mtu asiye na makuu mwepesi wa kuingilika.
Alizungumza na sisi kama vile ni watu tunajuana miaka.
Siku anaondoka kurudi Marekani kanikuta pale ''reception,'' kaja ku-''check out,'' na mimi nina ''check out,'' tukaagana.
Nakumbuka ''typical Mazrui trend,'' alimwambia Manager on Duty pale Hilton, ''Tengenezeni hizi lift kwani zinagoma sana na ikija Mmarekani kanasa kwenye hizi lift zenu atawapelekeni mahakamani.''
Sijui kama wenzangu waliokuwa pale walielewa lakini kwangu mimi ujumbe ulikuwa umefika sawia.
Nikamkumbuka katika ''The Africans: A Triple Heritage,'' anaonekana anafungua bomba la maji katika hoteli moja ya Nyota Tano katika mji mmoja mkubwa Afrika bomba linakohoa halitoi maji.
Mimi kwa tahadhari ile Prof. akawa kanikumbusha hoteli moja Lagos ndiyo nimefika nataka kukoga, nimefungua bomba la maji kwanza bomba likakohoa kisha maji yakaanza kutoka lakini rangi yake ilikuwa ya udongo rangi ya kahawia.
Na Prof. Ali Mazrui
Nile Hilton Kampala 2003
Uko sahihi mkuu! After then wazee wengi waliomsaidia kupigania uhuru hawakuwa wasomi! Lakini hata hivyo alijitahidi sana kumridhisha kila mtu lakini ukizingatia nchi ilikuwa changa na masikini asingeweza kumtosheleza kila mtu!
Yoda,Kuna conmen wanatoka hadi vyuo bora kabisa duniani kama Havard, kwa sasa wako hadi katika mabunge yote mawili ya Marekani.
Yoda,Hivi na jamii nyingine kama Wachaga nao wakianza kudai "wazee wao" kama Thomas Marealle waenziwe sawa na Nyerere kupigania uhuru utakubali?
Yoda,Huko Zanzibar Historia ya Mapinduzi imeandikwa kumzunguka Karume ila hukomalii kuonyesha kuna watu wengi walihatarisha maisha yao kumuondoa Sultan ila kwa Nyerere aliyeweza kuzungumza na wazungu wakawahi kuondoka ndio umeng'ang'ana kumuonyesha alikuwa wa kawaida tu!
"Mrengo."Unapoteza muda na nguvu zako kuandika maandiko marefu yaliyojaa majivuno kujisifu na kujiona wa maana kumbe ni takataka tu,mlengo wako unajulikana.
Wanapewa Tuzo za Academic ama Tuzo za Field zao?Kuna wacheza por**n nao hupewa tuzo,kwahiyo tuzo sio kitu cha kushangaza sana.
Wapelekee wanaozitaka, kwa nini uniletee mimi takataka nisizozithamini, huoni kuwa huo wenyewe nii uchizi unaokusumbua wewe?Kalamu,
Zisikupe shida.
Puuza waachie wengine wanaofurahia kalamu yangu wafurahi.
Kalamu,Wapelekee wanaozitaka, kwa nini uniletee mimi takataka nisizozithamini, huoni kuwa huo wenyewe nii uchizi unaokusumbua wewe?
Jiwe...Sasa tangu lini wauza kahawa wasio enda shule walio kalia kucheza bao wakawa na akili zaidi ya chuki na illusion za dini ya waarabu,
Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...Habari Mh. Mohamed Said ,Tafadhali jibu hoja,Ni Kipi kilichomfanya J.K Nyerere kuwazidi Ujanja wazee wa DONTA?
Mpe,Mpe...
Umependezewa na historia ya babu yangu?
Hei...Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...
Deliberate.Hivi tuna maana gani "UJANJA"? toka lini wazee wa downtown kama wanavyoitwa wakawa wajanja? wazee au watu wengi walikuwa Kariakoo wanadhani walikuwa wajanja lakini ukweli hakuna watu wajinga kama hawa wazee waliokuwa wakidhani wajanja ndio maana hata leo hii hawamiliki chochote Kariakoo hawana asset yoyote wamekuja wageni ndio wanamiliki kila kitu kwa hiyo Nyerere hajamzidi mtu mjanja sababu hakukuwa na wajanja wanywa kahawa tu kama walivyo leo, Nyerere wala hakutumia akili kubwa sababu hakujawahi kuwa na wajanja zaidi ya porojo za midomo tu. Wazee walimiliki nyumba zote za Kariakoo lakini wakaacha magarasa tu kizazi chao kuambulia kuuza tu. Mtu mjanja ni mtu mwenye malengo na Nyerere alikuwa na malengo...
Kwanza naomba msamaha katika nilichoandika sababu nimeandika sikusoma kila kitu lakini nikawa napitia maandiko yako humu na kuelewa unachoaminisha na mimi ni mtu napenda sana kusoma history na umri wangu sio mkubwa kujuwa kila kitu ila ningependa kuongea kidogo katika historia na sio ya Tanzania tu nyingi ziliandikwa kwa malengo fulani ya kisiasa lakini ukweli haukundikwa hata katika suala la kupigania uhuru mimi siamini na sio kwa Tanzania tu ni kwa yaliyokuwa makoloni ya waingereza yote kupewa uhuru ilikuwa arranged sababu England walikuwa hawana uwezo tena ki mali kuendelea kutawala ilikuwa mipango kuziachia nchi hizi zote naamini utatuma darasa kwenye hili uhuru ulipiganiwa au tulipewa? Nyerere alikuwa mwana siasa na siasa ni mchezo na akaucheza ila wazee wengi hawakuwa wanasiasa labda walidhani kama kushabikia Yanga na Simba ndio maana wakaishia njiani. Kitu kimoja na uhakika 100% historia imeandikwa kunufaisha kikundi fulani sio ukweli maana ukweli siku zote unaleta shida ndio maana sijawahi kuamini Iddi Amin alikuwa anakula nyama ya watoto wake lakini wakati ule niliamini sababu tulilishwa propaganda na history yetu kama propaganda. Naomba ushauri ni vitabu gani naweza kusoma haya unayoandika na wapi vinapatika sababu napenda kusoma upande wa pili. sababu sina upande ila nataka kujuwa ukweli kwa faida yangu tu mwenyewe kama hii issue ya Bibi Titi kusimama kupinga ni kitabu gani naweza kusoma hiyo history.Hei...
Tunaweza tukafanya mjadala wa maana usiokuwa na mihemko.
Litengeneze swali lako liwe linaloweza kueleweka.
In Shaa Allah nitakuja kukupa majibu.
Muhimu ni kuwa kwanza uwe na subira ya kusoma rejea nitazokuwekea hapa
(nyingine ni za Kiingereza).
Hapa nazungumzia kusoma kurasa kama 500 hivi.
Uzoefu umenionyesha kuwa wengi wetu hapa hatuna kwanza elimu ya haya tunayotamani kujadili na pili tunapenda kuja hapa kushambuliana na kumshambulia Mohamed Said.
Napenda kuhitimisha kwa kukueleza kuwa ilibidi ipatikane ridhaa ya Mwalimu Nyerere kuweza kujibu mengi katika uliyochanganya katika swali lako hapo juu.
Mwalimu alitoa ridhaa yake na kimeandikwa kitabu ''Nyerere Biography,'' (2020).
Soma kitabu hiki kitakusaidia kupata majibu.
Lakini kabla ya kusoma kitabu hiki itabidi kwanza usome In Shaa Allah hizo rejea nitakazo kuwekea.
Jiwe...Unapoteza muda na nguvu zako kuandika maandiko marefu yaliyojaa majivuno kujisifu na kujiona wa maana kumbe ni takataka tu,mlengo wako unajulikana.
Jiwe...
Niruhusu nikueleze historia ya Msham Awadh na wenzake ''wauza kahawa wasioenda shule...'' katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tangnayika.
''Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake.
Msham Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.
Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba.
Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni Tanganyika.
Hawa ndiyo wazalendo ambao historia yao ilifutwa.
Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya kimagharibi.
Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.
Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.
Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda kutoka Mtwara kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.
Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe wananchi kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.
Wakati haya yanafanyika wamishionari wa Peramiho kulikuwa na mipango ya kuizuia TANU isiingie Jimbo la Kusini.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji Makonde Street Lind aliyoitoa kwa TANU kama ofisi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wanapewa Tuzo za Academic ama Tuzo za Field zao?