Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Yoda,
Sikulazimishi kuamini lakini nimekuwekea hapo nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji iliyokuwa ofisi ya TANU ipo hadi leo.

Nimekueleza na watu waliomleta Nyerere Kusini nk. Salum Mpunga dereva wa lori na ndiye mmoja wa waasisi wa TANU Lindi.

Hawa watu nimekutananao.
 
Chamsingi tuzo,kumaanisha hata wajinga na wapumbafu hupewa tuzo.
Ndio ila unapewa tuzo ya Kijinga, huwezi kuwa mjinga ukapewa Tuzo ya Academic. Kasome hizo Tuzo za Huyo proffesor halafu nitajie mjinga mmoja unayemjua wewe mwenyewe tuzo kama hizo.
 
Ndio ila unapewa tuzo ya Kijinga, huwezi kuwa mjinga ukapewa Tuzo ya Academic. Kasome hizo Tuzo za Huyo proffesor halafu nitajie mjinga mmoja unayemjua wewe mwenyewe tuzo kama hizo.
Baba...
Ghafla naona ukumbi umekuwa kimya.

Kataka mtu kujua nasaba yangu na waliopigania uhuru.

Nimemwela babu yangu kifupi.
Kimya.

Kuna mtu nimemwambia akae kimya.
Kweli kanyamaza.

Kuna mtu kataka historia ya babu yangu.

Nimeweka.
Kimya.

Kuna mtu kanipinga kuwa muuza vipodozi hawezi kupigania uhuru.

Nimemweleza mmoja wa aliyeasisi TANU Southern Province alikuwa dereva wa lori.

Kimya.

Ukimya huu si kawaida.
Iweje watu wawe wapole kiasi hiki?

Tuzo kwa maana ya tuzo umezungumza.

Kimya.
 
Kalamu,
Nitakusaidia tena.
Tufunge mjadala.

Kaa kimya.
Hutonisikia.

View attachment 2555941
Chuo Kikuu Cha Azhar
Cairo 1991

Kwani wewe huwezi kukaa kimya?

Ni nani anayemfuatafuata mwingine akilazimisha takataka zake zionekane kwake?

Ukiendelea kunifuatafuata, ni lazima nikutupie tena hizo takataka zako usoni mwako.
 
Kwani wewe huwezi kukaa kimya?

Ni nani anayemfuatafuata mwingine akilazimisha takataka zake zionekane kwake?

Ukiendelea kunifuatafuata, ni lazima nikutupie tena hizo takataka zako usoni mwako.
Kalamu,
Mimi maisha yangu ni kuandika siwezi kukaa kimya.
Wala sijapata kumfuata mtu kumbughudhi.

Siku zote mimi ndiyo hufuatwa.

Laiti ningekaa kimya watu wengi wangekosa kujua historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na mengine mengi.

Lifikirie Jukwaa la Historia bila ya makala nilizoweka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na mijadala yake inavyotuchangamsha.

Kukaa kimya ningekuwa nimefanya khiyana:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.​
  2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006​
  3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.​
  4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.​
  5. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.​
  6. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.​
  7. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam​
  8. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam​
  9. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam​
  10. Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam​
  11. The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam​
  12. Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam​
  13. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).​
  14. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).​
  15. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)​
  16. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).​
  17. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).​
  18. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).​
  19. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).​
  20. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).​
  21. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).​
  22. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).​
  23. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.​
  24. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.​
  25. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.​
  26. Awards: Several Awards​
  27. Visiting Scholar: (2011)
  28. University of Iowa, Iowa City, USA​
  29. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA​
  30. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.​
  31. OTHER COUNTRIES VISITED
  32. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.​


 
Wewe ni 'conartist', kazi ambayo kila anayeifanya ni lazima aifanye vizuri. Umejifunza mbinu kadhaa za kudanganyia, ikiwemo jinsi ya kung'ang'ania jambo kama unavyofanya hapa.

Nimekwisha kueleza, 'as long as you keep following me, I will not let you go'. That is the bottomline.
Takataka zako unazoziita uandishi hazinikogi mimi, wapelekee wanaokubali kazi yako, siyo mimi.
 
Kalamu,
Nikitaka tuagane.

Ingekuwa kweli unanirushia taka nisingethubutu.

Umenifahamu.
Naamini hutonigusa.

Baki salama.

Angalia watu wangapi wamekuja katika uzi huu.

Umeniandikia Kiingereza.
Nitakuambia.

Nina Merit Pass First Class English Oral.
Cambridge School Certificate 1970.

Nakijua vyema Kiingereza.

Kwaheri ndugu yangu sina kinyongo na wewe juu ya kunizulia uongo kuwa uliniona Northwestern University, Evanston Chicago nikiwa na Wapakistani na juu ya kunitukana.


Prof. Michael Lofchie

 
Naona huko uliko kumejaa takataka. Hii ndiyo biashara yako muhimu inayokupeleka chooni. Kwa hiyo utaing'ang'ania kufa kupona.
 
Kwaheri ndugu yangu sina kinyongo na wewe juu ya kunizulia uongo kuwa uliniona Northwestern University, Evanston Chicago nikiwa na Wapakistani na juu ya kunitukana.
Kwa hili sitanii hata kidogo na najua limekuchoma moyo.
 
Kutokana na hulka yako, hili lingekuwa ni bandiko jingine hapa JF!

Huna kitu.
Kalamu,
Umesema kweli.
Kama kuna kitu Allah amenipendelea toka udogoni ni kusoma na kuandika.

Hakika naweza kuweka bandiko katika hilo.
Ngoja nikupe ambayo naweza kueleza.

Amekuja mhariri kutoka Oxford University Press Nairobi kaja Dar es Salaam tukamilishe kitabu changu ili kichapwe.

Tumemaliza kazi akaniuliza kama kitabu changu nilichoandika niliandika kwa Kiswahili kisha nikamtafuta mtu afanye tafasiri.

''Hapana nimeandika kwa Kiingereza mimi mwenyewe OPU wamenichukua kwa ajili ya ujuzi wangu wa historia na lugha ya Kiingereza.''

Hilo ndilo lilikuwa jibu langu.

Niliingia mashindano ya English Elocution na nilisoma hotuba ya Dr. Martin Luther King, ''I have a Dream.''

Shule yetu St. Joseph's Convent ikiogopewa Dar es Salaam nzima kwa wanafunzi kuzungumza Kiingereza safi.

Je, ungependa kujua kama nilishinda hayo mashidano au vipi?
Nina vitu vingi sana.

Watu wa vitabu wanataka niwape mswada watoe kitabu.
Ndugu yangu unasema sina kitu.


Lincoln Memorial, Washington DC
Martin Luther King alisimama hapo niliposimama kutoa hotuba hiyo ''I have a Dream" mwaka wa 1963​
 
Kwa hili sitanii hata kidogo na najua limekuchoma moyo.
Hapana.
Wewe ndiye unachomwa moyo na ndiyo sababu unanitukana.
Wewe ni mtu wa matusi.

Mtu hatoi matusi kutukana ila awe akili yake imemkimbia.
Hili sitanii hata kidogo...
 
Mpe
Mpe...
Imekuwaje umekuwa kimya?
Napenda kukuhadithia historia ya babu yangu Salum Abdallah.

Bado haijesha:

SIKU BABU YANGU SALUM ABDALLAH ALIPOMKABILI FREDERICK MCHAURU KATIKA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TANGANYIKA RAILWAYS TABORA 1947​

Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania January 10, 2018 0
SIKU BABU YANGU SALUM ABDALLAH ALIPOMKABILI FREDRICK MCHAURU KATIKA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TANGANYIKA RAILWAYS TABORA 1947



Fredrick Mchauru


Salum Abdallah
Ndani ya gazeti la Raia Mwema (Januari 3-9, 2018) kulikuwa na makala ya maisha ya Mzee Fredrick Mchauru.

Kama kawaida yangu kupenda kusoma maisha ya Watanzania maarufu niliitupia jicho.

Haikunipitikia kabisa kama Mzee Mchauru niliyemtaja katika kitabu change cha historia ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1998 bado atakuwa hai.

Jina hili likawa linajirudia akilini kwangu.
Naam Mzee Mchauru yu hai akiwa sasa na umri wa miaka 97.

Huyu Mchauru ndiye yule aliyekabiliana na na babu yangu Salum Abdallah katika uwanja wa mpira wa Town School Tabora chini ya miembe wakati wa kupambana na wakoloni, babu yangu akisimama na wananchi wa Tanganyika wakati Mchauru akiwa mtumishi wa serikali ya Waingereza?

Naam ndiye yeye.

Makala ile ilikuwa tamu haikuisha imekuja kuhitimishwa na toleo la juma hili la Raia Mwema (10 – 16 Januari 2018).

Katika toleo hili mwandishi Ezekiel Kamwaga kanitaja kwa jina kuwa nimemwandika Mzee Mchauru katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kamwaga akaeleza kuwa nimepata kusema kuwa Mzee Mchauru alipata shida kuelewana na wale waliokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.


Dhulma ilikuwa imezidi sana na wafanyakazi wa bandarini Dar es Salaam wakiongozwa kwa siri na Abdul Sykes wakati ile kijana mdogo wa miaka 23 waliamua kufanya mgomo kudai haki zao. Mgomo wa Makuli kama ulivyokujafahamika ulienea Tanganyika nzima.

Lakini ili kuuelewa mgomo huu ni muhimu sana msomaji akasoma historia nzima ya mgomo huu chanzo chake na vipi wananchi waliweza kujiunga pamoja hadi kufikia kuwa na uwezo wa kuitingisha serikali kwa mgomo kuenea Tanganyika nzima.

Haiwezekani kwa hapa kueleza historia yenyewe nitakachifanya nitaweka link ili msomaji kwa wakati wake mwenyewe baadae aweze kusoma lakini kwa sasa napenda kukunyambulieni ilikuwaje hadi babu yangu akapambana uso kwa macho na Fredrick Mchauru katika mgomo wa wafanyakazi wa mwaka wa 1947:


http://www.mohammedsaid.com/2014/03/the-book-abdulwahid-sykes-and-dar-es.html

http://www.mohammedsaid.com/2014/03/abdulwahid-sykes-and-dar-es-salaam.html
http://www.mohammedsaid.com/2014/03/abdulwahid-sykes-and-dar-es-salaam_7.html

Itaendelea In Shaa Allah...
 
'Con artist' yeyote ni lazima awe na ufundi wa kutengeneza matukio yanayo 'support' kazi hiyo anayofanya. Wewe usingekuwa con artist' mzuri bila ya kutengeneza na kuyapangilia matukio yote haya ili kuonyesha ushahidi wa utapeli unaoufanya.
 
Hapana.
Wewe ndiye unachomwa moyo na ndiyo sababu unanitukana.
Wewe ni mtu wa matusi.

Mtu hatoi matusi kutukana ila awe akili yake imemkimbia.
Hili sitanii hata kidogo...
Matusi yapi tena wakati nazipa jina sahihi la 'takataka' hizi kazi za utapeli ulizofanya maisha yako yote?
Hivi unayo kazi nyingine yoyote mbali ya takataka hizi?
 
Ndiyo takataka gani hii tena?
BBC Kiswahili? Mbona unasoma maandishi yaliyotayarishwa na wengine?
Kalamu,
Kuna mtu kaniuliza kwa nini unanitukana nami nakuwa kimya sirejeshi matusi.
Inaelekea huyu ni kijana mdogo damu yake inachemka anadhani jibu ni moto kwa moto.

Akaenda mbali akaniambia kwa nini hapo juu badala ya kukuita ''Kalamu,'' nisikuite hilo neno ambalo wewe unalipenda kulitumia.

Neno lenyewe nimelifanyia heavy ink hapo kwako yaani bold.

Nikamwambia kuwa mimi hii elimu ya mnakasha yaani mijadala nimesomeshwa chuoni sina maana ''university'' maana yangu madrasa.

Mwalimu wangu Sheikh Haruna alituwekea sana msisitizo katika adabu ya mijadala kuwa umuheshimu mtu unaejadiliananae usimtukane wala kumkejeli.

Sasa ikiwa mimi nitamwita yeye neno hili nitakuwa nimemtukana.

Maalim Haruna akatufunza kuwa ukitukana au kukejeli hiyi ni dalili kuwa kichwani hamna kitu.

Sheikh akipenda kusema hivyo, ''kichwani hakuna kitu.''
Watu wakijua hamna kitu watakudharau na hutokuwa katika kundi la wajuzi.

Tuingie katika Studio za BBC.
Hapo sisomi cha mtu.

Nasoma ''script'' niliyoandika mwenyewe kuhusu kumbukumbu ya David Livingstone iliyoko kijiji cha Blantye, Scotland alikozaliwa.

Kijiji kizima kimeguzwa kuwa kumbukumbu.
Kijiji hiki hakiko mbali sana na Glasgow.

Nilifika hapo kwa ajili ya kufanya kipindi ''Barua Kutoka Glasgow.''

Shughuli hii ilianzia BBC London Bush House siku kama tatu zilizopita hadi mimi kuingia hapo studio BBC Glasgow kufanya kipindi hicho.


Picha ya chini kushoto ni Blantyre, Scotland David Livingstone Museum​
 
haya matakataka utajaza humu hadi lini na kwa faida gani?
 
haya matakataka utajaza humu hadi lini na kwa faida gani?
Kalamu,
Ninayoandika hapa ni historia inayopendwa na wasomaji wengi.
Angalia uzi huu watu wangapi wanaingia.

Wanakuja kusoma historia ambayo inayowafurahisha.
Naandika kwa faida ya wasomaji wa Ukumbi wa Historia.

Mchana huu nimeweka hapa historia ya babu yangu Salum Abdallah siku alipoongoza mgomo wa railways mwaka wa 1947.


Viongozi wa TRAU
Kulia kwa Salum Abdallah ni Kassanga Tumbo​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…