Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Mzee saidi Mohammed mpaka leo anamlaani Mh nyerere kwa kuwanyima wazee wa kariakoo madaraka wale wazulu wahamiaji kutoka koloni la wareno na kusaidia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964
 
Madai yako ni imaginable ndiyo maana Pro. Haroub alishangazwa na madai yako.
Kwa elimu na wakati alioshi P. Haroub asingelishangazwa na madai yako ikiwa Yalikuwa kwenye ukweli.
Unadanganya hadi unapitiliza na kujishitaki mwenye.
Let..
Hapana sithubutu kuandika uongo katika historia ya uhuru wa Tanganyuika kwa sababu wenyewe waliopigania uhuru huo walikuwa hai.

Ngombale Mwiru alikuwa yu hai yeye aliingizwa TANU na Ally Sykes haya kaeleza mwenyewe.

Prof. Haroub hakuwa anajua ule udugu uliokuwapo kati ya Mwalimu na Abdul.

Prof. Haroub hakuamini hadi alipokwenda kumuuliza Ahmed Rashad yale ambayo yeye hakuyaamini.

Ahmed Rashad na Abdul Sykes walijuana 1936 wakiwa watoto wadogo na wakawa marafiki ndugu hadi Abdul alipofariki 1968.

Ahmed Rashaad alimweleza kila kitu Prof. Haroub kiasi akamwambia ikiwa wewe unashangaa kuambiwa kuwa Abdul Sykes ndiye aliyekuwa nguvu katika kuasisi TANU utashangaa pia nikikuambia kuwa African Association iliasisiwa na baba yake Abdul, Mzee Kleist Sykes mwaka wa 1929?

Mimi ndiye niliyepata mshangao mkubwa zaidi kuwa Prof. Haroub hakuwa anaijua historia ya TANU.

Nitakueleza kitu ujue kuwa Prof. Haroub hakuwa anazijua siasa na historia za watu wa Dar es Salaam.

Prof. Haroub alikuwa mshenga wa kutaka kuposwa bint ya Ahmed Rashaad.

Walipofika nyumbani kwa Ahmed Rashaad na shughuli imeanza Prof. akatoka barua kumpa Ahmed Rashaad na walikuwa wamekaa pamoja bega kwa bega na Abbas Sykes.

Ahmed Rashaad hakupkea barua hiyo akamwambia amkabidhi Abbas Sykes.
Prof. akaja kunieleza kisa hiki na kuniuliza kwa nini aliambiwa posa ile ipokelewe na Abbas Sykes?

Nikampa historia nzima ya Mzee Rashaad na Abdul Sykes na kuwa ule urafiki baada ya kifo cha Abdul ulihamia kwa Abbas.

Ndipo nikajua kuwa Prof. Haroub si mjuzi wa historia yetu.
Ningeandika uongo sasa hivi nishafedheheka.

Kulia Sheikh Ahmed Islam, Ahmed Rashad Ali na Prof. Haroub Othman 1997​
 
Mzee saidi Mohammed mpaka leo anamlaani Mh nyerere kwa kuwanyima wazee wa kariakoo madaraka wale wazulu wahamiaji kutoka koloni la wareno na kusaidia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964
Nelson...
Hapana siwezi kumlaani mtu imani yangu inakataza.

Wala sikuandika kitabu cha Abdul Sykes kwa kuwa wazee wangu hawakupewa madaraka katika serikali.

Wala wazee wangu hawakupigania uhuru ili wao waje kukalia viti.

Mimi nimeandika kitabu kusahihisha historia ya TANU ambayo ilijaa makosa mengi sana.

Ukisoma kitabu hutokuta popote nilikotaja kugawana madaraka.
Hayo mengine nimeyakalia kimya kwa kuwa naona si muhimu kuyasemea hapa.

Unajua mchango wa hao akina mama hapo chini katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Watu wanacheza bao,kunywa kahawa cku nzima,wanawaza simba na yanga tu kwa nini wasizidiwe ujanja🤣🤣
 
Watu wanacheza bao,kunywa kahawa cku nzima,wanawaza simba na yanga tu kwa nini wasizidiwe ujanja[emoji1787][emoji1787]

Hawakua na akili kama mjukuu wao mzee side boi,amebaki kujisifia na kujitambia picha alizopiga na wazungu,mzee limbukeni na mshamba.
 
Watu wanacheza bao,kunywa kahawa cku nzima,wanawaza simba na yanga tu kwa nini wasizidiwe ujanja🤣🤣
Kop...
Mathalan nikikuomba ushahidi kuwa wazee wangu walikuwa wanacheza bao na kunywa kahawa siku nzima na wanawaza Simba na Yanga unaweza kuuweka hapa?

Kahawa na kucheza bao ni katika mila za watu wa Pwani kama wengine wanavyokunywa pombe za kienyeji katika vilabu vya pombe zinazouza dengerua, mbege, kimpumu nk.

Hawa unaowakejeli wewe kuwa ni wanywa kahawa na kucheza bao ndiyo waliounda chama cha TANU na kupiogania uhuru wa Tanganyika.

Soma majina ya ''wanywa kahawa na wacheza bao'' waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo August 1954:

Rajab Diwani, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Julius Nyerere, Mshume Kiyate, Max Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Rashid Ali Meli, Clement Mohamed Mtamila, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafungo, Schneider Abdillah Plantan, Iddi Tulio, Marsha Bilal na Denis Phombeah aliyekuwa Menaja wa Arnautoglo.

Soma pia hapo chini majina ya wanywa kahawa na wacheza bao walioasisi African Association mwaka wa 1929:

Kleist Abdallah Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Naomba nami nikuulize wakati hawa ''wanywa kahawa'' wanawatayarisha Watanganyika kupigania uhuru wazee wako wewe wanywa pombe za kienyeji siyo siku nzima bali kwa nyakati maalum walikuwa wanafanya nini?

Mwangalie Julius Nyerere hapo chini na ''wacheza bao kutwa nzima na wanywa kahawa'':

Attachments

  • 1679334745619.png
    1.8 MB · Views: 4
Watu wanacheza bao,kunywa kahawa cku nzima,wanawaza simba na yanga tu kwa nini wasizidiwe ujanja🤣🤣
Kop...
Mathalan nikikuomba ushahidi kuwa wazee wangu walikuwa wanacheza bao na kunywa kahawa siku nzima na wanawaza Simba na Yanga unaweza kuuweka hapa?

Kahawa na kucheza bao ni katika mila za watu wa Pwani kama wengine wanavyokunywa pombe za kienyeji katika vilabu vya pombe zinazouza dengerua, mbege, kimpumu nk.

Hawa unaowakejeli wewe kuwa ni wanywa kahawa na kucheza bao ndiyo waliounda chama cha TANU na kupiogania uhuru wa Tanganyika.

Soma majina ya ''wanywa kahawa na wacheza bao'' waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo August 1954:

Rajab Diwani, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Julius Nyerere, Mshume Kiyate, Max Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Rashid Ali Meli, Clement Mohamed Mtamila, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafungo, Schneider Abdillah Plantan, Iddi Tulio, Marsha Bilal na Denis Phombeah aliyekuwa Menaja wa Arnautoglo.

Soma pia hapo chini majina ya wanywa kahawa na wacheza bao walioasisi African Association mwaka wa 1929:

Kleist Abdallah Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Naomba nami nikuulize wakati hawa ''wanywa kahawa'' wanawatayarisha Watanganyika kupigania uhuru wazee wako wewe wanywa pombe za kienyeji siyo siku nzima bali kwa nyakati maalium walikuwa wanafanya nini?

Mwangalie Julius Nyerere hapo chini na ''wacheza bao kutwa nzima na wanywa kahawa'':

View attachment 2559601
View attachment 2559604
 
Kalamu,
Ahsante.

Madina 2014​
Picha ninayoiona juu yako ni mtu aliyekaa juu ya mlima wa taka, akichimbua kwenye rundo hilo taka na kuzisambaza kila mara. akitegemea kila anayemsambazia ataona thamani ya hizo taka.
Tena anazisambaza kwa kulazimisha.
 
Huwezi.kulazimisha chochote mtandaoni.

Kuna "Block" na "Delete.
Rahisi sana.

Muscat

Kalamu,
Huwezi.kulazimisha chochote mtandaoni.

Kuna "Block" na "Delete."
Rahisi sana.
Hapana.
Rahisi ni kutobonyeza kitufe hapo nilipoweka maneno yangu. Usibonyeze hicho kidude, hapo mambo yatakuwa yamekwisha.
Hili nakufundisha kama ulikuwa hujui.
Usibonyeze"Reply". Simple!
 
Hapana.
Rahisi ni kutobonyeza kitufe hapo nilipoweka maneno yangu. Usibonyeze hicho kidude, hapo mambo yatakuwa yamekwisha.
Hili nakufundisha kama ulikuwa hujui.
Usibonyeze"Reply". Simple!
Hapana,
Mimi sina tatizo tuko pamoja.
Wewe unifundishe mimi?

Maryland, Washington
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…