Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Umeandika uongo umestukiwa na sasa unajishaua.

Mwandiko wako ni ule ule(arrogantly) haufichiki hata ukija na id nyingine, tunaukumbuka miaka ile mkaungana kikundi mkijidai mtakuja na kitabu, mkadondokea pua mpaka leo hii.
Duh!
Na wewe umeibuka toka pango gani linalokuhifadhi kusikofika mwanga!

Humjui 'Kalamu' wewe?
 
Duh!
Na wewe umeibuka toka pango gani linalokuhifadhi kusikofika mwanga!

Humjui 'Kalamu' wewe?
Nikujuwe wewe nani zaidi ya kuja hapa na uongo ukastukiwa.

Unamtisha Muislam? Umebuugi.

Muislam hamuogopi isipokuwa Allah pekee. Kumbuka hilo.
 
Yatanisaidia kitu gani haya mimi!
Kalamu,
Waingereza wanasema, "Seeing is believing."

Hapa unapoweka kitu umekiweka kwa dunia nzima kukiona au kukisoma.

Hii ndiyo faida yake.

Nimemweka Yvonne Chakacha kwa makusudi ili wanaofatilia mjadala huu na kusoma mimi nikinasibishwa na taka wakupime kwa maneno yako.

Hii mosi.

Pili ni kutaka kuhangaisha akili za wasomaji - Mohamed Said na Yvonne Chakacha wapi na wapi?

Wapi wamekutana?
Hapo wanazungumza nini?

Mimi huwa sijibu tusi kwa tusi:


''Let the Good Times Roll''


 
Wewe achana na mambo ya TANU. Unachoandika chochote kinaishia kwa Sykes na uislamu. Wewe ni mtu hatari.
 
Wazee wa Kariakoo hawakuwa tofauti na wale wazee wa kichaga waliotaka uhuru wa uchagani tu. Hao nia yao ilikuwa sio kuikomboa nchi nzima.. Mwalimu Nyerere alifanya vizuri kuwafutilia mbali kwasababu nia yao ilikuwa ovu ya kujinufaisha na kuueneza uislamu. Wewe mwenyewe ulishawahi sema ulishiriki kwenye kuwavunia wafanyabiashara mabucha yao ya kitimoto. Mngesikilizwa si mngefanya mambo mengi zaidi ya kipuuzi kwenye nchi huru?
 
Wewe achana na mambo ya TANU. Unachoandika chochote kinaishia kwa Sykes na uislamu. Wewe ni mtu hatari.
Mama...
Siwezi kuachana na TANU kwani ndiyo chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Hii mosi.

Pili chama hiki kimeasisiwa na wazee wangu.

Nikikiacha chama hiki maana yake ni mimi kuwa mtu nisiyekuwa na historia.

Huu ni muhali mkubwa kwangu.

Mwisho huwezi kuitenganisha TANU na akina Sykes.

Wala huwezi kuwatenganisha akina Sykes na harakati za uhuru.

Huwezi kuwatenganisha akina Sykes na historia ya Julius Nyerere.

Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ni sehemu ya historia ya TANU.

Safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO 1955 dua na hafla ya kumuaga ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika New Street na Stanley.

Walijaribu kuifuta historia hii na kuwafuta akina Sykes katika historia ya Tanganyika.

Matokeo yake ndiyo haya.
 
Mama...
Nionyeshe mahali niliposema nimevunja mabucha ya nguruwe.

Hii ni historia nzuri.
Naamini sote tutaburudika.

Ama kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika nimeiandika na ipo inasomwa hapa nchini na nje ya mipaka yetu.

Kitabu cha historia hii sasa ni maarufu sana.

Kinakwenda chapa ya tano.
 
Kalamu,
"Con" anahadhiri vyuo vikuu anatiwa kwenye miradi ya Harvard na Oxford University Press ya kuandika vitabu vya historia.

Itabidi nitoe darsa kwa faida ya wasomaji:

COUNT VICTOR LUSTIG JIZI BINGWA

Dunia haijapata kushuhudia mwizi kumshinda Count Victor Lustig.

Nimesoma kitabu chake miaka 50 iliyopita lakini hadi leo jina lake sijalisahau wala kitabu kilichaoandikwa kuhusu yeye, ''The Man Who Sold The Eiffel Tower.''

Hili jizi liliuza Eiffel Tower si mara moja bali mara mbili.

Kila nikifika Paris lazima nikautazame huu mnara marufu duniani ambao ndiyo umekuwa alama ya Paris na kununua kijimnara kidogo kupamba nyumbani kwangu.

Lazima mtu utashangaa vipi jizi hili liliweza kuuza mnara ule si mara moja bali mbili na kuchukua fedha?

Nini ilikuwa siri yake?
Siri yake ilikuwa akili yake.

Hata wizi unahitaji matumizi ya akili na mipango mizuri ya kuiba.

Ukiacha huu wizi wa kuuza huu mnara wa Paris, Count Victor Lustig kawaibia watu wenye akili na nguvu duniani kama Fidel Castro wa Cuba na Papa Doc wa Haiti.

Ingawa Castro hakuwa mtu wa kumfanyia maskhara na ukapona jinsi alivyokuwa na watu ambao kama atamnyooshea mtu kidole watu wake wa usalama wanaweza kukusaka hadi wakakutia mkononi uko hai au maiti lakini hakumpata Count Victor Lustig baada ya kumuingiza mjini.

Count Victor Lustig aliingia Havana Cuba kwa ndege binafsi akitokea Florida na alikuwa na miadi na Castro.

Hakuwa na maneno mengi alimuomba avute pazia za ofisi yake pawe kiza akaweka ''projector'' na ''screen'' akamuonyesha filamu anayotaka kutengeneza ya Castro yuko Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.

Filamu ilikuwa fupi ya kiasi cha dakika kumi hivi.

Akamwambia Castro kuwa yeye ni mtengenezaji filamu na amekusudia kutengeneza filamu ya maisha yake akiwa Sierra Maestra na Che Guevara wanapambana na Batista.

Castro alikipenda kile alichokiona na mikataba ikawekwa saini.

Count Victor Lustig akaondoka Havana na mkoba umejaa dola mpya za mia, mia zilizofungwa vyema.

Count Victor Lustig hakuonekana tena Havana.

Castro na wasaidizi wakajua kuwa wameliwa.

Papa Doc wa Haiti aliyekuwa anatawala watu wake kwa uchawi na vitisho vya Ton Ton Macoute.

Papa Doc alimuuzia magari ya kifahari aina ya Cadillac lakini yote yalikuwa yameibiwa Marekani akayavusha kwa njia za panya hadi Haiti.

Papa Doc alipotambua kuwa yale magari yote yalikuwa yameibiwa Count Victor alikuwa kesharejea Marekani siku nyingi.

Mazombie yaani wale Ton Ton Macoute wala uchawi wake uliokuwa unaogopwa na wananchi wake haukuweza kumdhuru Count Victor Lustig.

Maofisa wa serikali yake walishangaa vipi ule uchawi wake na ''vodoo'' na Ton Ton Macoute wake hawakuweza kufua dafu mbele ya akili ya Count Victor Lustig.

Wizi wowote ule ili ufanikiwe unahitaji mipango na matumizi ya akili.

Bila matumizi ya akili na mipango mwizi atakuwa anakamatwa kila siku.


Eiffel Tower hiyo nyuma yangu​
 
Wewe kama Great thinker unayeheshimika humu ulitakiwa uje na Hoja za kuonesha Huyu mzee ni Con, na sio kutoa tuhuma za maneno matupu na kashfa

Mambo haya ya kashfa waachie kina Jiwe na kundi Lao.
 
Kalamu,
Nakuelewa vizuri.

Hutokea wakati mwingine mtego ukamnasa chui.
Mwindaji mjinga ndiye atausogelea mtego wake.

Ulidhani una uwezo wa kupambana na mimi.

View attachment 2554163
Columbia University, New York.​
Samahani mkuu, naomba kujua miongoni mwa wanaharakati wa ukombozi wa Tanzania yupi ni mzazi au una damu nae ya kindugu? Samahani kama mtakuwa nimekukosea
 
Samahani mkuu, naomba kujua miongoni mwa wanaharakati wa ukombozi wa Tanzania yupi ni mzazi au una damu nae ya kindugu? Samahani kama mtakuwa nimekukosea
Ngome,
Hujanikosea ndugu yangu.
Inapendeza watu tukifahamiana:

BABU YANGU SALUM ABDALLAH POPO

Ikiwa umemsoma babu yangu Salum Abdalah na kigoma chake cha daku utakuwa umeona kuwa alipata kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964.

Hayo hapo chini yatakusaidiwa kumwelewa mtu huyu.

Ilikuwa mwaka wa 1965 babu yangu Salum Abdallah katoka jela ya Uyui Tabora alikowekwa kizuzini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964 hana kazi yuko nyumbani.

Mwaka wa 1953 akiwa na taarifa kutoka Dar es Salaam kuwa kuna harakati za kuunda chama cha siasa yeye na wenzake Tabora wakawa wanafanya mikutano ya siri kila Jumapili Town School ambako Abubakar Mwilima alikuwa mwalimu na yeye Mwalimu Abuu kama walivyopenda kumwita ndiye aliyekuwa akiwafungulia darasa moja kukutana na kupeana habari kutoka New Street Dar es Salaam, Makao Makuu ya TAA.

Hii ailikuwa baada ya kumtuma Katibu wa TAA Western Province, Germano Pacha kwenda Makao Makuu ya TAA kuwapa taarifa kuwa Tabora inataka kuunda chama cha siasa.

Germano Pacha alipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes na akamwambia arudishe salamu Tabora kuwa wafanye subira.

Tufupishe kisa kwani kuna mengi.

TANU ikaundwa mwaka wa 1954 babu yangu akiwa mmoja wa wanachama wa mwanzo.

Mwaka wa 1955 babu na Kassanga tumbo wakaunda Tanganyika Railway African Union (TRAU) babu akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary.

Babu yangu Salum Abdallah ana historia ya uzalendo ya kusisimua ambayo hutochoka kuisikiliza kila inapohadithiwa kwa kuwa mkasa una kuwa ndani ya mkasa mwingine visa vikiunganishwa kama ushanga katika uzi.

Mwaka wa 1965 baba akanifungia safari niende Tabora kumwangalia babu baada ya kutoka kifungoni.

Babu yangu jina lake alililopewa na baba yake Abdallah Mwekapopo (naweza kwenda vizazi saba hadi kwa waliokuwa Belgian Congo) ni Rashid lakini katika ujana wake akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1930 alimpiga Mzungu akafungwa na alipotoka jela akabadili jina lake akawa Salum Abdallah.
Kisa gani akampiga Mzungu?

Huyu Mzungu alikuwa mbaguzi, mnyanyasaji Waafrika kwa hiyo babu siku moja akaamua kumshughulikia.

Hili lilikuwa kosa kubwa sana wakati wa ukoloni.

Hukaa nikafikiri yule Mzungu alikuwa katika hali gani baada ya kuingia katika mikono ya babu kwani alikuwa kapanda juu futi sita ana kifua kipana ile mitambo, yaami maumbo makubwa ya Kimanyema.

Kwa ajili ya umbo hili akiwa kijana Waingereza walimfunza kazi ya kufua chuma, yaani ‘’foundry,’’ kazi ngumu katika moto na joto kali.

Hii ‘’foundry ’’ ilikuwa ndani ya karakana ya Tanganyika Railways.

Humo ndani ya karakana wanaume wako vifua wazi na nyundo nzito ni kelele za chuma kikigonga chuma cheche za moto zikiruka na miaka ile hakuna vifaa mfanyakazi atavaa kuzuia kelele.

Hii karakana ndiyo ilikuwa ikachonga spea za treni.

Wenyewe kwa wenyewe ndani ya karakana wakizungumza kwa sauti za juu.

Labda ndiyo sababu babu hata akizunngumza hata katika mazungumzo ya kawaida sauti yake siku zote ilikuwa juu.

Hii karakana ilikuwa ndani ya eneo la Tanganyika Railway lakini jirani na Arab Street hivi sasa Mtaa wa Nkrumah na ndiko lilipokuwa lango kuu la wafanyazi wa Tanganyika Railways wakiingilia na kutokea katika miaka ile ya 1930.

Babu akiishi Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes).

Nyuma aliyokuwa akiishi ilikuwa inatazamana na nyuma ya Kleist Sykes ambae yeye alikuwa Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu) Tanganyika Railways.

Nafasi kubwa sana wakati ule kwani hio kazi wakifanya Wahindi.

Lakini babu yangu juu ya ubabe wake na haya yote alikuwa mtu karimu sana mimi nimeshuhudia kwa macho yangu na labda huu ukarimu alimrithisha baba yangu kwani mara nyingi nikipisha wageni chumbani kwangu nami kwenda kulala ‘’sitting room,’’hadi waondoke.

Hii Karakana ya Railway ikahamishwa Dar es Salaam mwaka wa 1947 kupelekwa Tabora na babu yangu akahamanayo kwenda huko.

Hakurudi tena Dar es Salaam.

Lakini mwaka huo huo alipofika Tabora akaongoza mgomo wa Railway ulioenea nchi nzima na akafanya hivyo mwaka wa 1947, 1949 na tena mwaka wa 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka.

Huu mgomo wa mwaka wa 1960 ulidumu kwa siku 82 na kuweka rekodi kushida mgomo wa Kenya ulioongozwa na Makhan Singh uliodumu kwa siku 62.

Baada ya mgomo huu wa mwaka wa 1960 Nyerere ilimhidhihirikia kuwa mtu huyu atakuja kumpa shida katika Tanganyika huru akawa sasa anamtazama kwa macho mawili.


Salum Abdallah Popo​
 
Ikawaje sasa baada ya hapo maana umeishia njiani hii simulizi tungeomba uendelee kusimulia
 
Hii nimeipenda sana inafikirisha sana kumbe dunia Ina watu wenye akili nyingi hivi

Ungetusimilia na ile ya Charles Ponzi maarufu km Ponzi Scheme

Pia usimsahau Eduardo de Valfierno huyu nasikia alikwiba picha ya Mona Lisa
 
Nikujywe wewe bani zaidi ya kuja hapa na uongo ukastukiwa.

Ubamtisha Muislam? Umebuugi.

Muislam hamuogopi isipokuwa Allah pekee. Kumbuka hilo.
EEeeenHeeee!
hata hueleweki unachoandika hapa. Ulevi uliokukolea kichwani mwako usidhani kila mtu anaushadadia.
Kaa na ulevi wako, usitake na wengine wahusike nao.

Hovyo kabisa.
 
 
Takataka tu hizi.
 
Wewe kama Great thinker unayeheshimika humu ulitakiwa uje na Hoja za kuonesha Huyu mzee ni Con, na sio kutoa tuhuma za maneno matupu na kashfa

Mambo haya ya kashfa waachie kina Jiwe na kundi Lao.
Mkuu, nilishaeleza msimamo wangu siku nyingi kuhusu haya ya huyu mzee. Hii siyo mara ya kwanza; na hata katika mada hii hii, bandiko langu la kwanza kabisa nimeeleza ninaposimamia.

Mweleze huyo mzee wako kwamba hamsaidii kitu kuendelea kuniita kwenye takataka zake humu anazobandika akini'quote', sina muda nazo isipokuwa kumjibiu tu kuwa ni takataka ambazo sina muda wa kuzisoma.

Akiacha kunifuatilia, hunioni tena. Lakini akeendelea, ni kazi rahisi kwangu kuendelea na kuziita takataka tu.
Hili halinipi shida, na wala haliniondolei kitu chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…