Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Anakupa za uso mpaka na picha juu zinakulamba viboko. umebaki kubwabwaja tu. Hoja huna umeanza name calling. Muflis.
 
Kalamu,
Nimekupa nafasi ya kumaliza mjadala nikakuambia umeghadhibiko tusitishe mjadala.

Hukutaka ukarejea.
Nikakueleza tena tumalize mjadala.

Sina shida na hiyo milango yako na ni kwa vipi inafunguka.
Kila mtu ana milango yake.
''Kalamu,
Umeghadhibika.

Mimi na wewe tusitishe mjadala huu hadi baadae.''
#68

Ukarejea tena:
''Dah!
Hizi mbinu za mijadala wengine tulishazisoma na kuzielewa siku nyingi sana.
Kiufupi ni kwamba hakuna "mjadala" kati yetu. Huwezi kujadili uongo, jambo ambalo ni batili.''
#71

Hilo la taka halinipi shida kwani hapa JF na kwengine nafahamika.


Humburg​
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hiki Kiswahili anachoongea Mohamed Said,inaonekana hata wazee waliomsaidia Nyerere ndio walichoongea-kimejaa ujanja ujanja mwingi-endapo Nyerere angekaa nao bega kwa bega,hii nchi ingemshinda mapema-ilibidi kwa manufaa ya nchi apige upanga mapema
 
Nyerere alijenga Taifa moja lisilo na ubaguzi au migawanyiko ya kikabila, kikanda au kidini sasa ni zamu yenu nyie watoto na wajukuu wake kujenga uchumi imara katika Taifa. Badala ya kujikita kufanya hili, huyu mzee wako kucha kutwa analalamika kuhusu wazee wake wa Kariakoo kufunikwa umaarufu na Nyerere na udini.
Manufaa yepi yaliyopatikana nchi hii? Ikiwa mpaka leo miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado tunashindwa kukidhi hata mahitaji ya bajeti ya nchi sisi wenyewe.
 
Anakupa za uso mpaka na picha juu zinakulamba viboko. umebaki kubwabwaja tu. Hoja huna umeanza name calling. Muflis.
Sina muda wa kupoteza na chizi wa aina yako.
Nakuachia hapa.
 
Mzee, ni hivi, kila utakapokuwa unaweka takataka zako baada ya kuni'quote', jibu toka kwangu ni lile lile. Hizi ni takataka nisizokuwa na muda wa kuzisoma.
 
Uko sahihi mkuu! After then wazee wengi waliomsaidia kupigania uhuru hawakuwa wasomi! Lakini hata hivyo alijitahidi sana kumridhisha kila mtu lakini ukizingatia nchi ilikuwa changa na masikini asingeweza kumtosheleza kila mtu!
 
Huko Zanzibar Historia ya Mapinduzi imeandikwa kumzunguka Karume ila hukomalii kuonyesha kuna watu wengi walihatarisha maisha yao kumuondoa Sultan ila kwa Nyerere aliyeweza kuzungumza na wazungu wakawahi kuondoka ndio umeng'ang'ana kumuonyesha alikuwa wa kawaida tu!
 
Nyerere aliyakuta hayo, ndiyo maana akapokewa na kukaribishwa kuishi na Waislam, yeye na familia yake.
 
Ukishakuwa fanatic wa kidini kuna watu pia huko kwenye systems za kidunia vichwa vyao ni fyatu kwenye hayo mambo, wanaweza kukuchanganya tu kama extremist hatari wa kidini.
 
Sina muda wa kupoteza na chizi wa aina yako.
Nakuachia hapa.
Kalamu,
Umerejea tena.

Sina muda wa kupoteza na chizi wa aina yako.
Nakuachia hapa.
Kalamu,
Umerejea tena.

Vitu ninavyoweka hapa si lazima usome.

Viti ninavyoweka hapa nimewakusudia wale wanaofuatilia mjadala huu wasome na watujue sote wawili kwa uzuri kabisa:

PROF. ALI MAZRUI MWALIMU WANGU WA MASAFA MAREFU
Leo alfajir nimeikuta video ya Mwalimu wangu wa masafa marefu Prof. Ali Mazrui.
Imenikumbusha mbali.

Nina umri wa miaka 15/16 namsoma Ali Mazrui katika Sunday Nation kutoka Kenya.
Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."

Sikusita nikakinunua.
Nikimpenda Mazrui sana.

Katika umri ule nilikuwa namsoma Kwame Nkrumah, "Challenge of the Congo."
Namsoma Nkrumah anavyochambua matatizo na fitna ya kampuni kubwa ya Wabelgiji - Union Miniere kwa Patrice Lumumba.

Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.

Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.

Hela zangu zilikuwa zinakwenda kwanza kwenye comics, ice cream, records na mwisho tiketi za cinema kuangalia movies Jumamosi mchana na Jumapili asubuhi saa nne Empire Cinema.

Mara yangu kumuona Prof. Mazrui ilikuwa miaka ya mwishoni 1960s Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sikumbuki ilikuwa kwenye sherehe gani na Julius Nyerere alikuwapo.
Nilikuwa nimefuatana na kaka yangu na rafiki yangu pia Shaabani Muhunzi maarufu kwa jina la Mkorofi yeye alikuwa mwanafunzi pale chuoni na nikimuusudu sana kwa hilo.

Shaaban alinitia hamu ya mimi kufika alipofika yeye.

Chumbani kwangu nilikuwa na ubao na ubao huu alinipa Abdallah Tambaza.
Hivi sasa Abdallah ni mwandishi nguli wa historia ya Dar es Salaam.

Shaaban akija chumbani kwangu mwisho wa juma akitokea Chuo Kikuu anakuta kwenye ubao juu kabisa nimeandika, "English Literature."

Chini yake patafuatia ''passages'' za William Shakespeare tena nikiziandika kutoka kichwani.

Yeye atafuta ataandika, "Literature in English," kunisahihisha bwana mdogo wake.
Akiondoka nitafuta na nitaandika kama nilivyoandika mwanzo.
Juma linalofuatia itakuwa mchezo ni ule ule.

Atanisahihisha mwanafunzi mkaidi na mwalimu wangu akiondoka nitafuta.

Sasa nimekuwa kijana wa kati Mazrui akatengeneza ile ''documentary'' maarufu sana, "Africans: A Triple Heritage."

Hapa ndiyo alinimaliza kabisa.

Nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Said Baamumin tukikaa jirani yeye akifanyakazi UNDP.

Siku moja akaniambia angependa kunipeleka kwao Mtondia Mombasa nikamuone mama yake.

Said Bamumin akanifahamisha kuwa wao wamejenga na wana mashamba katika ardhi ya ukoo wa Mazrui.

Tulipofika Mtondia akanipeleka Takaungu kuona msikiti wa Mazrui ambao una umri kiasi ya miaka 400 na kisima cha asili kipo hapo na bado kinatoa maji.

Ardhi hii ya ukoo wa Mazrui ina historia ndefu katika historia ya Kenya na Mombasa.
Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilimpelekea nakala mwalimu wangu na niliandika ''Kwa Mwalimu wangu wa Masafa Marefu Prof. Ali Mazrui.''

Hivi ndivyo nilivyofahamiana na Prof. Mazrui na tukawa tunaandikiana.

Nakumbuka baada ya kupata kile kitabu Prof. aliniandikia kunishukuru na akaniambia, ''Nimefurahi jinsi ulivyowaandika Waswahili.''
Miaka ikaenda.

Harith Ghassany ndiye yeye aliyenijulisha tena kwa Prof. Mazrui kwa staili nyingine kabisa.

Nilikuwa nimealikwa mkutano Kampala na Prof. Mazrui alikuwa na yeye amealikwa pia.

Nilipomfahamisha Harith akanipa salamu nimfikishie Prof. Mazrui.
Harith alisomeshwa na Prof. Mazrui University of Michigan.

Sote tulikuwa tunakaa Hilton Hotel.

Nilikuwa nimesimama kwenye ''lobby'' ya hotel kwa mbali nikamuona Prof. Mazrui anakuja upande wangu.

Aliponikaribia nikapiga hatua nikamtolea salamu.

Akaniitikia na alipoona ile tabasamu yangu hakupita akaniuliza, ''Tunafahamiana?''
Nikamwambia pia nina salamu zake kutoka kwa Dr. Ghassany.

Nilikuwa nimemtajia Prof. Mazrui watu wake basi akaniambia tukae kitako tuzungumze.

Nilimstaajabisha sana nilipomwambia kuwa nimefika hadi kwao Takaungu na tulizungumza mengi na haukupita muda jamaa wengi wakaja pale tukakaa na Prof. Mazrui na kuzungumzanae.

Mazrui ni mtu asiye na makuu mwepesi wa kuingilika.
Alizungumza na sisi kama vile ni watu tunajuana miaka.

Siku anaondoka kurudi Marekani kanikuta pale ''reception,'' kaja ku-''check out,'' na mimi nina ''check out,'' tukaagana.

Nakumbuka ''typical Mazrui trend,'' alimwambia Manager on Duty pale Hilton, ''Tengenezeni hizi lift kwani zinagoma sana na ikija Mmarekani kanasa kwenye hizi lift zenu atawapelekeni mahakamani.''

Sijui kama wenzangu waliokuwa pale walielewa lakini kwangu mimi ujumbe ulikuwa umefika sawia.

Nikamkumbuka katika ''The Africans: A Triple Heritage,'' anaonekana anafungua bomba la maji katika hoteli moja ya Nyota Tano katika mji mmoja mkubwa Afrika bomba linakohoa halitoi maji.

Mimi kwa tahadhari ile Prof. akawa kanikumbusha hoteli moja Lagos ndiyo nimefika nataka kukoga, nimefungua bomba la maji kwanza bomba likakohoa kisha maji yakaanza kutoka lakini rangi yake ilikuwa ya udongo rangi ya kahawia.



Na Prof. Ali Mazrui
Nile Hilton Kampala 2003
 
Ukishakuwa fanatic wa kidini kuna watu pia huko kwenye systems za kidunia vichwa vyao ni fyatu kwenye hayo mambo, wanaweza kukuchanganya tu kama extremist hatari wa kidini.
Yoda,
Hilo si tatizo kwangu.

Nadhani umesoma historia yangu na Wamarekani nikawekewa alama katika pasi yangu ya kusafiria.

Mwenyezi Mungu Mkubwa.
Nikaalikwa mkutano nchi moja ya Kiarabu.

Wakaniombea visa.

Wakaona kwenye pasi yangu kuna ile alama ya Wamarekani na hawa hawatoi pasi sharti kwanza wakupekue vyema.

Pakawa na mawasiliano ya ziada kuhusu mimi.

Jamaa wakawaeleza jamaa zao kuwa wao wananifahamu vyema na miaka ya nyuma nimeshaingia kwao na wakanitaja kuwa ni mwandishi wa vitabu kadhaa pamoja na kuwa mwandishi wa Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford Universty Press, New York.

Ile alama ikaondolewa na wao wenyewe US.

Wale walionajisi safina ndiyo hao hao wenyewe waliyoitoharisha safina.

System za dunia si fyatu.
Wewe unajisemea kwa kuwa huzijui.

Mimi nimepata uzoefu.
Zina watu wanazijua kazi zao.

Nilipofika mkutanoni jamaa akanifuata.

Akajitambulisha na kunipa ''good news.''

Haya ndiyo maajabu ya Allah.
 
Twende tu sawasawa, hizi ni takataka unazopotezea muda wako kuzibandika hapa.
 
Hivi na jamii nyingine kama Wachaga nao wakianza kudai "wazee wao" kama Thomas Marealle waenziwe sawa na Nyerere kupigania uhuru utakubali?
 
Kuna conmen wanatoka hadi vyuo bora kabisa duniani kama Havard, kwa sasa wako hadi katika mabunge yote mawili ya Marekani.
 

Kuna wacheza por**n nao hupewa tuzo,kwahiyo tuzo sio kitu cha kushangaza sana.
 
Siyo "kujari" ni kujali.

Amani ni jadi yetu Waislam, hata neno Uislam linaashiria salama na amani (peace).

Unataka kulinganisha pwani na kwa wakurya? Usitake kuchekesha watu.

.

Ajuza asante kwa kunirekebisha,amani haisemi kwa maneno bali kwa vitendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…