Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kalamu,Hapana, hatuwezi kamwe kuwa pamoja.
Wewe ni mtu wa 'taka', mimi takataka ni mwiko.
Niko na wewe hapa JF pamoja wa wengine wengi.
Sasa wamefikia 7K and counting...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kalamu,Hapana, hatuwezi kamwe kuwa pamoja.
Wewe ni mtu wa 'taka', mimi takataka ni mwiko.
Nipo hapa kwa sababu yako. Usisahau hilo.Kalamu,
Niko na wewe hapa JF pamoja wa wengine wengi.
Sasa wamefikia 7K and counting...
Kalamu,Nipo hapa kwa sababu yako. Usisahau hilo.
As long as you keep clicking 'reply' against my posts, I will stay with you. That's a promise.
Sawa. Nitavumilia hivyo hivyo hizi takataka zako hadi hapo tutakapofikia.Kalamu,
Hakuna tatizo mimi nataka ubakie na mimi.
Watu wengi wanatufatilia.
Nia yangu tugonge 10K.
Kalamu,Sawa. Nitavumilia hivyo hivyo hizi takataka zako hadi hapo tutakapofikia.
Hakuna shida kuziona takata nyingine.Kalamu,
Nilisimama kwa miezi 6 hapa JF miaka 10 iliyopita na faida kubwa niliyopata ni kuwa nilisomesha historia ya wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini wakafutwa.
Kwanza walidhani ni maskhara.
Kila siku zilivyozidi kusogea maswali yakawa yanabadilika wanauliza mbona historia hii hatukufundishwa?
Hapo nimewaeleza card no 1 ya TANU ni ya Territorial President JK Nyerere, No. 2 Ally Sykes, No. 3 Abdul Sykes, No. 4 Dossa Aziz ....
Kisha nasherehesha siku za mwanzo za usajili wa TANU watu watatu walihusika, Nyerere na Sykes Brothers Abdul na Ally na mikasa waliyokutananayo hadi kumtuma Said Chamwenyewe Rufiji kutafuta wanachama.
Butwaa lilikuwa kubwa sana.
![]()
Istanbul
Turkey
Kalamu,Hakuna shida kuziona takata nyingine.
Takataka sisomi, najibu tu lolote linalofaa kufuatana na takazilizobandikwa.Kalamu,
Kuna jamaa hapa sasa wameniomba niweke hapa ''serialisation'' ya kitabu changu chote cha Abdul Sykes kwa Kiswahili hapa.
Kuweka kitabu kizima hapa kidogo kidogo itachukua miaka.
Hivi ndivyo watu wanavyopenda elimu mpya kila siku.
Kuwaonjesha tu hiyo ya kadi wanataka kitabu kizima.
Darsa hii itafurika wanafunzi.
Kalamu,Takataka sisomi, najibu tu lolote linalofaa kufuatana na takazilizobandikwa.
leo ushaweka taka ngapi hapa? Najua unahesabu kufikia lengo lako.Kalamu,
Sikukusudii wewe usome.
Hii ni kwa ajili ya watu wanaofatilia mjadala huu ambao umekuwa wa upande mmoja.
Wewe maneno yako yanafamika.
Kisichofahamika na ndicho kitakachowavutia wasomaji kuja hapa ni kile nitakachoweka.
Hawa wasomaji wanasema niwarudishe hadi miaka ya 1950 kwa simulizi na kwa picha za nyakati hizo.
Nashindwa kuwakatalia.
Nimewaambia wapeane taarifa nipate wasomaji 100 katika saa 24 hadi kesho Maghrib In Shaa Allah tutaanza darsa.
Nia ni kufikia 10K In Shaa Allah.
Kalamu,leo ushaweka taka ngapi hapa? Najua unahesabu kufikia lengo lako.
Kuna u'con' zaidi ya huu?
Huko juu umezitaja, hapa "hujahesabu'!Kalamu,
Sijahesabu post ninazoweka lakini ngoja nijaribu nitakuwekea links:
![]()
Humburg
Kalamu,Huko juu umezitaja, hapa "hujahesabu'!
'Con-artist' wa kushangaza sana!
Takataka sisomi.Kalamu,
Naandika wakati wote si kama natania...
Nafanya rejea makala za nyuma wakati wote nachukua kitu mfano huo hapo chini:
FIKRA YA KUUNDA TANU
Kipi kilichopitika hadi historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ikaandikwa bila ya kuwataja wazalendo waliokwenda mbio Tanganyika ipate chama cha siasa idai uhuru wake?
Angalia picha hizo hapo chini:
Chief David Kidaha Makwaia, Hamza Kibwana Mwapachu, Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere.
Ukijua historia za wazalendo hao utaijua historia ya TANU kwa ukamilifu wake.
Nje ya historia za hawa huna historia ya kweli ya TANU.
Wazalendo hawa baadhi yao machifu wakubwa Aisha "Daisy" Sykes ameeleza amewaona akiwa bint mdogo wakija nyumbani kwa baba yake.
Itaendelea...
Kalamu,Takataka sisomi.
Hii ni akili ya kihalifu, kuwajazia JF takataka zile zile ulizokwishajaza humu na sasa kuzirudia tena mara kadhaa. Lakini hilo wataamua wenyewe kama wanaona kuwa ni sawa.Kalamu,
Hapana usisome hapa nina wasomaji 7K.
Nakushukuru kwa kunipatia hii fursa.
Bila wewe hili singewezekana.
Na hili limezua project nyingine, ''The Story of My Life in Pictures'' na sasa hii ya historia ya TANU simulizi na picha za nyakati ile.
Huwezi kuamini kuna publisher tena wa hapa nyumbani ananiombia kuna uwezekano wa wao kufanya kitabu cha historia shule ya msingi.
Ananiuliza kuhusu haki miliki hya picha.
Mimi sikutoi shukurani.
Unanifanyia hjisani kubwa.
Safi mzee wetu uko vzr ,ila uislamu inakusumbua sanaYoda,
Unaijua historia ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) na aliyofanya kuwapata vijana wasomi kupigania uhuru wa Tanganyika?
Soma hapo chini:
MWALIMU WA MWALIMU:
HAMZA KIBWANA MWAPACHU (1913 - 1962)
Balozi Mwapachu afichua barua ya Shujaa Hamza
Na Bakari Mwakangwale
BALOZI Juma Hamza Mwapachu, ameiweka hadharani barua ya baba yake Mzee Hamza Kibwana Mwapachu, aliyomwandikia Mwalimu Julius K. Nyerere, mwaka 1949.
Barua hiyo imewekwa hadharani Watanzania wakielekea kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadae Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere, aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999.
Akizungumzia barua hiyo, mtafiti na mwandishi wa vitabu vya historia sahihi ya Tanganyika, Mohammed Said Salum, amesema barua hiyo karibu sasa itafikia miaka 70, tokea kuandikwa kwake.
Akitoa maoni yake Mohamed Said, alisema anadhani sababu ya kuiweka barua hiyo hadharani wakati huu, pengine ni kutaka kuwazindua Watanzania kuhusu kupotoshwa kwa historia ya wananchi wa Tanganyika katika kujikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni wa Waingereza.
“Kumekuwa na tatizo kubwa katika kutafiti na kuandika kwa usahihi historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika, sasa naona Balozi Juma Mwapachu ameiweka hadharani barua ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu (1913 1962) aliyomwandikia Julius Nyerere, mwaka wa 1949, ili pengine kulizindua Taifa.
Amesema Mzee Said.
Akifafanua Mohamed Said amesema, mengi yaliyoandikwa kuhusu historia ya Tanganyika, yamemtaja Julius Nyerere, peke yake kiasi cha kufanya iaminike kuwa kabla yake hapakuwa na wanasiasa wala hapakuwapo na watu waliofanya juhudi zozote za kutaka kuikomboa Tanganyika kutoka kwa wakoloni, isipokuwa Mwalimu Julius Nyerere peke yake hali iliyopelekea nchi kukosa kuwatambua mashujaa wake.
Alisema, barua hiyo imedhihirisha ukweli kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika, ipo katika vichwa vya watu na wengi wao wameshatangulia mbele ya haki na hata nyaraka nyingi zinazoonyesha mawasiliano ya kudai uhuru wakati huo pia zipo mikononi mwa watu binafsi.
Aidha Mohamed Said alisema, barua hiyo pia imefungua mlango na kuwawezesha watafiti wa historia ya Tanganyika kuchungulia ndani kusoma na kufahamu nini Mzee Hamza Mwapachu, alikuwa anasema kumwambia Mwalimu Nyerere, katika mipango ya kudai uhuru wa Tanganyika.
“Barua hii ni muhimu na kwa haraka iwekwe katika Makumbusho ya Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo na naamini katika Maktaba ya Mh. Balozi Juma Mwapachu, yapo mengi mbali na aliyohifadhi kichwani kwake."
Amesema Mzee Said.
Akasema, Mtafiti yeyote katika historia ya uhuru wa Tanganyika, kama atakuwa makini hatoweza kumuepuka Mzee Hamza Mwapachu, kwani ni vigumu kumtaja Mwalimu Julius Nyerere na usimtaje Mzee Hamza Mwapachu.
Akiizungumzia barua hiyo alisema, hiyo (barua) ni matokeo ya barua ambayo Mwalimu Nyerere, alimwandikia Mzee Mwapachu, kuhusu mambo muhimu waliyozungumza siku za nyuma.
Alisema, katika barua hiyo, Mzee Mwapachu, ameorodhesha moja baada ya jingine katika yale waliyozungumza ambayo ni ''Trusteeship as compared to Protectorate and Mandate, White Paper 191, White Settlement in Tanganyika.''
Anafafanua zaidi Mohamed Said kuwa, katika ukurasa wa kwanza katika barua hiyo yenye kurasa tatu, unaonyesha mambo manane lakini kwa uchache ameyataja hayo matatu ambayo (kwa Kiswahili) ni udhamini wa Tanganyika chini ya Waingereza, Mjadala wa Afrika Mashariki na Ukazi wa Wazungu Tanganyika.
“Haya yalikuwa mambo mazito, makubwa na ya kuzungumzwa kwa siri sana baina ya Waafrika, sasa inawezekana vipi historia kama hii ikaachwa ipotee hivi hivi tu?''
Amesema na kuhoji mwanahistoria Mohamed Said.
Alisema, jambo la kusikitisha ni pale inapojaribiwa, ingawa kwa kuchelewa kuwaenzi mashujaa walio pambana na ukoloni, hujitokeza maswali mengi, ambayo hakuna awezaye kuyajibu kwa uhakika na kwa ithibati ya kuaminika.
Mathalani, akahoji kuwa inawezekana vipi kutolewa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Abdulwahid na Ally Sykes, (ndugu wawili) waliokuwa kati ya waasisi 17 wa TANU, ukawaacha waasisi wengine kama Saadan Abdul Kandoro na Japhet Kirilo (kwa kuwataja wachache).
Mohamed Said akasema, itoshe tu kueleza kuwa medali hizo zimetolewa kwa kuchelewa miaka 50, kwani Ally Sykes, kapokea medali yake akiwa katika mwisho wa maisha yake akiwa mgonjwa, miaka miwili kabla ya kifo chake mwaka 2013.
“Lakini swali linakuja, vipi utawapa medali mashujaa hawa wa uhuru usimpe medali Mzee Hamza Mwapachu, ambae ushahidi wa historia unaonyesha kuwa ndiyo alikuwa, "mentor," wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abdul Sykes?”
“Hawa wote waliokuja kudai uhuru katika nafasi zao tofauti na baada ya uhuru kupatikana wakaja kuwa viongozi wa Tanganyika huru."
Amesema Mzee Said.
Akichimbua zaidi kumbukumbu ya historia alisema kuwa Dr. Vedasto Kyaruzi, alipata kumwambia Juma Mwapachu, kuwa kama si mpango waliouweka Hamza Mwapachu na Abdul Sykes, basi Tanganyika isingepata uhuru wake mwaka wa 1961.
“Dr. Kyaruzi, akaongeza kwa kumwambia Juma Mwapachu, kuwa kule Nansio Kisiwani, alikopelekwa baba yake na Waingereza, ile ilikuwa ni jela ya kumtia kizuizini ili kumzuia asishiriki katika siasa.”
Akasema, wazalendo hao ndio waliochora ramani ya njia ipi ichukuliwe kuidai Tanganyika na kuitoa katika mikono ya Waingereza kwa salama.
Mohamed Said, akasema kwa wale waliokuwapo katika 'circle’ ya kupambana na Waingereza hakuna ambae hakuwa anajua kuwa Hamza Mwapachu, ndiye aliyekuwa akisukuma mambo nyuma ya pazia.
Alisema, kazi hiyo aliifanya iwe yuko Nansio au Rungwe, sehemu ambazo ni za mbali alizotupwa na wakoloni ili asiwasumbue kwa kumtoa karibu na miji mikuu ambako ndiko yalipokuwa mashina ya kupinga ukoloni.
![]()
Kulia: Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) na Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962)
Dr.Safi mzee wetu uko vzr ,ila uislamu inakusumbua sana
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kalamu,Hii ni akili ya kihalifu, kuwajazia JF takataka zile zile ulizokwishajaza humu na sasa kuzirudia tena mara kadhaa. Lakini hilo wataamua wenyewe kama wanaona kuwa ni sawa.