Ni kwa namna gani wazazi wanaweza kudhibiti matumizi ya simu kwa watoto wao ambao ni wanafunzi

Ni kwa namna gani wazazi wanaweza kudhibiti matumizi ya simu kwa watoto wao ambao ni wanafunzi

Mr Mlokozi

Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
21
Reaction score
16
Wazazi wengi wamekuwa wakiwapatia simu watoto wao kwa lengo zuri tu la kufanya mawasiliano na familia na marafiki zao pamoja na wanafunzi wenzao pia, wakati mwingine kwa ajili ya kujifurahisha kwa kucheza michezo mbalimbali iliyomo kwenye simu pamoja na kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.

Kutokana na hatua ya ukuaji, vijana hawa wanakuwa katika hatua ya balehe ambayo inawafanya wawe wadadisi sana wa mambo ambapo mengi katika hayo huwa si mazuri kimaadili kutokana na mihemko ya mwili. Basi hutumia simu hizo kushirikiana na vijana wenzao kufuatilia mambo yasiyofaa, mfano kuangalia picha za ngono na kurasa zenye maadili yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo basi, ni kwa namna gani wazazi wanaweza kufanya ili kudhibiti matumizi ya simu yasiyofaa kwa vijana wetu ili kuepuka kutengeneza kizazi kisichokuwa na maadili?

Je, kutowapa simu ni sahihi hasa ukizingatia maisha haya ya sasa ya utandawazi?
 
Back
Top Bottom