Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Usiku Unatosha sana kupumzisha akili na mwili
 
Cha msingi ni kumuabudu Mungu wa kweli.

Dhehebu, siku ya kuabudu (Jmosi, Jpili n.k) sio tiketi ya kwenda mbinguni.

Aidha, siku ya sabato ni ipi hasa?. Siku ya kwanza katika juma ni ipi?, siku ya saba ni ipi?, yaani ni jumaa ngapi?.
Sabato ina lengo kuu la kupumzika na ndio asili ya neno lake shabaat, Tunajumuika pamoja na kufanya shughuli za kumuabudu Mungu ikiwa kama kumshukuru

Siku ya Sababto ni Ijumaa dakika chache kabla ya jua kuzama hadi Jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, ndio maelekezo aliyopewa Musa na Mungu aliempa amri 10 ikiwemo ya kuabudu siku ya sabato.
 
Inaabudiwa siku au mtu anaabudu kwenye siku hiyo? Pia Yesu alisema kuanzia sasa waabuduo halisi wataabudu kwenye roho na kweli. Siku haikuwekwa kama kigezo cha kuabudu halisi.
Sabato ni siku rasmi tuliyoruhusiwa kupumzisha miili na akili kutoka kwenye kazi tunazozifanya, Nasi tunamshukuru Mungu kwa kujumuika pamoja katika shughuli za kumuabudu ili kumshukuru, huwezi kupumzika kila siku
 
Aliyekuwepo kushuhudia anapewa hizo amri ni nani? Hizo unazoziita amri ni taratibu zilikuwepo almost kwenye jamii zote labda kwa utofauti kidogo kulingana na mila na desturi.
Si kila kitu kimeandikwa hata Fimbo ya Musa hatujui ilikuwa ni ya mtu gani, Hata Yesu hatuijui miujiza yote aliyoifanya wala mahubiri yake yote, n.k.

Amri kumi hazikuwepo kila jamii, baadhi ya jamii mfalme akitamani mke / mali yako unasifiwa na inabidi umpe, Kuiba kuliruhusiwa kuonyesha mvulana kawa mwanaume, kubudu shetani ili kuroga, kuua watoto walemavu kwa kuamini kunaondoa mikosi, n.k;
 
"Kwasasa ni ijumaa" alisema Musa?
Kwahiyo Musa alisema siku ya saba ni Jumamosi
Mfumo wa kuhesabu siku upo tangu zamani ikiwa siku ni nuru na giza kupita isipokuwa hazikuwa na majina ya sasa kama Ijumaa na Jumamosi ndio mana huwezi kukuta majina hayo kwenye biblia na hata mfumo haukuwa kama sasa wa kuanza siku mpya saa sita usiku.

Kwa mfumo waliotumia enzi hizo za Musa, Kipindi cha Yesu na mpaka sasa ukienda Israel, Siku ya Sabato imeangukia dakika chache kabla ya jua kuzama kwenye siku tunayoiita kwa sasa Ijumaa mpaka Jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, baada ya hapo inaanza siku ya kwanza upya.

Aliepanga hivyo ni Mungu aliempa Musa Amri 10 ikiwemo siku ya kuanza kuitekeleza hio amri, Hata Yesu alipokuja aliitambua, aliiabudu, aliisifia na kuitetea soma Marko 2.
 
Kama si kila kitu kimeandikwa unapinga nini sasa. Yaani hata hiyo biblia tu huijui vyema, hujasoma kisa cha mfalme aliyemtamani mke wa askari wake na kumpeleka vitani mstari wa mbele ili auawe na yeye arithi mke.
Hayo yote uliyoyataja hakuna jamii au utamaduni uliwahi kuyaruhusu. Hilo la kuabudu shetani ilikuwa ni upumbavu wa wazungu kushindwa kuelewa desturi na taratibu zetu za kumuabudu Mungu. Leo wanaovaa rozari na madude mengine ya hizo dini wanafanya hivyo kwa nini.
Sina nia ya kuwa sehemu ya aina hii ya mijadala.
 
Nyie ndio mmefungwa akili kwa ujinga wenu. KWA HIYO HUYO MCHUNGAJI WAKO NDIO ALIKUDANGANYA SABATO NI JUMAMOSI?
 
Basi hata wanaosali jumapili/Ijumaa hio ndio sabato yao! Kusali Jumamosi hakuna uspecial wowote ambao wanaosali jumamosi wanao... Sabato si siku ya mapumziko iwe juma3 jumamosi yote heri madamu mmeitakasa iwe siku ya bwana.
 
Wasabato walimuua Yesu ili wasali KWA uhuru jumamosi yao Yesu akiwa kaburini
Kama Yesu alifufuka jumapili na ndio siku ya Bwana wa Sabato
Ndio siku ambayo Bwana alikuwa na furaha ya kuukomboa ulimwengu
Mt. Paulo alifafanua vizuri sana hili; kwamba, kama Kristo asingalifufuka, imani yetu ingalikuwa bure! Bali Kristo amefufuka (siku ya kwanza ya juma), limbuko lao waliolala (kufa).

Tena imeandikwa; siku ile (ya hamsini baada ya kufufuka Bwana - Jumapili) almaarufu kama Pentekoste wanafunzi wakajazwa Roho Mtakatifu wakamwabudu Mungu katika roho na kweli - ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Katika historia ya ukombozi wa mwanadamu; iwe wa-Israel kutoka Misri, au kutoka Babeli, hakuna yanayozidi hayo mawili kwa ukuu - ufufuko wa Bwana; ubatizo wa Roho Mtakatifu!

And fortunately; hakuna lililotokea Sabato ya kimwili. Pasingekalika hapa!
 
Kifo cha Yesu ndio ilikuwa mwisho wa sheria, na hata zile kanuni za siku ya sabato hakuna hata msabato mmoja anayezifuata
ngoja nije nikubake maana sheria hazipo jiandae...πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜†
 
Ndiye

Musa aliepewa amri 10 kutuletea, akiwa huko patakatifu, alielekezwa sabato iwe jumamosi na ikawa hivyo
Embu niambie kwa alie marekani siku ya jumamosi ndivyo iko kwa alie Australia, India ana unchina? Sabato hasa sio siku maana kama ingekua siku ingebidi nchi zote ziwe na siku moja ya jmosi, ila si hivyo utofauti wa Masaa unaonyesha wazi mapokeo ya siku ya jmosi sio sahihi, maana siku ya jmosi ya israel ni tofauti na ya marekani na unchina na Tanzania.
Sabato ni siku yeyote utakayoitenga kumwabudu Mungu wako.!

Achaneni na msingi ya walio Leta dini, soma neno la Mungu kwa mafunuo ya Roho Mtakatifu na hato fungwa na yeyote, maana kila dini inamambo yake inayoona bora kuliko nyingine... Na matokeo yake dini hizi zinaleta utofauti baina ya Mkristo na mkristo.. Huyo dini si kitu cha kujali kama kujali Roho Mtakatifu anae mshujudia huyu Kristo ambae sote tuwafuasi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…