Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA nasi tunamshukuru kwa kujumuika kwenye shughuli za kumshukuru na kumuabudu kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kupumzika, kazi nazo muhimu.
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 inaanza upya siku ya kwanza, Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa majina ya kisasa ya siku huanza Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, ndio maana huwezi kukuta neno jumamosi wala ijumaa kwenye biblia.
Hata Yesu aliikuta, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi mpaka sasa ukienda Israel siku ya jumamosi wanaabudu Sabato maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.
Yesu anaweza kuwa Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito lakini siku ya sabato tunahitaji pia pumziko la mwili, akili, n.k.