Sisi wenyewe ndiyo tunajidharau kwanza, timu zetu bila kutumia kocha mzungu tunajiona hatuwezi. JPM alituamsha kwamba tunaweza. Tabia zetu ni tofauti na wengine. Wenzetu wanawekeza sana kwenye tafiti na zinafanyika ki kweli. Sasa uje siye ipe taasisi pesa za utafiti, itaishia kwenye mifuko ya watu, kwa nini tusibaguliwe.
Ugonjwa wa malaria mpaka leo unatushinda. Wakati huo huo ukimpa hii nchi au bara zima mzungu haipiti miaka miwili malaria kwisha. Siyo kwamba hatuwezi ila tabia ya kuchopoa/ kuiba pesa za tafiti ndiyo ugonjwa wetu. Kwa nini tusibaguliwe?
Miradi mingi inatushinda kuiendesha au kuifanya kwa sababu ya uroho wa pesa binafsi na wizi. Kwa nini tusibaguliwe?
Unafunga pump ya maji kwa ajili ya wanakijiji ili wapate maji, inaibiwa na hao hao. Kwa nini tusibaguliwe?
Serikali inatoa dawa za bure kwa hospitali zetu, zinaibwa na hao hao watoaji. Kwa nini tusibaguliwe?
Mwizi wa mali ya umma anaonekana mjanja mbele za jamii, na jamii inamuona wa maana. Kwa nini tusibaguliwe?
TUJITHAMINI WENYEWE, TUJIPENDE WENYEWE, KURITHIKA NA KILE UPATACHO, TUPUNGUZE UBINAFSI ILI NA SISI TUONEKANE BINADAMU TULIOSTAARABIKA NA WENYE AKILI ZA KUZALIWA MBELE ZA BINADAMU WENGINE.